07/06/2026
ENDELEA KUSIMAMA
Wakati mwingine maisha hayana adabu kabisa.
Unaweza kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii sana lakini wapi mambo hayaendi.
Mshahara wako ni hautoshi,si boss wala ofisi yako wanatambua jitihada zako.
Hakuna marupurupu wala nyongeza ya mshahara yaani ni hivi vyuma vimekaza blaza.
ENDELEA KUSIMAMA
Haya mjomba unaamua kujichanganya unafungua kibiashara chako angalau ujikomboe kimaisha.
Hapo ndo kwanza mambo hayaendi mbaya zaidi unaongeza madeni juu biashara inakufa.
ENDELEA KUSIMAMA
Unakuwa mwaminifu kwa Mungu na wanadamu.
Haujawahi kuiba ,kutukana wala kumfanyia mtu ubaya wowote lakini bado maisha yanakupiga ngumi tena za uso.
ENDELEA KUSIMAMA
Pengine familia yako ndo imekuwa faraja kwako.
Ndo kwanza unamiaka mitatu kwenye ndoa na Mungu amewabariki kachalii kamoja unaitwa baba Ima.
Wife kuona life limechanganya anakwambia;
Hukunioa ili nipate shida hapa mjini anaondoka na mwanae na kurudi kwao.
ENDELEA KUSIMAMA
Kwanza pole kwa yote blaza ,na ushauri wangu kwako ni kwamba;
ENDELEA KUSIMAMA
~Mwl Deo Kabuje
+255767451108