Uwaridi Official

Uwaridi Official Ukurasa maalumu wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira (UWARIDI)

11/05/2026

FASIHI IMEFIKA UWANJANI

UWARIDI tunatoa pongezi za dhati kwa mtangazaji wa Azam TV, Bwana Ramadhan Ngoda, kwa namna alivyoiinua na kuiweka fasihi andishi ya Kiswahili katika jukwaa kubwa la michezo kupitia matangazo ya Kariakoo Derby, tarehe 3 Mei, 2026.

Katika zama ambazo vijana wengi hukutana zaidi na simulizi kupitia burudani nyinginezo, hatua yake ya kuitaja na kuhusisha fasihi andishi kwenye matangazo ya soka si jambo dogo.

Ni kitendo cha kuifanya fasihi kuwa sehemu ya mazungumzo ya kawaida ya jamii kwa kuionesha (jamii) kuwa riwaya, hadithi waandishi wetu na maandishi yetu vinaweza kuishi sambamba na michezo, muziki na maisha ya kila siku.

Kwa kufanya hivyo, amechangia kile tunachokiita:
“Kuipa Fasihi ya Kiswahili Sauti.”

UWARIDI tunaamini kuwa taifa linalosoma ni taifa linalofikiri. Na kila sauti inayobeba vitabu, waandishi na simulizi za Kiswahili kwenda kwa umma, ni “sauti ya fasihi," na mshirika wa mapinduzi ya kifikra na kimaarifa nchini.

Asante Ramadhan Ngoda kwa kuitambua fasihi.
Asante kwa kuipa fasihi jukwaa.
Asante kwa kuifanya fasihi isik**e katikati ya shangwe za kabumbu.

Wewe ni Sauti ya Fasihi.





KITABU KIPYA.Baada ya ukimya wa muda mrefu, mwandishi Hassan Mboneche anayo furaha kukutangazia ujio wa kitabu chake kip...
25/04/2026

KITABU KIPYA.

Baada ya ukimya wa muda mrefu, mwandishi Hassan Mboneche anayo furaha kukutangazia ujio wa kitabu chake kipya cha MSAMAHA WA RAIS.

Kitabu hiki kitakuwa madukani kuanzia tarehe 26/04/2026. Bei ni Tshs. 7,000/=

Kitapatikana katika maeneo yafuatayo;

DAR ES SALAAM

Kona ya riwaya, Kinondoni—0655428085

Kwa George, Posta—0755454152

MAKAMBAKO

APM Bookshop—0762282599

ARUSHA

Kwa Ally Said—0757690302

MOSHI—0673056571

Nje ya maeneo hayo unaweza kutumiwa popote ulipo.

23/04/2026

APRILI 23 NI SIKU YA VITABU DUNIANI.
"Asomaye, hatoki mtupu."

MSHINDI WA KWANZA wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu katika tamthilia, kwa mwaka 2026, ni mwanachama...
14/04/2026

MSHINDI WA KWANZA wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu katika tamthilia, kwa mwaka 2026, ni mwanachama wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira (Uwaridi), Bw. Hamisi Kibari

Hii ni mara ya pili kwa Bw. Kibari kushinda tuzo hii. Mara ya kwanza (2023) alishinda nafasi ya kwanza katika riwaya. Hii inafanya jumla ya TUZO nne ( Laura Pettie 2024; Maundu Mwingizi 2025) kukusanywa na waandishi kutoka UWARIDI.

Hongera sana Hamis Kibari. Hongera Uwaridi.

UWARIDI tunawatakia wanawake wote nchini na duniani, heri ya kila mnalolisimamia, kwenye siku hii ya kimataifa ya wanawa...
08/03/2026

UWARIDI tunawatakia wanawake wote nchini na duniani, heri ya kila mnalolisimamia, kwenye siku hii ya kimataifa ya wanawake Duniani. UWARIDI tunahitaji tupate waandishi wengi zaidi wa k**e zaidi nchini.

NJOONI TUNUKIE!!

Na ukawe ni Mwaka wenye faraja, amani na utulivu... utakaosheheni uandishi bora na usomaji wenye kuridhika na kitakachos...
01/01/2026

Na ukawe ni Mwaka wenye faraja, amani na utulivu... utakaosheheni uandishi bora na usomaji wenye kuridhika na kitakachosomwa.

Address

Ilala
Dar Es Salaam

Telephone

+255746039697

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Uwaridi Official posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Uwaridi Official:

Share