11/05/2026
Tawi la Mkoa wa Pwani limeungana na wanachama pamoja na volunteers kuadhimisha Siku ya Red Cross Duniani kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo upandaji wa miti, usafi wa mazingira na uchangiaji wa damu.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Wilaya ya Rufiji ndani ya Ukumbi wa FDC-Ikwiriri, yakihusisha wanachama na wadau mbalimbali wa Tanzania Red Cross Society.