Sickle Cell Disease Patients Community of Tanzania

Sickle Cell Disease Patients Community of Tanzania Sickle Cell Disease: Is a hereditary problem (which mean it runs in families). It causes a type of faulty hemoglobin in red blood cells.

Read more.http://www.ornl.gov/sci/techresources/Human_Genome/posters/chromosome/sca.shtml The registered office of the Company located in Tanzania. Its main objective is to infiltrate the knowledge and raise awareness of sickle cell disease to the society and create a forum to air problems of SCD and share knowledge, skills, solutions and experiences among people living with SCD. This is done by p

roviding counseling, support and education to patients suffering from complication associated with sickle cell disease and the society, assisting patient with psychosocial complication, ensuring drug availability and accessibility for management of sickle cell patients, establishing an official sickle cell treatment centre in Tanzania, decreasing stigmatization and other problems of such kind surrounding sickle cell disease, helping other organizations/institutions working or intended to work in this field, documenting, publishing articles, newsletters, books and other materials and disseminate findings of the scientific researches carried out for the purposes of enhancing awareness and promote education in the areas of its operation.

10/05/2026

πŸ‘©β€πŸΌβœ¨Kwa kila shujaa ambaye pia ni mama tambua kuwa wewe ni wa thamani sana 🀍

Wewe ni baraka kubwa. Safari yako imejaa changamoto nyingi, lakini bado unaendelea kusimama imara kila siku.

Unaendelea kupambana, kujitunza mwenyewe na kuitunza familia yako kwa upendo na nguvu ya kipekee.

Hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kila siku.

Ujasiri wako unaangaza na kugusa maisha ya wengi πŸ’ž

🀰🌸 Kheri ya Siku ya Mama Duniani 🌸



β€”β€”β€”β€”β€”β€”β€”β€”β€”β€”β€”β€”

πŸ‘©β€πŸΌβœ¨To every sickle cell warrior who is also a mother know that you are truly valuable 🀍

You are a blessing. Your journey may carry many challenges, yet you continue to stand strong every single day.

You keep fighting, caring for yourself, and nurturing your family with love and strength.

Thank you for the incredible work you do. Your courage shines brightly and inspires so many πŸ’ž

🀰🌸 Happy Mother’s Day 🌸

10/05/2026

πŸ’“ Ni Nguzo Yangu

Amenilea kwa upendo mkubwa na wa dhati 🀍

Naamni hakuna mtu anayeweza kusimama na mimi kwa nguvu na moyo k**a yeye anavyofanya.

Katika nyakati za maumivu yangu, hukosa usingizi akikesha pembeni yangu na kuniombea kwa upendo wa mama usio na mfano.

Kwangu, wewe ni kila kitu. Nashukuru kuwa na mama wa namna hii, na nakupenda kwa moyo wangu wote πŸ’ž

🌸 Kheri ya Siku ya Mama Duniani 🌸



β€”β€”β€”β€”β€”β€”β€”β€”β€”

πŸ’“ My Pillar

She raised me with so much love and care 🀍

I truly believe no one stands by me as strongly as she does.

During my painful nights, she stays awake beside me, praying for me and comforting me with a mother’s endless love.

To me, mom you are my everything. I am deeply grateful for your love, and I love you with all my heart πŸ’ž

🌸 Happy Mother’s Day 🌸

10/05/2026

πŸ’ͺ Mama Shujaa Wangu

Upendo wako hauna masharti 🀍

Mama yangu ni shujaa wangu wa kweli mwenye uvumilivu, nguvu na moyo wa kipekee usiochoka kunisitiri na kunipa matumaini kila siku.

Ninatambua na kuthamini mchango wako mkubwa katika maisha yangu.

Asante kwa kuwa nguzo yangu katika kila hatua ya safari yangu πŸ’ž

🌸 Kheri ya Siku ya Mama Duniani 🌸



β€”β€”β€”β€”β€”β€”β€”β€”β€”

πŸ’ͺ My Hero Mother

Her love is unconditional 🀍

My mother is my true hero patient, strong, and endlessly supportive.

She continues to stand by me with love, courage, and hope every single day.

I deeply appreciate her presence in my life and the incredible impact she has made on my journey πŸ’ž

🌸 Happy Mother’s Day 🌸

10/05/2026

Upendo wa mama ni tiba ya moyo 🀍

Katika safari ya Siko Seli, mama wamekuwa nguzo ya nguvu, faraja na matumaini kwa mashujaa wengi kila siku.

Tunawashukuru kwa upendo wao usiochoka, dua zao na kujitoa kwao bila masharti.

Leo tunawaenzi mama wote wanaopambana, kulea na kusimama imara pamoja na watoto wao πŸ’



β€”β€”β€”β€”β€”β€”

A mother’s love heals beyond words 🀍

In the sickle cell journey, mothers continue to be pillars of strength, comfort, and hope for so many warriors every single day. We celebrate their endless love, sacrifices, prayers, and unwavering support.

Today, we honor every mother who stands strong, nurtures, and fights alongside their children πŸ’

πŸ’―% Kila tone la upendo wako ni nguvu kwetu. ❀️Leo tunawaadhimisha akina mama wote wanaokesha hospitalini, wanaofuta mach...
10/05/2026

πŸ’―% Kila tone la upendo wako ni nguvu kwetu. ❀️

Leo tunawaadhimisha akina mama wote wanaokesha hospitalini, wanaofuta machozi ya watoto wao kwa matumaini na wanaotoa tabasamu pana hata kati-kati ya mapambano mazito. 🌹

Wewe ni zaidi ya mama; wewe ni nguzo ya kwanza, tabibu wa kwanza na shujaa wa kweli asiyekata tamaa. Katika safari hii ya Siko Seli, upendo wako usio na kikomo ndio unaoandika hadithi za ushindi kila siku. πŸ’ͺ

Heri ya Siku ya Mama Duniani kwa mama wote wa Mashujaa wa Siko Seli. Upendo wako ni dawa ya moyo.

Unaijua nguvu ya sauti yako, ndani mwako inaweza kukufanya mshindi katika mengi ambayo unakutana nayo karibu kila siku k...
04/05/2026

Unaijua nguvu ya sauti yako, ndani mwako inaweza kukufanya mshindi katika mengi ambayo unakutana nayo karibu kila siku kwenye maisha yako? Ukweli halisi wa mambo ulivyo, sauti yako ina nguvu kubwa dhidi ya sauti za nje. Unawaza nini, unaona wewe ni nani?

Mashujaa wetu 14 tumewaleta pamoja na kupeana maarifa namna bora ya kusikiliza sauti zao za ndani, kutambua nguvu iliyobebwa na sauti hiyo, kwanini hawapaswi kukata tamaa hata k**a jamii inayowazunguka haielewi kile wanachokipitia, maumivu yao na ndoto walizo nazo kwamba zinaweza siku moja kutimia na wakafanya makubwa duniani k**a ambavyo wale wasio na ugonjwa wa Siko Seli hufanya.

Umekuwa wakati mzuri kwetu, kushirikisha hadithi za maisha yetu, baina yetu. Tumejaa ujasiri mpya na mkuu zaidi wa kupambania ndoto zetu, licha ya maumivu makali tunayopitia, unyanyapaa na kukatishwa tamaa kwingi, kikao hiki kimejumuisha pia wanajamii wengine na imani yetu ujumbe sahihi kuhusu Siko Seli utaendelea kuifikia jamii kwa ukubwa. Sisi ni mashujaa na sauti yetu ina nguvu. Asante Power of Sentence kwa kutuleta pamoja.

Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Siko Seli Tanzania (SCDPCT), k**a taasisi inayofanya kazi moja kwa moja na jamii, imeshirik...
17/04/2026

Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Siko Seli Tanzania (SCDPCT), k**a taasisi inayofanya kazi moja kwa moja na jamii, imeshiriki semina ya kimataifa iliyoandaliwa na St. Jude Children’s Research Hospital (ALSAC) tarehe 12–13 Aprili 2026, Lagos, Nigeria, pamoja na wadau kutoka nchi zaidi ya 10 barani Afrika. Semina hii imewakutanisha wadau wa uchechemuzi, uelimishaji na tafiti kuhusu Siko Seli na saratani za watoto, kujadili mustakabali wa afya ya mtoto katika Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mada zimejikita katika uongozi wa taasisi, usimamizi wa miradi, mifumo ya kifedha, uwazi na uwajibikaji, huku tukibadilishana uzoefu kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, uelewa wa jamii na mifumo ya afya tukitambua kuwa changamoto nyingi huanza ngazi ya jamii kabla ya takwimu rasmi. Ushiriki wetu ni uthibitisho kuwa sauti za jamii zina nguvu ya kuleta mabadiliko ya kweli. Jumuiya imewakilishwa na Afisa Habari na Mawasiliano kwa Umma, Veronica Mrema.

**********

The Sickle Cell Disease Patients Community of Tanzania (SCDPCT), as a grassroots organization, participated in an international seminar organized by St. Jude Children’s Research Hospital (ALSAC) on April 12–13, 2026, in Lagos, Nigeria, alongside stakeholders from over 10 African countries. The seminar brought together advocates, educators, and researchers working on sickle cell disease and childhood cancers to discuss the future of child health in Sub-Saharan Africa.

Key discussions focused on institutional leadership, project management, financial systems, transparency, and accountability, while emphasizing experience-sharing to strengthen partnerships, community awareness, and health systems recognizing that many challenges emerge at the grassroots level before official data. Our participation affirms that grassroots voices have the power to drive real change. The organization was represented by Public Relations and Communications Officer, Veronica Mrema.

Mwezi huu wa Aprili, tunakukaribisha katika safari ya kujitambua, kujikubali, na kujithamini.Kupitia Power of Sentence P...
01/04/2026

Mwezi huu wa Aprili, tunakukaribisha katika safari ya kujitambua, kujikubali, na kujithamini.

Kupitia Power of Sentence Programme, tunalenga kukuinua kiakili na kihisia kwa kukusaidia kuona picha halisi ya wewe ni nani ndani yako na katika jamii inayokuzunguka. Kwa wale wanaoishi na Siko Seli, kumbuka: Wewe si ugonjwa wako. Wewe ni nguvu, matumaini na ndoto zilizo hai.

Aprili hii, chukua muda:
✨ Kujitazama kwa jicho la huruma
✨ Kutambua thamani yako
✨ Kujenga fikra chanya zinazoleta mabadiliko. Pamoja, tutajenga jamii yenye uelewa, upendo, na uthubutu ambapo kila mmoja anajiona kuwa na nafasi na thamani.

🌟 Kauli mbiu ya mwezi: β€œNajitambua, Najikubali, Nanguvu.”

Karibu tushirikiane, tukue pamoja na tuandike upya simulizi la maisha yetu. πŸ’›

🩸 USIRUHUSU SIKO SELI IKUZUIE NDOTO ZAKO! πŸ’ͺ✨Wapo watu wengi wanaoishi na Siko Seli na bado wanasoma, wanafanya kazi, wan...
31/03/2026

🩸 USIRUHUSU SIKO SELI IKUZUIE NDOTO ZAKO! πŸ’ͺ✨

Wapo watu wengi wanaoishi na Siko Seli na bado wanasoma, wanafanya kazi, wanaoa/kuolewa, na kutimiza malengo yao kila siku πŸ™Œβ€οΈ

πŸ“˜ Jarida la Shujaa linakuletea:β€¨βœ… Elimu sahihi kuhusu Siko Seliβ€¨βœ… Shuhuda za watu halisi wenye mafanikioβ€¨βœ… Siri za afya bora na mtindo wa maishaβ€¨βœ… Habari mpya za tiba na juhudi za serikali

πŸ’‘ Maarifa haya yanaweza kubadilisha maisha yako au ya mtu unayemjua.

πŸ“² Jiunge sasa na channel yetu ya WhatsApp:

https://whatsapp.com/channel/0029Vb7PzlQGehEFDKmJKh3x

πŸš€ Kuwa sehemu ya jamii ya mashujaa wanaoelimika na kuhamasika!



Siko Seli haiathiri damu pekee.Kadiri muda unavyopita, inaweza pia kuathiri viungo muhimu vya mwili ikiwemo figo.Kupungu...
14/03/2026

Siko Seli haiathiri damu pekee.

Kadiri muda unavyopita, inaweza pia kuathiri viungo muhimu vya mwili ikiwemo figo.

Kupungua kwa mtiririko wa oksijeni na matatizo yanayojirudia mara kwa mara vinaweza kusababisha uharibifu wa muda mrefu k**a hali hii haitafuatiliwa vizuri.

Ndiyo maana uchunguzi wa mara kwa mara, kunywa maji ya kutosha, na kupata huduma ya afya kwa kuendelea ni muhimu.

Uelewa hulinda afya, na elimu huwezesha familia shiriki ujumbe huu ili kumsaidia mtu kuelewa kuhusu Siko Seli.

Mama shujaa Ester Mwangili kutoka Iringa ametufundisha maana halisi ya upendo na uvumilivu. Kwa zaidi ya miaka 10 amekuw...
14/03/2026

Mama shujaa Ester Mwangili kutoka Iringa ametufundisha maana halisi ya upendo na uvumilivu.

Kwa zaidi ya miaka 10 amekuwa akimlea binti yake anayeishi na Siko Seli kwa nguvu, matumaini na moyo wa kupambana.

Licha ya maumivu, changamoto za shule na gharama za matibabu, bado anaendelea kusimama imara kuhakikisha mtoto wake anaishi ndoto zake k**a watoto wengine.

Leo tunamsheherekea mwanamke huyu jasiri na kuwakumbusha wazazi na jamii: watoto wanaoishi na Siko Seli wanahitaji upendo, uelewa na ulinzi wetu ili waweze kufikia malengo yao makubwa ya maisha.πŸ’œ

Graphic by

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255786707050

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sickle Cell Disease Patients Community of Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share