Lusifa_Kuzimu_Tz_Waabudu Shetani

Lusifa_Kuzimu_Tz_Waabudu Shetani Sisi Ni Jamii Kubwa Ulimwenguni, Sisi Ni Occultists (Wajuzi Wa Elimu ya Siri), Waponyaji, Wanajimu,W

MAAGIZO YA LUSIFAIV MAMA WA GIZANimeamka ndani ya roho yake inayojizungusha,Nikiwa nimeangaziwa kwa damu na moto.Yeye nd...
27/04/2026

MAAGIZO YA LUSIFA

IV MAMA WA GIZA

Nimeamka ndani ya roho yake inayojizungusha,
Nikiwa nimeangaziwa kwa damu na moto.

Yeye ndiye anayenikamilisha kikamilifu,
Kile kinachosukuma asili yangu na kuamsha roho.

Mahali pake pa siri pa uwepo ni wa milele.
Mama wa Maada/mwili ni Bibi-arusi wangu,
Kwa maana tutaamka ndani ya chumba chenu cha ndoa,
Ambamo kaburi hubadilika kuwa Hekalu la Mpinzani (satan).

Yeye amewazaa malaika wangu.
Yeye aitwaye Onorthochrasaei ni Mama wa Mapepo,
Wale wa roho yangu walioasi dhidi ya udhaifu.
Anawalisha ndani ya mwili.

Phloxopha hutawala joto la mwili,
Akilishwa na Moto Mweusi na asili yake.

Oroorrothos ni roho iliyo ndani ya mwili inayotawala baridi.
Pepo linalotawala ukavu ni Erimacho,
Na linalotawala unyevunyevu ni Athuro.

Wanajulikana kwa majina mengi.
Mapepo wakuu wanne wa kale ni:
Ephememphi, wa starehe—
Kile kinachochochea na kuridhisha… usikatae starehe, bali iwe na nidhamu.

Yoko, pepo wa tamaa—
Jua hili kwa jina jingine:
Hutawala tamaa yako, ielekeze kwenye akili na mantiki,
Na iridhishe roho.

Nenentophni, pepo wa huzuni—
Kuwa mwangalifu na roho hii,
Kwa kuwa itachukua zaidi kutoka kwako kuliko utakavyopata kutoka kwake.

Jiruhusu kwa kiasi katika roho na mwili,
Usiruhusu mwili kuwa mtego,
Wala akili au roho kufungwa na hali hiyo.

Yeye huongoza kwa silika
Na yale yanayojulikana kimya kimya.
Yeye ni taji la nyoka anayeshambulia kwa ajili ya chakula.

Yeye ni taya za mnyama mla mawindo anapong’ata ili kuishi.
Yeye ni msuguano wa wapenzi wanapotuliza hamu yao.

Mama wa Giza anaishi katika kila mwili,
Lakini hupatikana kwa roho, kwa maana yeye ni Bibi-arusi wangu.
Ni kupitia kwake pekee ndipo naweza kupatikana.

Mama amefungua jeraha lake mbele yetu,
Likisikika k**a mwangwi wa kaburi.

1. “Mama wa Giza” ni nini?

Hapa “Mama wa Giza” si lazima awe kiumbe halisi, bali ni nguvu ya ndani ya asili (primordial force)—chanzo cha uhai, hisia, mwili, na silika. Ni upande wa ndani ambao mara nyingi hufichwa: tamaa, hofu, nguvu ya ubunifu, na mabadiliko.

Ni k**a:

chanzo cha uhai (creation)

giza linalozalisha mwanga (transformation)

nguvu ya k**e ya ndani (divine feminine / receptive force)

2. “Bibi-arusi” na “ndoa” vina maana gani?

Hii inaashiria muungano wa nafsi mbili ndani ya mtu mmoja:

akili (logic, consciousness)
silika/ndani (instinct, subconscious)

“Chumba cha ndoa” ni eneo la ndani (inner state) ambapo mtu anakubali na kuunganisha pande zote mbili.
Ndipo “kaburi linakuwa hekalu” — yaani:
kile kilichokuwa giza au hofu kinageuka kuwa chanzo cha nguvu na uelewa.

3. “Mapepo” na “malaika” hapa ni nini?

Hawa si viumbe wa nje, bali ni nguvu za kisaikolojia ndani yako:

Mapepo = silika nzito (tamaa, huzuni, raha, maumivu)

Malaika = uwezo uliokua baada ya kushinda udhaifu
Mfano:
tamaa (desire) inaweza kukuangamiza au kukuongoza

starehe (pleasure) inaweza kuwa utumwa au nguvu

huzuni (grief) inaweza kukuangusha au kukupa hekima

4. Vipengele vinne au elementi nne za msingi (joto, baridi, ukavu, unyevunyevu)

Hivi vinafanana na falsafa za kale (k**a vile alkemia au tiba za zamani)
Vinawakilisha mizani ya mwili na roho:

Joto ni nguvu, msukumo

Baridi ni utulivu, kuzuia

Ukavu ni uthabiti, mipaka

Unyevunyevu ni hisia, mabadiliko

Ujumbe: uwe katika usawa (balance)

5. Ujumbe mkuu wa maandiko haya
Kiini chake ni hiki:

Usikimbie upande wako wa giza
Uuelewe, uukubali, na uutawale
Badala ya kupigana na tamaa, huzuni, au raha zitumie kwa hekima

Nidhamu + ufahamu = nguvu

Ndiyo maana inasema:

“Usikatae starehe… bali iweke chini ya nidhamu”

6. “Kupatikana kupitia yeye” ina maana gani?

Hii inaonyesha kuwa:
huwezi kujijua kikamilifu bila kukubali upande wako wa ndani
ukweli wa nafsi yako hauko kwenye mwanga tu—bali pia kwenye giza
Kwa lugha rahisi:
👉 Ukikimbia giza lako, hujijui-huwezi kujitambua. Ukilikubali, unapata nguvu.

Maandiko haya yanaelezea safari ya ndani ya kujitambua (inner awakening) ambapo mtu:
anakutana na upande wake wa ndani (giza)
anaujenga kuwa nguvu
na hatimaye anafikia hali ya juu ya ufahamu.

LUCIFERIAN PATH. THE LEFT HAND PATH.

MWENDESHA GARI LA FARASI NA WALINZI WA NAFSI.Katika alama ya kale ya Gari la Farasi (Chariot), Ushindi si juu ya ulimwen...
02/04/2026

MWENDESHA GARI LA FARASI NA WALINZI WA NAFSI.

Katika alama ya kale ya Gari la Farasi (Chariot), Ushindi si juu ya ulimwengu, bali ni juu ya nafsi ya mtu yeye mwenyewe. Farasi wawili wanao vuta gari hilo...ambao mara nyingi huonyeshwa wakiwa na rangi na tabia tofauti..wanawakilisha akili ya Juu na akili ya chini; matarajio makubwa ya juu na tamaa; akili iliyo tiwa nuru/akili iliyoangaziwa na hamu isiyodhibitiwa. Mwendesha Farasi hatakiwi kumuua farasi yeyote, wala hatakiwi kuachia kamba za kuwaongozea; badala yake anatakiwa kuwatawala wote kwa mapenzi thabiti, kwasababu maendeleo/kukua huzaliwa kutokana na uwiano, si kwa kuharibu ama kwa kukandamiza sehemu fulani ya Nafsi.

Vivyohivyo, karika Uashi-Huru (masonry) , mafundisho haya yamefichwa ndani ya majukumu na ulinzi wa ofisi mbalimbali.

Mlinzi wa ndani (Inner Guard) na mlinzi wa nje (Outer Guard) husimama k**a walinzi wanao fafanua ama wanao rejelea siri moja/fumbo moja: mlinzi wa ndani hulinda mawazo na nia za ndani, na mlinzi wa nje hulinda matendo na mwenendo wa nje. Wote wawili wana umuhimu; na wote wawili wanaweza kuwa hatari endapo hawatodhibitiwa. Ndio maana huwekwa chini ya mamlaka ya "Junior Warden", ambaye jukumu lake ni kudhibiti hisia na tamaa, na kuweka uwiano kati ya kazi na mapumziko.

Yule anayetaka kusonga mbele katika njia hii ni lazima ajifunze siri hii ya kujitawala: kuunganisha mbingu na dunia ndani yake yeye mwenyewe, na kuendesha gari la farasi si kwa kutumia nguvu bali kwa uelewa.

NDIPO MILANGO YOTE ITAFUNGUKA NA GARI (LA MAISHA) LIINASONGA MBELE
ISHI KWA UWIANO, USAWA,MAELEWANO NDANI YAKO MWENYEWE NA ULIMWENGU

ISHI KWA UWIANO NA MAELEWANO NA MAPEPO NA SI KUSHINDANA NAO, MWISHONI WATAKUONYESHA NJIA YAKUTOKA.

NAAMAHMkono wa Lilith.Katika mafundisho ya siri ya Uyahudi yaani Kabbalah hasa katika kitabu cha Zohar, Lilith ametajwa ...
21/03/2026

NAAMAH

Mkono wa Lilith.

Katika mafundisho ya siri ya Uyahudi yaani Kabbalah hasa katika kitabu cha Zohar, Lilith ametajwa k**a Pepo wa k**e wa ngono (Succubus). (Naamah) akiwa pamoja na Lilith inaelezwa kwamba walimshawishi Adamu na hatimaye kuzaa naye viumbe na maafa yote yanayo leta mateso kwa wanadamu.

Naamah: ni pepo mwenye nguvu kubwa (succubus) na mtawala wa Qliphoth, yaani mwangaza hasi au maumbo mabaya ya Ayin, kutoka katika tabaka za chini kabisa za Jehanamu.

MUHTASARI KWA UFUPI

NAAMAH ni pepo wa k**e anayetajwa katika (kitabu) cha Zohar, ambapo ni mojawapo ya vitabu muhimu katika mafundisho ya siri za mafumbo ya kiyahudi. Inaelezwa kwamba alimshawishi na kumpenda malaika aitwaye Shamdon, na kwa pamoja walimzaa Asmodai (Asmodeus). Yeye ni pepo anayehusiana na ngazi za chini za tufe ya Qliphoth hasa katika eneo linalolingana na Malkuth, na mahali ambapo Shekinah na Sandalphon wanahusishwa.

Naamah pia anajulikana k**a "Mama wa uaguzi": au "Mshawishi":. Mwonekano wake unafanana na Lilith ambapo inaelezwa kwamba ni mrembo sana, mwenye mvuto wa kimwili, na aliye wapotosha Malaika walinzi walio anguka wakiongozwa na Samyaza.

Mapepo wenzake wa k**e wake Naamah ni k**a vile Lilith, Eisheth Zenunim, na Agrat Bat Mahlat. Mapepo hawa wanne kwa pamoja hujulikana k**a "mashetani ama Mapepo wakuu wa Tamaa na Malikia wa Anasa".

Naamah anatajwa k**a mmojawapo miongoni mwa Malaika wanne wa Uasherati. Anatajwa pia kuwa miongoni mwa wake au mke mwenza wa Pepo Samael ambaye ni Mama wa Asmoday, na ni mmoja kati ya Malikia wa Jehanamu akitawala upande wa Mashariki (Damascus).

Kwa mujibu wa Zohar, baada ya kaini kumuua Abel, Adamu alijitenga na Hawa kwa miaka 130. Katika kipindi hicho (cha upweke), Pizna na Naamah walimtembelea Adamu na kuzaa naye watoto wa kipepo walio kuja kuwa mateso kwa wanadamu. Naamah pamoja na Mapepo wenzake wanahusishwa kusababisha kifafa kwa watoto.
Naamah anatajwa kuwa amewahi kuingia katika mapenzi na Malaika, Mapepo, na mashujaa wengi mashuhuri katika Biblia. Naamah amewahi kuwa mke wa malaika na mapepo mbalimbali akiwemo Az**el, Samael, Samyaza, Sulemani na Nuhu na huenda pia amewahi kuwa na mahusiano na mtoto wake yeye mwenyewe. Watoto wa Naamah inaelezwa kuwa ni Wanefili/Nephilim, Shedim, na Ashmodai.

Kiroho, Naamah anawakilisha uhuru wa kijinsia wa mwanamke na ibada takatifu ya hisia za Mwili. Anatawala mahali ambapo ngono, furaha ya kiroho, na muziki vinakutana. Wanaotambua hali hiyo na kuitafuta huonekana kuwa wapo chini ya ulinzi au chini ya mvuto wake.

MUONEKANO WA NAAMAH

Katika umbo lake la kweli, Naamah ni pepo wa kutisha sana na huitwa "binti wa giza". Ana ngozi ya kijivu, macho meusi kabisa, na uso wa mwanamke aliye katika maumivu ya kudumu. Sehemu ya juu ya mwili wake ni ya mwanamke, huku sehemu ya chini ya mwili wake ni Nyoka. Katika hali hii, urefu wake hufikia takribani mita 9.

TABIA ZA NAAMAH

Kuna taarifa chache sana zinazo julikana kuhusu tabia za Naamah. Hatahivyo, inaelezwa kwamba baada ya Adamu na Hawa kutengana, Naamah aliishi na Adamu kwa miongo kadhaa, jambo linalo onyesha kuwa tayari Naamah alikuwa na hisia kwake hata kabla ya Anguko la Adamu.

NGUVU NA UWEZO WA NAAMAH

Kwakuwa Naamah anaelezwa kuwa ni Pepo, Ni malaika aliye anguka, Pepo wa ngono (Succubus), na vile vile pia ni binadamu, kutokana na hilo inaelezwa kwamba Naamah anauwezo wa kujibadili maumbo na sura au asili yake vile apendavyo.

HISTORIA YA NAAMAH

Mwanzoni kabisa inaelezwa kwamba, Naamah alikuwa ni mwanamke binadamu aliye umbwa na Mungu kwa ajili ya Adamu, pamoja na wanawake wengine k**a vile Agrat na Eisheth, waliumbwa kuwa k**a wake zake watarajiwa. Adamu alipowachumbia, wote walimkataa, isipokuwa Lilith. Naamah na dada zake waliondoka, wakisindikizwa kupelekwa nje ya Bustani ya Edeni na Malaika Uriel.

Baada ya Lilith kuanguka, Naamah na Lilith waliishi karibu na Bahari nyekundu hadi pale walipo fukuzwa na Mungu. Kabla ya vita vya mbinguni, Belzebub alimkuta Naamah akiwa amelala kando ya bahari, akavutiwa kimapenzi naye, na wakafanya muungano wa kimwili yaani tendo la ndoa. Baada ya vita hivyo na anguko la mwanadamu , Naamah akaja kuwa Malkia wa Mapepo pamoja na dada zake, na huku mpenzi wake Samael, akitawala eneo la Mashariki (Damascus).

Pia Naamah anatajwa kuwa ni binti wa Lameki, ingawa namna na jinsi alivyo geuka kuwa pepo haijaelezwa wazi.

UHUSIANO WAKE NA ADAMU.

Baada ya Anguko la Adamu na mauaji ya Abeli, Hawa alimtenga Adamu kwa miaka 130. Katika kipindi hicho, Naamah alijitambulisha k**a "rafiki" wa Adamu, na kuwa mpenzi wake kwa muda mrefu. Walizaa watoto wengi, ambao baadaye walitajwa kuwa mateso kwa wanadamu.

ANGUKO LA MALAIKA WALINZI (THE WATCHER OF HEAVEN)

Inaelezwa kwamba, Naamah aliwapotosha malaika Samyaza na Az**el, pamoja na wanawake walio itwa Nashiym. Kupitia muziki na uchawi wa mvuto wa kiroho, walibadilisha sura na roho za wanawake, hata Malaika wakavutiwa. Kwa njia hii, Malaika walinzi wakajiingiza katika tamaa na maovu, jambo lililo kuja kusababisha uharibifu mkubwa duniani. Naamah alitoroka kabla ya kuwasili kwa Malaika wakuu, na hivyo akaepuka ghadhabu ya Mungu karika gharika kuu.

HADITHI YAKE NA MASILIZI YAKE

Jina Naamah kutoka katika neno la kiebrania linamaanisha "mpendeza" "mzuri" "mwenye kupendeza/mwenye mvuto". Jina Naamah limetajwa katika Mwanzo 4:22. Ambapo Naamah ametajwa k**a dada wa "Tubal-Kaini na binti wa Lameki. Ambapo pia "Tubal-kaini ni mtu muhimu mno katika historia ya Freemasonry.

Talmud ya wayahudi inaeleza kwamba, Naamah alkuwa ni mwanamke mwenye kipaji cha muziki na uaguzi, aliye wapotosha wanadamu kupitia sauti yake nzuri. Katika maandiko yaliyo kuja kugunduliwa hapo baadaye yaani maandiko ya Kabbalah k**a vile Zohar, Naamah aligeuzwa kutoka kuwa mwanamke wa kawaida kuja kuwa Roho au pepo wa k**e.

Katika kutafuta muungano ama kuungana na maarifa ya kina ya ndani yaWaluciferi (Gnosis of Luciferians) si jambo rahisi. ...
11/03/2026

Katika kutafuta muungano ama kuungana na maarifa ya kina ya ndani yaWaluciferi (Gnosis of Luciferians) si jambo rahisi. Njia hii ya kiroho ina miiba na maumivu mengi kwa wale watakao potea njia hata kwa muda mfupi. Hivyo basi, baki Imara na uwe Makini.

Shirika la Phosphorus (Order of Phosphorus) la Walusiferi, ni wazo lililo zaliwa kutoka kwa wale waliomo ndani ya familia "coven Nachttotet, tunawakaribisha watu wa njia zote wanao taka kuchunguza na kutafiti kuhusu upande wao wa ndani ulio jificha ama upande wao wa ndani wa Giza wa nafsi zao.

Black Flame yaani Moto Mweusi utaweza kuufikia kwa kugundua chanzo kilicho fichwa ndani yako mwenyewe. Jambo hili linahitaji nguvu, akili na Ustadi, kwani utajaribiwa na kupimwa kwa kila namna.

Huu ni mtazamo chanya wa kile kinacho itwa "Black Magick" yaani Uchawi mweusi...na ndiyo, kuna njia yakutazama hilo kwa mtazamo chanya.

Maadui wetu ni Ubaguzi/ubaguzi wa rangi, ujinga na Udhaifu.

Ni wakati wa kuinuka juu ya maumbo haya ya kimwili matupu yasiyo na kitu yanayo husiana na nafsi ya uongo yaani Ego, na hatimaye kujitokeza k**a Miungu na Miungu wa k**e huru wa Luciferian

Karibu kwenye malango ya Jehanamu..ingia kwa hiari yako, lakini fahamu na kumbuka juu ya onyo hili;-

Hatuto wajibika kwa chochote kutokana na matokeo mabaya utakayo yapata baada ya kukosea kanuni zetu utakazo kwenda kuzijua kupitia page hii.

Naamah au Nahamoth ambapo kutoka katika lugha ya kihebrania ni neno linalo maanisha "kupendeza" au "mwenye kuvutia", ni ...
11/03/2026

Naamah au Nahamoth ambapo kutoka katika lugha ya kihebrania ni neno linalo maanisha "kupendeza" au "mwenye kuvutia", ni kiumbe anayetajwa katika Zohar, ambapo ni mojawapo ya maandiko muhimu ya siri ya kiyahudi (Kabbalah).

Asili yake inaelezwa kuwa inahusiana na Naamah mwingine wa kibinadamu aliyetajwa katika Biblia, ambaye alikuwa dada wa Tubal-Cain.

NAAMAH KATIKA FASIHI ZA KIYAHUDI

Katika maandiko ya kale ya Talmud na Midrashi, Naamah mara nyingi hutazamwa k**a mwanadamu yuleyule anaye julikana katika Biblia. Inaelezwa kwamba alipata jina hilo kwa sababu ya kuwavutia na kuwashawishi wanaume kwa Muziki wa matowazi aliyokuwa akipinga. Katika hadithi hizo inaelezwa kuwa alimshawishi (kingono) Malaika aitwaye Shamdon au Shomron na kuzaa naye mtoto aitwaye Asmedeus (Ashmodai) aliye kuja kuwa Mfalme wa pepo wabaya.

Baadaye, katika maandiko ya siri ya kabbalah yaani Zohar, Taswira yake ilibadilika kutoka kuwa mwanadamu wa kawaida na kuja kuwa Roho ya kipepo / Roho ya kishetani au pepo.

HADITHI YAKE KATIKA ZOHAR

Kwa mujibu wa Zohar, baada ya Cain kumuua Abel, Adam alijitenga na Eve kwa miake 130.

Katika kipindi hicho, Naamah pamoja na Lilith walimshawishi Adam kingono na kuzaa naye watoto wa kipepo /demonic children ama watoto wa kishetani. Watoto hao kwa mujibu wa masimulizi hayo, walikuja kuwa chanzo cha mateso na majanga kwa wanadamu..ama walikuja kuwa mateso au mapigo ya wanadamu duniani. Pia hadithi hizo zinadai kuwa Naamah na Lilith husababisha kifafa kwa watoto.

Katika Hadithi nyingine ya Zohar, inaelezwa kuwa Naamah na Lilith waliwashawishi malaika wawili Az**el na Ouza kingono, Malaika walio kuwa sehemu ya kundi linaloitwa Watchers.
Maandiko hayo yanaeleza kwamba Naamah aliwavutia mapepo wengi. Kila siku usiku hufuatiliwa na Wafalme wa mapepo wanaoitwa Afrira na Qastimon. Lakini yeye hujibadilisha maumbo na kuwatoroka huku akiendelea kuwashawishi wanaume.

TABIA YAKE KATIKA HADITHI ZA KABBALAH

Kwa mujibu wa Zohar pia inaelezwa kuwa:

Naama huwashawishi wanaume (kingono) kupitia ndoto zao.

Naamah huchukua tamaa ya mwanaume, na kisha kutokana na tamaa hiyo huzaa mapepo mbalimbali.

Viumbe hao baadaye huwajia wanawake wa wanadamu na kusababisha kuzaliwa kwa roho au viumbe wa kiroho wengi zaidi.

Na wote hao hurudi kwa Lilith ambaye ndiye huwalea.

Kumbuka kwamba, Hadithi hii imetoka katika fasihi za mafumbo ya kabbalah, na sio simulizi rasmi katika Biblia.

Hadithi hizi zinatumika zaidi kuelezea kwa Lugha ya alama mambo k**a vile; mawazo kuhusu tamaa, ndoto, nguvu za kiroho, na upande wa giza wa nafsi ya mwanadamu.

Uchawi wa Lusifa (Luciferian Witchcraft) ni itikadi inayo husu "njia ya mkono wa kushoto" (The Left Hand Path), mara nyi...
13/02/2026

Uchawi wa Lusifa (Luciferian Witchcraft) ni itikadi inayo husu "njia ya mkono wa kushoto" (The Left Hand Path), mara nyingi inahusishwa na mwandishi "Michael W. Ford.

Itikadi hii ya Uchawi wa Lusifa, inamchukulia Lucifer k**a alama kuwakilisha nuru, mwangaza wa kiroho, uhuru na kujitukuza nafsi badala ya kumwona Lucifer k**a shetani mwovu k**a baadhi ya dini wanavyo amini. Ni itikadi inayo sisitiza waumini wake kujijenga wao binafsi, kufikiri kwa kina, na utafutaji wa maarifa. Wafuasi wake hujikita katika kutafuta mabadiliko ya ndani na utawala wa nafsi kupitia ibada na mazoezi ya kiroho.

MISINGI MIKUU YA UCHAWI WA LUSIFA.

ALAMA YA LUSIFA

Lusifa anaonekana k**a "mleta nuru" , roho au ishara ya uongozi wa ndani, hekima, na pia anawakilisha giza la ndani lenye maarifa, Na sio Mungu wa kuabudiwa kiuhalisia.

UANZISHWAJI KATIKA NJIA YA MKONO WA KUSHOTO (LHP INITIATION)

Njia hii huweka mkazo kwenye uhuru wa kiroho wa mtu binafsi,vkugeuzwa kuwa chanzo cha nguvu (Kufanyika Mungu wa nafsi), na kujiwezesha.

FALSAFA:

Mfumo huu unathamini sana fikra zenye mantiki/zenye mashiko, uwajibikaji wa mtu binafsi, na kuvunja mipaka ya mila au miiko ya kijamii na kidini.

MAZOEZI:

Kitabu cha "Luciferian witchcraft" cha mwaka 2005 chake Michael W. ford, ni maandiko ya msingi kuhusu mazoezi ya vitendo ya uchawi wa Lusifa, kikitoa (Grimoire), mwongozo wa ibada kuelekea njia hii ya kiroho.

UHUSIANO WAKE NA DINI YA SHETANI (SATANISM):

Ingawa baadhi ya wafuasi huyaunganisha mashirika haya mawili k**a kitu kimoja, lakini wengine hutofautisha kwa uwazi kati ya Lusifa anayechukuliwa k**a alama ya maarifa na mwamko wa kiroho, na wakati huo huo Shetani anachukuliwa kwa dhana tofauti kabisa.

Kwa ujumla, falsafa hii inawahimiza wafuasi wake kukumbatia nguvu yao ya ndani, kujijua ama kujitambua, na kutilia shaka imani za jadi tulizo zaliwa nazo ili kufikia Ufahamu wa juu wa nafsi..

JINSI YA KUGUNDUA PEPO WAKO MLEZIKwahiyo utaweza kuona kwamba Roho za juu (Higher spiritis)  zinaendana kitabia na mafun...
22/09/2025

JINSI YA KUGUNDUA PEPO WAKO MLEZI

Kwahiyo utaweza kuona kwamba Roho za juu (Higher spiritis) zinaendana kitabia na mafundisho ya kisasa katika dini kuhusu Malaika. , wakati huohuo pia Demons au mapepo sifa zake zinafanana na Roho au mizimu katika tamaduni zetu ambao ni roho walio karibu na ulimwengu wa kimwili au wanajihusisha na mambo ya mwilini au matter.

Lakini pia linapkuja swala kuhusu uchawi wa aina yetu (luciferians) ambazo ni Grimoires k**a vile Ars Goetia kuna namna fulani ya muhimu inayo lingana katika swala hili. Lakini katika Luciferians inaeleweka kwamba Roho wengi wa Agizo la Juu walibadilishwa kuja kuwa Demons/Mapepo katika ngazi za uongozi wa Roho zilizo kuja kuanzishwa na Dini za Abraham. Mifano ya Roho wa juu walio kuja kubadilishwa kuwa mapepo ni k**a vile Ashtaroth, ambaye ni umbo la kipepo la Mungu mke ISHTAR.

ROHO ZA WALINZI WA ULIMWENGU WA KALE.

Ukweli muhimu wa kihistoria ambao tunaweza kuupata kutoka katika maandiko ya kale ni kwamba jamii za kale zilikuwa na Roho za walinzi. Hizi zilikuwa ni Roho za mababu, Miungu na Mapepo. Wazee wetu walikuwa wakitoa ibada za dhabihu, sala na katika baadhi ya matukio walifanya mila/matambiko na sherehe za kichawi , wakitafuta msaada kutoka kwa Roho zao za Walinzi.

Hii ndiyo aina ya ukiroho ambayo imepotea katika Ulimwengu wa hivi sasa. Kwakusema hivyo sina nia ya kufufua mambo hayo kwa uhusiano mpana zaidi wa kijamii na Ulimwengu wa kiroho, kwasababu jamii yetu kwa sasa imechafuliwa na mambo ya kimila za kidini na yakudhalilisha (ukitoho huo wa kale) ambayo yamechukua fursa ya uhusiano huo. Kwakusema hayo ni jambo lililo wazi kwamba kwasasa tunaishi katika Ulimwengu ambapo Ulimwengu wa kiroho umeachwa kwa watu binafsi kuweza kuuchunguza na kuutumia vyema. Mwanzo mzuri wa kuweza kuchunguza jambo hili ni kumfanya mtu binafsi aweze kutambua na kumgundua Pepo mlinzi wake binafsi k**a vile ilivyo kwa malaika mlinzi pia kuna pepo mlinzi ambapo unapaswa kujenga uhusiano nae. Kwako binafsi.

Kwa upande wangu binafsi, Demon paimon ndiye pepo wangu Mlinzi. Jambo hilo lilitokea k**a bahati mbaya wakati nilipo kuwa nikifanya maombi ya kimila ya Pepo Paimon na kuja kugundua uhusiano huu. Kilicho tokea k**a matokeo ya kile nilicho kigundua kilikua ni jambo la kushangaza. Kilicho tokea k**a matokeo ya kugundua uhusiano wangu na Pepo Paimon kuanzia wakati huo hadi hivi leo, niliweza kuungana na Mapepo wengine kiurahisi na majibu ya shughuli zangu za uchawi yakawa ya kipekee. Kumbuka, kabla ya kukutana huku na demon Paimon nilikuwa tayari nimefikia cheo cha juu katika Agizo la siri ambalo nilianzishwa na tayari nilikuwa mchawi mwenye sifa kubwa. Lakini baada ya kupata bahati hii ya kukutana na Pepo wangu mlezi (guardian demon) iliharakisha maendeleo na mafanikio yangu kwa makumi ya miaka (miongo mingi).

Sasa kwanini jambo hili la kumtafuta Pepo wako mlezi halizungumzwi sana?

K**a ilivyo katika sayansi zote za uchawi, mbinu na mafundisho yenye nguvu sana yamefichwa kwaajili ya wachache walio chaguliwa (wateule) na huku siri ndogo tu hutolewa kwaajili ya watu wengi. Vivyohivyo pia hata sisi ambao tumepanda ngazi na kufikia daraja za juu, bado tunakabiliwa na shimo pana ambalo linatutenganisha na babu zetu wa kipagani.

Mimi binafsi sidai wala sina hati ya uhakika kusema kwamba Mambo ya kale ya kipagani ni bora kuliko haya ya kisasa. Lakini ni ukweli usio pingika kwamba Ulimwengu wa kale kwa ujumla wake ulikuwa umezama ndani zaidi katika mambo ya kichawi na kwa maana hiyo kulikuwa na matokeo makubwa zaidi (watu wa zama hizo za uchawi wa kale waliweza kuita mvua au kusimamisha mvua kupitia Mapepo wa kale au Roho zao za kipepo). Hivi sasa tumerithi sehemu ndogo tu ya maarifa hayo ya kale,na inatubidi tugundue mengine peke yetu ndani ya muda mfupi uliopo. Uwezo wa Pepo mlinzi ni sehemu moja ya maarifa hayo yaliyo sahaulika ambayo mimi binafsi nilijikwaa juu yake. Kisha niliamua kusonga mbele kuendelea kutengeneza mbinu za kuwasaidia wengine kugundua pepo wao wa kuwalinda.

MBINU ZA KUMGUNDUA NA KUMTUMIA PEPO MLINZI AU MLEZI WAKO. ACHANA NA MALAIKA MLINZI NI DHAIFU HAO IKIWA MATAMANIO YAKO NI MATTER K**A VILE UTAJIRI, HESHIMA N.K MGUNDUE PEPO (DAIMON - DEMON)

GUNDUA PEPO WAKO MLEZI.Sote tumekuwa tukisikia na kufundishwa juu ya Malaika walinzi, na tumekuwa tukifundishwa kuwa kil...
21/09/2025

GUNDUA PEPO WAKO MLEZI.

Sote tumekuwa tukisikia na kufundishwa juu ya Malaika walinzi, na tumekuwa tukifundishwa kuwa kila mmoja wetu ana malaika wake wa Ulinzi (guardian angel) tangu kuzaliwa kwake . Lakini yakupasa kujua kwamba kuna Pepo Mlezi au Pepo mlinzi yaani Guardian Demon. Ingawa jambo hili kuhusu Mapepo walinzi linaweza kuwa ni geni kwa walio wengi hilo ni kwasababu ya mafundisho ya kidini na kiutamaduni.

Katika mafundisho ya kiroho na uchawi, inaelezwa kuwa Ulimwengu wa kiroho una kambi mbili , kambi ya kwanza ni kambi ya Roho waovu (evil spirit) yaani demons na Kambi ya pili ni Roho wema ambao ni malaika (angels) ambapo ni Roho zinazopigana na kupigania dhidi ya nafsi zetu zisizo weza kufa.. Hii ndiyo sababu ya kwamba wazo juu ya Pepo walinzi ni gumu kueleweka kwa baadhi ya watu.

Watu wengi wanajiuliza Hivi pepo mchafu (evil spirit) anaweza kuwa mlinzi wa wanadamu?

Ulimwengu wa Upagani unaelewa ya kwamba kuna mgawanyiko wa uongozi wa Roho (na wanadamu). Mgawanyiko huo haukuwa ukihusisha duality au asili ya uwili uwili au maadili yake, bali ni aina ya maslahi yaliyowashughulisha na ukaribu wao zaidi ulio tokana na mambo safi au roho safi.

Kwamfano, mtu anayependezwa na mambo ya kiroho alizingatiwa kuwa mtu wa juu zaidi katika uongozi wa kiroho na kwahivyo hivyo katika uongozi wa kijamii, kwa kuwa jamii za kitamaduni zilijaribu kuiga ulimwengu wa kiroho. Kwahiyo maalahi ya mtu k**a huyo yangemleta katika ushirika na Roho za mbinguni na zenye mwanga zaidi. Mtu k**a huyo angeweza kuchukua nafasi za ukuhani, au kujitolea k**a shujaa.

Mtu mwenye kupendezwa au anayependelea mafanikio ya kimwili aliwekwa katika daraja la chini la uongozi, inawezekana labda ni mfanyabiashara au fundi, akiwasiliana na Roho wa mali au zile roho ambazao zinaweza kumsaidia kukidhi maslahi yake duni. Lakini hapakua na maadili yoyote baina ya pande mbili

Kwa maana kwamba Roho za Juu zinachukuliwa k**a Roho nzuri na Roho za chini zinachukuliwa k**a roho mbaya (Roho waovu au demon). Kwa maelezo mazuri na rahisi tunaweza sema Nuru na giza. Ngono ni ni giza kwasababu huvuta na kumtega Roho kwenye ulimwengu wa mada au kwenye matter. Utajiri ni giza kwasababu huishughulisha Roho na mambo ya mwilini au matter na hatimaye humfanya Roho aendelee kuwepo kwenye ulimwengu duni wa matter

Useja (kutokufanya ngono kwa kujizuia) ni Nuru pamoja na kutokuwa na Ubinafsi ni nuru pia kwasababu humweka huru Roho / huiweka huru Roho kutoka kwenye mitego ya kimwili.

Kwahiyo kuna Roho wa nuru na Roho wa giza, kulingana na namna zinavyo fanya kazi kwa kupendelea na kufuata maslahi ya Roho au maslahi ya mwilini.

Lakini naomba nirudie tena kwamba hakuna suala la maadili katika njia yoyote, kwamba labda kukaa kwemye upande wa Roho za giza ni kosa na kwamba wote lazima wakae upande wa nuru hapana hakuna maadili yoyote. Roho waovu na Roho wema hugawanywa kutegemeana na mambo wanayo yapendelea (maslahi yao) k**a Roho anapendelea maslahi ya mwilini mfano Utajiti huchukuliwa kuwa Roho wa chini au giza kwakua anapendelea ya mwilini au anapendelea mitego ya mwilini. Na roho wema ni Roho wanao pendelea kujishughulisha na mambo ya rohoni ili kuiweka huru roho na mitego ya mwilini. Kwahiyo hakuna maadili yoyote kwa tamaa yoyote ya mwanga au giza.

Matamanio yetu yanatofautiana, kuna mtu anaweza kuona njia ya kiroho sio bora kuliko njia ya mali, jambo hili ni swala la upendeleo wa mtu binafsi anacho kipenda. Kwahiyo basi Njia ya kiroho ya Mali na utajiri inaweza kuimarishwa ikiwa mtu atajiunga na Tawi lolote la njia ya mkono wa kushoto LHP yaani The Left hand Path Occultism

THE SIGIL OF LUCIFERSIGIL YA LUSIFA | MUHURI WA LUSIFANi alama isiyo julikana sana lakini kihistoria ni Sigil ambayo hut...
21/09/2025

THE SIGIL OF LUCIFER

SIGIL YA LUSIFA | MUHURI WA LUSIFA

Ni alama isiyo julikana sana lakini kihistoria ni Sigil ambayo hutumika k**a nembo kuwakilisha maarifa ya kiroho na mwangaza.

Picha hiyo ilitokea na kuanzia katika karne ya kumi na sita katika kitabu cha uchawi huko Italia kiitwacho "Grimoirium Verum, "Grimoire of Truth" kumaanisha "Grimoire ya Ukweli" ni alama inayotumika kwa kushirikiana naalama zingine,

Kusudi kuu la Sigil hii ya Lusifa lilikuwa ni kuweza kusaidia katika maombezi ya kumuona au kumuita Malaika Lusifa.

Takwimu na tafiti zinaonyesha kwamba Sigil hii ya Lusifa imetolewa kutoka katikakazi za hivi karibuni, wengine wanaeleza ya kwamba alama hiyo ilibuniwa na kuchorwa kutoka katika Mraba wa kichawi ambao asili yake kwa sasa imepotea.

Muundo wa pembetatu katika alama hiyo unao onyeshwa ukielekea juu unawakilisha kupaa kiroho/kukua kiroho na jitihada ya Roho katika kupambana kuelekea Ulimwengu wa juu, wakati huohuo alama iliyopo ndani yake, inawakilisha maelewano baina ya maono ya ndani na udhihirisho wa nje. Kwahiyo ni nembo inayo wakilisha umoja, Safari ya roho kufika ulimwengu wa juu huku ikiakisi ulimwengu wa ndani kupitia jicho linalo ona yote.

Baadhi ya watu wengine wanaamini kwamba, Sigil ya Lusufa ni alama ya kale kumuwakilisha Enki, ambaye ni miongoni mwa Miungu wakongwe wa kale anaye julikana sana kwa wanadamu, takriban miaka 12,000 ilitopita wakati wa ustaarabu wa kwanza wa wanadamu.

Enki anajulikana kwamba ndiye aliyekuwa kiongozi wa Miungu ambao walikuja kusaidia kujenga ustaarabu wa wanadamu, kisha kuwapa maarifa na muongozo.

Katika mila za kale za Sumeria, Enki alikua Mungu wa maji, Hekima, na Uumbaji na pia alikuwa mleta nuru ya kujitambua na ndiye aliye leta Sheria za Ustaarabu na maendeleo ya wanadamu. Muunganiko huo unalenga kuonyesha maana ya kina ya Sigil ya lusifa kwamba ni sigil inayo husishwa na Mwangaza wa kiroho sambamba na maarifa ya siri yaliyo fichwa.

Muhuri ni wa uganga na maombi ya uchawi wa Lusifa, yeye ni malaika lakini anajulikana kwa njia mbadala kwa muda mrefu katika historia kuhusiana na uwanja huu wa kiroho

Macho ya vipofu wanacho weza kuona ni namna zenye kufanana katika habari hii lakini hawawezi kuona kina chake cha ndani. Lakini kwa kutazama kupitia Jicho la tatu unaweza kuona kina cha maana juu ya sigil hii ya lusifa.

Hapa neno "Lusifa" halikuwa na lengo kumaanisha uovu au muovu lakini neno hilo lilikusudiwa k**a ilivyo katika lugha ya kilatini kumaanishs "Light bringer" yaani mleta nuru ambapo ni uwakilishi wa Mwangaza, ni mwali wa moto wa ndani ambao hufunua Kweli (ndani yetu) ma kuwaongoza watafutaji wa nuru.

Kwahiyo Jicho linaloona yote na nyoka aliye jifunga katika eneo lililo baki kwenye alama yetu pichani kwa pamoja ni alama ya umilele, kuzaliwa upya na maarifa. Kwa pamoja ukiunganisha na Sigil ya Lusifa alama hizo zinatengeneza hirizi ya mabadiliko, ikitukumbusha kwamba hekima kamwe haipatikani kwenye imani za utii za upofu lakini katika umoja wa maono ya ndani na kufanyika upya milele...

By Ruina, Surgit Lux

"Luciferian (Muumini wa Dini ya Lusifa) ni mtu bora mwenye nguvu, aliyeangaziwa , tofauti na wale ambao huabudu sanamu k...
20/09/2025

"Luciferian (Muumini wa Dini ya Lusifa) ni mtu bora mwenye nguvu, aliyeangaziwa , tofauti na wale ambao huabudu sanamu kutokana na imani za upofu. Yeye ni msafiri mpweke kwenye njia nyeusi zaidi kuliko wote, ni njia ambayo inaelekea kwake yeye mwenyewe, ili kutembea katika ulimwengu wa maadui zake wakubwa, na pepo wake yeye mwenyewe.

Dini ya Lusifa haiwezekani kufundishwa (kwa mafundisho tu). Watu ambao ni waumini wa Lusifa hawakufundishwa kuwa waumini wa Lusifa au kujifunza kuwa hivyo, huwa wanahamasishwa tu kuamsha uwezo ambao tayari umezikwa ndani yao"

༒︎By Patrick Gaffier. (Kwenye njia ya ndani ya Luciferians)

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255757567678

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Lusifa_Kuzimu_Tz_Waabudu Shetani posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share