21/11/2025
Yaliyojiri Siku ya Ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu Tanzania 2025, Maktaba Kuu.
Umoja wa Waandishi wa Vitabu Tanzania ulipata fursa ya kushiriki maonesho haya ya kimataifa ya vitabu nchini yaliyoandaliwa na umoja wa Wachapishaji Vitabu Tanzania (PATA). Mgeni Rasmi akiwa ni Mheshimiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi.
Mgeni rasmi alipata nafasi ya kutembelea banda la UWAVITA - banda namba 12 na kupelekea vitabu vya waandishi wa UWAVITA kutia fora! Pamoja na vitabu vyengine, palikuwa na "Kamusi ya Kisumbwa-Kiswahili-Kingereza ya Prof. KK Kahigi", kitabu cha Ushairi cha Omary Baajun "Olives, Watermelon & Kufiyyeh: Poems for Palestine", pia kitabu cha "Rafiki yangu Kipepeo" cha Gwiji Hussein Wamaywa alivyopewa k**a zawadi.
Kwa upekee kabisa aliguswa na vitabu vya Nukta nundu akisema, aliwahi Kusoma na wanafunzi wenye changamoto ya uoni, hivyo kupatikana kwa machapisho hayo ni jambo zuri.
UWAVITA ilipata dakika chache za kusema jambo kuhusu Umoja wetu. Mheshimiwa Waziri amepongeza sana juhudi za waandishi katika kuandika na kuchapa machapisho.
Aidha, kwa upekee kabisa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi alimpa maua yake Mwalimu Richard Mabala, ambaye ni mwanachama na miongoni mwa walezi wa UWAVITA.
Mwenyekiti wa PATA naye alitoaa maombi kadhaa:
- Isaidie uuandaaji wa Sera ya vitabu na usomaji wa vitabu Tanzania.
- Udhamini wa kudumu toka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Wizara ya Elimu.
- Uwezeshwaji wa Wajumbe kutoka Tanzania katika Maonesho ya Vitabu Duniani.
- Ipitishe vifaa vya tozo ya vibebeo vya kazi za machapisho.
- Ukumbi wa Maonesho ya Vitabu katika Sports Arena.
- Maktaba ya Kimataifa ya Kiswahili na Duka la vitabu.
Imetolewa na;
Ofisi ya Katibu Mkuu
UWAVITA