15/05/2026
Mwanamke na Uongozi kwa kushirikiana na Afya Yangu Foundation tunakualika kwenye tukio maalum la “Her Flow Gathering” Jukwaa hili litakuwa la kipekee sana kuwakutanisha mabinti na wanawake kwa mazungumzo ya wazi, ya karibu na yenye kujenga.
🎯 Lengo letu ni:
Kujadili kwa kina masuala ya Hedhi Salama, Uongozi, Sisterhood, pamoja na Afya ya Uzazi kwa ujumla, ili kujenga uelewa sahihi na kuimarisha nafasi ya mwanamke katika jamii ya leo.
💬 Katika siku hii utapata fursa ya:
* Kujifunza na kupata maarifa sahihi
* Kushirikiana uzoefu na wanawake wengine
* Kujenga kujiamini na kujitambua k**a mwanamke
* Kujadili changamoto za hedhi na namna ya kuzitatua kwa pamoja
* Kujifunza kwa uwazi kuhusu afya ya uzazi
🎲 Zaidi ya yote:
Tutashiriki michezo mbalimbali (games) itakayochochea kujifunza kwa njia ya kufurahia na kuongeza uzoefu.
🍽️ Na siku hiyo;
Tutakula, tutakunywa, na kusherehekea pamoja Mwezi wa Wanawake Duniani, tukihamasisha umuhimu wa Hedhi Salama.
⚠️ Kumbuka: Nafasi ni chache sana
Wahi kujisajili kwa kulipia kupitia nambari: 0752820316
(Jina litaonekana: Mwanamke na Uongozi)
🤝 Karibu tusherekee pamoja, huku tukijenga mshik**ano na kuendeleza mazungumzo muhimu ya kijamii yanayomhusu mwanamke wa leo.