Sadaka Yetu Group

Sadaka Yetu Group Huu ukurasa ni kwa ajili ya kuwasaidia wenzetu ambao hawana uwezo kifedha kuwawezesha kupata mitaji ya kuanzisha biashara ama kutatua changamoto wanazopitia.

Walengwa wakuu ni yatima, wajane, walemavu na wenye uhitaji maalum

TAARIFA YA SADAKA  – KANDA YA DAR ES SALAAM NA PWANIJumapili, tarehe 06/09/2026, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani ya Sada...
07/09/2026

TAARIFA YA SADAKA – KANDA YA DAR ES SALAAM NA PWANI
Jumapili, tarehe 06/09/2026, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani ya Sadaka Yetu ilifanya tukio la kwenda kumtembelea na kumpa pole Mama Naomi, anayesihi Tabata Senene, Dar es Salaam.

Mama Naomi anakabiliwa na changamoto ya saratani ya kizazi, ambayo imefikia hatua ya mwisho. Kutokana na hali hiyo, kwa sasa hawezi kufanyiwa upasuaji, na anaendelea kupata matibabu maalum katika Taasisi ya Ocean Road kwa ajili ya kupunguza makali ya ugonjwa.

Mama Naomi anaendelea kuhudumiwa na binti yake wa pekee, Naomi, ambaye pia ni mwanasadaka mwenzetu kutoka Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

Baada ya kanda kupata taarifa kuhusu changamoto anayopitia mwanasadaka mwenzao katika kumhudumia mama yake, waliamua kumtembelea nyumbani kwao Tabata Senene kwa lengo la kumpa pole, kumfariji na kumtia moyo katika kipindi hiki kigumu.

Katika ziara hiyo, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani ilifika ikiwa na mahitaji mbalimbali yenye thamani ya TZS 208,000/= (Laki Mbili na Elfu Nane) pamoja na mchango wa fedha taslimu wa TZS 150,000/= (Laki Moja na Elfu Hamsini).

Kwa pamoja, msaada huo ulikuwa na thamani ya jumla ya:

TZS 358,000/= (Laki Tatu na Elfu Hamsini na Nane).

Tunawapongeza na kuwashukuru wanasadaka wote walioshiriki katika jambo hili la upendo, faraja na utu. Mchango huu, pamoja na thamani yake, ni ishara ya kuwa hakuna mwanasadaka anayepaswa kupitia changamoto peke yake.

Tunaendelea kuamini katika nguvu ya upendo, mshikamano na kusaidiana katika nyakati za furaha na changamoto.

Mungu awabariki sana wote mliohusika na kuwaimarisha Mama Naomi na binti yake Naomi katika kipindi hiki.

!

Tunashiriki baadhi ya picha za wana Sadaka Yetu waliohudhuria kwenda kumfariji mwenzetu Erick, ambaye amefiwa na baba ya...
03/09/2026

Tunashiriki baadhi ya picha za wana Sadaka Yetu waliohudhuria kwenda kumfariji mwenzetu Erick, ambaye amefiwa na baba yake. Mazishi yamefanyika leo.

Tunamwomba Mungu awape nguvu, faraja na uvumilivu Erick pamoja na familia yake katika kipindi hiki kigumu. πŸ™πŸ½πŸ•ŠοΈ

26/08/2026
Dear Wanasadaka,Tunapenda kuwajulisha habari njema ndani ya Taasisi ya Sadaka Yetu. Tumefanikiwa kupata mwingine kati ye...
24/08/2026

Dear Wanasadaka,

Tunapenda kuwajulisha habari njema ndani ya Taasisi ya Sadaka Yetu. Tumefanikiwa kupata mwingine kati yetu aliyefikia Daraja Takatifu la Upadri β€” Padri Edwin, ambaye alipadrishwa tarehe 30 Julai 2026. πŸ™β›ͺ

Kwa bahati mbaya, tulichelewa kupata taarifa zake, hivyo hatukuweza kushiriki katika tukio hilo muhimu.

Kwa sasa, Padri Edwin anategemea kuandaa Misa ya Shukrani, ambayo itafanyika nyumbani kwao Rombo. Tarehe rasmi ataitangaza mara atakapokuwa amepanga.

Jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba Padri Edwin na Padri Erasto Lekule ni marafiki na wamesoma katika chuo kimoja.

Tunampongeza sana Padri Edwin kwa hatua hii kubwa ya maisha yake ya utume. Tunamuombea Mungu amjalie hekima, nguvu, uaminifu na neema katika kulitumikia Kanisa na jamii.

Hongera sana Padri Edwin! πŸ™β€οΈβ›ͺ

Sadaka Yetu β€” Tukiungana, Tunagusa Maisha. 🀝❀️

Uongozi wa Sadaka Yetu Kanda ya Kaskazini unapenda kutoa shukrani za dhati kwa wanafamilia wote walioshiriki kwa namna m...
23/08/2026

Uongozi wa Sadaka Yetu Kanda ya Kaskazini unapenda kutoa shukrani za dhati kwa wanafamilia wote walioshiriki kwa namna mbalimbali katika michango na uwepo wao kwenye Ibada ya Misa ya Shukrani ya Padri Erasto Lekule.

Tunawashukuru kwa upendo, umoja, moyo wa kujitoa na ushirikiano wenu. Uwepo na mchango wa kila mmoja umeifanya siku hii kuwa ya kipekee na yenye kumbukumbu njema.

Mungu awabariki sana, awaongezee pale mlipopunguza, na aendelee kuimarisha umoja na mshikamano wetu.

Imetolewa na:
Afisa Habari na Mawasiliano
Taasisi ya Sadaka Yetu
22 Agosti 2026
Moshi, Tanzania

TAARIFA YA SADAKA YETU KANDA YA DAR ES SALAAM NA PWANI 08/08/2026.Jumamosi kanda ya Dar Es Salaam na Pwani  walikuwa na ...
09/08/2026

TAARIFA YA SADAKA YETU KANDA YA DAR ES SALAAM NA PWANI 08/08/2026.

Jumamosi kanda ya Dar Es Salaam na Pwani walikuwa na tukio lao maalumu la kuwaona wagonjwa hospital ya Ocean Road Dar Es Salaam .

Tukio hili lilihudhuriwa na wana sadaka wa kanda hii takribani watu 60 .Kutokana na mazingira na taratibu za hospital, hawakuhitaji kununua mahitaji yoyote kwenda nayo badala yake wana kanda walichanga sadaka zao na kufikisha kiasi cha TZS 1,000,000/= (Milioni Moja ) ambacho walienda nacho hospital !

Uongozi wa hospital ulitupatia control namba za wagonjwa 20 ambao kupitia kiasi cha TZS 1M tuliweza kusaidia malipo kidogo ya matibabu kwa kila mgonjwa ,wastani wa TZS 50,000/= kila mgonjwa alilipiwa kwenye akaunt yake ya Bill ya hospital !

Wana Sadaka wa kanda wanaushukuru Uongozi wa Sadaka Yetu ,wanasadaka wote kwa maombi na kibali katika kufaninikisha zoezi hili la jana.

Pia uongozi wa Hospital wa Ocean unatushuruku sanaa kwa majitoleo yetu ya kusaidia wahitaji ,na kwa watu mbalimbali waliokuwa hospital walishawishika kwa huduma hii na kutupatia namba zao kujiunga nasi moja kwa moja !

Mungu atubariki sote !

YETU KWA AJILI YA WENGINE!

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255755559013

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sadaka Yetu Group posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share