11/05/2026
NAMNA YAKUPATA POINTS ZA UBORA WA KLABU BARANI AFRIKA(CAF CLUB RANKING)
* CAF clab ranking ndiyo hutoa orodha ya ubora wa KLABU ulioonyeshwa ndani ya miaka MITANO mfululizo Kwa kujumuisha points za KLABU ktk mashindano ya CAF klabu BINGWA na shirikisho Kuanzia msimu uliopo na nyingne NNE za nyuma mfululizo.
✓ mfano; msimu huu 2025/26 x Unit 5, 2024/25 x unit 4, 2023/24 x unit 3, 2022/23 x unit 2 na msimu 2021/22 x unit 1. Misimu nyingne inaondolewa (Nulfied) maana inazidishwa na sifuri.
A. POINTS ZA KOMBE LA SHIRIKISHO
1. Mshindi wa mwisho ktk Kundi hupata points 0.5 na mshindi wa tatu hupata points 1
2. Robo Fainali hupata points 2
3. Nusu hupata points 3
4. Mshindi wa pili hupata points 4 na BINGWA hupata points 5
B. POINTS ZA KOMBE LA KLABU BINGWA
1. Mshindi wa mwisho ktk Kundi hupata points 1 na mshindi wa tatu hupata points 2
2. Robo Fainali hupata points 3
3. Nusu Fainali hupata points 4
4. Mshindi wa pili hupata points 5 na BINGWA hupata points 6
Mfano Points alizonazo Simba SC Tanzania
Msimu 2021/22 alipata ponts 2 toka robo ya CAF shirikisho zidisha Kwa 1, msimu 2022/23 alipata points 3 toka robo CAF klabu BINGWA zidisha Kwa 2, msimu 2023/24 alipata ponts 3 toka KLABU BINGWA zidisha Kwa 3, msimu 2024/25 alipata ponts 4 toka kuwa mshindi wa pili CAF shirikisho zidisha Kwa 4 na msimu huu 2025/26 alipata point 1 baada ya kuwa mshindi wa mwisho ktk Kundi la KLABU BINGWA zidisha Kwa 5.
Hapo utapata==2 x 1 + 3 x 2 + 3 x 3 + 4 x 4 + 1 x 5 Jumla inakuja POINTS 38:
Mfano wa pili Points za Al Ahly SC
✓Msimu 2021/22 alipata points 5 baada ya kuwa mshindi wa pili klabu BINGWA zidisha Kwa 1, 2022/23 Points 6 baada ya kuwa BINGWA CAFCL zidisha Kwa 2 , 2023/24 Points 6 baada ya kuwa BINGWA CAFCL zidisha Kwa 3, 2024/25 Points 4 baada ya kuishia Nusu klabu BINGWA zidisha Kwa 4 na msimu huu 2025/26 Alipata points 3 zidisha Kwa 5
Jumla POINTS ni 66
∆ ndizo alizonazo mpaka sasa, tusubirie Fainali za mashindano (CAFCL na CAFCC ) msimu huu tuone atakuwa nafasi ya ngapi?!