Wanawake Katika Jitihada Za Kimaendeleo

Wanawake Katika Jitihada Za Kimaendeleo Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Wanawake Katika Jitihada Za Kimaendeleo, Non-Governmental Organization (NGO), Dar es Salaam.

Wajiki is a non-governmental Organization Aiming to Empower Womens Socially And Economically,also We promote children rights by using Advocacy and Sensitization Activities.

Ni miaka 64 sasa tangu nchi yetu ipate uhuru,uhuru huu una maana kubwa sana kwetu k**a wananchi  Katika Jitihada Za Kima...
09/12/2025

Ni miaka 64 sasa tangu nchi yetu ipate uhuru,uhuru huu una maana kubwa sana kwetu k**a wananchi

Katika Jitihada Za Kimaendeleo tunaadhimisha siku hii maalumu kwetu Kwa kuendelea kutoa elimu na hamasa juu ya mapambano dhidi ya ukatili Kwa watoto na wanawake.

Uhuru bila haki na usawa wa Kijinsia bado sio uhuru, hivyo tuitumie siku hii Kwa kuendelea kupambana na kupinga vitendo vya ukatili katika jamii.

Salama Bila Rushwa Ya Ngono kwa wasichana na wanafunzi inawezekana,ni jukumu letu kuhakikisha watoto wanapata haki sawa bila ubaguzi na vikwazo vyovyote.
Bila Ukatili Inawezekana
Salama Bila Rushwa Ya Ngono Inawezekana.

Tukiwa katika siku 16 za Kupinga ukatili tunaendelea kutoa elimu kwa watoto  elimu na kuinua uwelewa juu ya usalama wao ...
28/11/2025

Tukiwa katika siku 16 za Kupinga ukatili tunaendelea kutoa elimu kwa watoto elimu na kuinua uwelewa juu ya usalama wao na kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili.

Katika Jitihada Za Kimaendeleo katika utekelezaji wa kampeni yetu ya SAFARI SALAMA BILA RUSHWA YA NGONO tunaimarisha club za wanafunzi za kupinga ukatili na kutoa elimu kwa watoto.

Fund Tanzania Trust, WFT Trust wanatuwezesha kufanikisha utekelezaji wa mradi wetu.Hii inatupa nguvu na kutusukuma kuwafikia watu wengi kupitia hamasa na vipeperushi vyenye ujumbe maalumu wa kupinga ukatili.
SALAMA BILA RUSHWA YA NGONO INAWEZEKANA

Katika siku 16 Za kupinga ukatili Mkurugenzi wa shirika la Wanawake Katika Jitihada Za Kimaendeleo anatia mkazo katika k...
28/11/2025

Katika siku 16 Za kupinga ukatili Mkurugenzi wa shirika la Wanawake Katika Jitihada Za Kimaendeleo anatia mkazo katika kusimamia haki na usawa, na mapambano dhidi ya ukatili ni zoezi endelevu,dhamira yetu ni kuleta usawa katika jamii na kutokomeza vitendo vya ukatili Kwa ujumla.

Katika kuhakikisha tunapiga hatua tumefungua milango Kwa wadau wengine kutoka makundi mbalimbali katika jamii na kushirikiana pamoja, ushiriki wao ni muhimu kwasababu unaleta hamasa kwa wengine na kuinua uwelewa.

Vilevile katika kampeni ya salama bila rushwa ya ngono tunashirikiana na shule mbalimbali katika kuunda na kuimarisha club za wanafunzi za kupinga ukatili.

Tunatumia club za wanafunzi kutoa elimu ya kujitambua na kujilinda kwa watoto, kupitia elimu hii mtoto anapata ufahamu na kujua wajibu wake katika kuhakikisha usalama wake.

Ushiriki wa vikundi vya Jogging pia ni njia ya kuleta hamasa kwenye jamii na kuongeza ushiriki wa pamoja katika mapambano dhidi ya ukatili.
TUNAWEZA..
SALAMA BILA RUSHWA YA NGONO INAWEZEKANA.

Siku 16 za Kupinga ukatili Katie jamii Ushiriki wa wanafunzi wa chuo kikuu na madereva katika utekelezaji wa kampeni yet...
28/11/2025

Siku 16 za Kupinga ukatili Katie jamii
Ushiriki wa wanafunzi wa chuo kikuu na madereva katika utekelezaji wa kampeni yetu ya Salama Bila Rushwa Ya Ngono kwa wasichana na wanafunzi.

Katika Jitihada Za Kimaendeleo katika kuhakikisha tunafanikiwa kutokomeza rushwa ya ngono na vitendo vya ukatili tunashirikisha makundi mbalimbali katika jamii.

Ushiriki wa madereva ni chachu ya mabadiliko Kwa wengine na kujua ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha anapinga ukatili.

Katika siku 16 za Kupinga ukatili  Katika Jitihada Za Kimaendeleo tunaendelea kuimarisha club za wanafunzi shuleni na ku...
28/11/2025

Katika siku 16 za Kupinga ukatili Katika Jitihada Za Kimaendeleo tunaendelea kuimarisha club za wanafunzi shuleni na kuendelea kutoa elimu.

Kwa ushirikiano na Fund Tanzania Trust, WFT Trust tunahamasisha makundi mbalimbali katika ushiriki wao kwenye harakati za kupinga ukatili.

Ushiriki wa madereva wa daladala na vyombo vingine vya usafiri k**a bodaboda na bajaji umeleta athari chanya na kaleta chachu ya mabadiliko Kwa wengine kuelewa na kushiriki katika utekelezaji wa kampeni ya safari salama bila rushwa ya ngono.
Rushwa Ya Ngono

We all have to live in peace, Let's stand together and raise our voices fighting against all acts of violence.  From Vio...
14/10/2025

We all have to live in peace, Let's stand together and raise our voices fighting against all acts of violence.
From Violence Is A Basic Human Right.
Nyerere Day

Today as we're celebrating   DAY OF THE GIRL CHILD,we join the global community in recognizing rights of every girl. Kat...
11/10/2025

Today as we're celebrating DAY OF THE GIRL CHILD,we join the global community in recognizing rights of every girl.

Katika Jitihada Za Kimaendeleo we stand with girls everywhere through our campaign which aimed to support and protect girls from all acts of violence.
POWER RIGHTS.

Mkurugenzi wa Shirika la  Katika Jitihada Za Kimaendeleo  Bi.Janeth Mawinza akiwa katika utekelezaji wa mradi wa safari ...
10/10/2025

Mkurugenzi wa Shirika la Katika Jitihada Za Kimaendeleo Bi.Janeth Mawinza akiwa katika utekelezaji wa mradi wa safari salama bila rushwa ya ngono kwa wasichana na wanafunzi.

Kwa ufadhili wa Fund Tanzania Trust, WFT Trust umefanikiwa kuwafikia watu wa makundi mbalimbali na kutoa elimu juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili.

Elimu na hamasa inainua uwelewa mkubwa kwa wale wasiojua wajibu wao, hivyo kupitia kampeni hii ya safari salama bila rushwa ya ngono tunahamasisha na wadau wadau wengine kushiriki kikamilifu katika harakati hizi.
Tunaweza.
RUSHWA YA NGONO UKATILI

Zoezi la kutoa elimu Kwa watoto ni endelevu na ni jambo la kitiliwa mkazo sana,tukiwaelimisha watoto wetu jinsi ya kuepu...
03/10/2025

Zoezi la kutoa elimu Kwa watoto ni endelevu na ni jambo la kitiliwa mkazo sana,tukiwaelimisha watoto wetu jinsi ya kuepuka na kujilinda dhidi ya ukatili tutawapa uwezo wa kujitambua.

Katika Jitihada Za Kimaendeleo Katika kuhakikisha tunatoa elimu Kwa watoto tumeanzisha klabu za watoto shuleni na kutoa elimu pia kuwapa nafasi ya kujielezea Kwa uhuru.

Fund Tanzania Trust, WFT Trust wanatusapoti na kutusaidia Katika utekelezaji wa mradi wetu wa SAFARI SALAMA BILA RUSHWA YA NGONO.
Ukatili Rushwa Ya Ngono
Mtoto
SAFARI SALAMA BILA RUSHWA YA NGONO INAWEZEKANA.

Thank you  Fund Tanzania Trust, WFT Trust for enabling us. As we fight against all forms of violence we must educate our...
02/10/2025

Thank you Fund Tanzania Trust, WFT Trust for enabling us. As we fight against all forms of violence we must educate our communities especially the youth and children about consent equality and respect.

Katika Jitihada Za Kimaendeleo we establish students clubs in school and talk to them friendly,we also educate them about all acts of violence and how to avoid.
Awareness.
the Silence Violence.
https://whatsapp.com/channel/0029VbBBxbWI1rck7uV2PJ2p

Kila sehemu yenye mkusanyiko wa watu sisi  Katika Jitihada Za Kimaendeleo  kwetu ni sehemu ya kutoa elimu na hamasa kuhu...
02/10/2025

Kila sehemu yenye mkusanyiko wa watu sisi Katika Jitihada Za Kimaendeleo kwetu ni sehemu ya kutoa elimu na hamasa kuhusu mapambano dhidi ya Ya Ngono na ukatili kwenye jamii yetu.

Kwa ufadhili wa Fund Tanzania Trust, WFT Trust Tunatumia njia nyingi katika kuhakikisha tunafikisha ujumbe Kwa haraka, tunatumia vipeperushi vyenye meseji za uhamasishaji na uelimishaji jamii.

Vilevile tunatumia stika Kwa kubandika kwenye vyombo vya usafiri k**a daladala,bajaji na pikipiki.Hii ni kwasababu tunataka elimu ifike Kwa watu wote.
Ukatili Rushwa ya ngono.
https://whatsapp.com/channel/0029VbBBxbWI1rck7uV2PJ2p

Rushwa ya Ngono haikubaliki  Katika Jitihada Za Kimaendeleo tunasonga mbele katika kuhakikisha tunafanikiwa kufikisha uj...
02/10/2025

Rushwa ya Ngono haikubaliki Katika Jitihada Za Kimaendeleo tunasonga mbele katika kuhakikisha tunafanikiwa kufikisha ujumbe kwenye jamii na kuleta mabadiliko chanya.

Tunashukuru Fund Tanzania Trust, WFT Trust kwa ufadhili wa kuhakikisha tunafanikisha mradi wa safari salama bila rushwa ya ngono Kwa wasichana na wanafunzi

Mapambano dhidi ya ukatili ni endelevu na juhudi za makusudi zinahitajika ili tuweze kufanikiwa kutokomeza rushwa ya ngono kabisa.
Sauti Ukimya Rushwa ya Ngono.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wanawake Katika Jitihada Za Kimaendeleo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share