07/05/2026
Leo, Mei 07, 2026, tumepata fursa ya kushiriki kikao cha Bunge jijini Dodoma kikao muhimu sana kwa sekta ya elimu nchini, ambapo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf F. Mkenda (Mb), amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2026/27 ya wizara hiyo. 📚✨
Katika hotuba hiyo ya bajeti iliyoongozwa na kauli mbiu ya “Uwekezaji katika Elimu na Ujuzi, Sayansi na Teknolojia kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi na Shindani”, Prof. Mkenda amesema kuwa lengo ni kuwa na Mtanzania aliyeelimika, mwenye maarifa, stadi na mtazamo chanya utakaomwezesha kuchangia maendeleo endelevu ya Taifa.
Aidha, ili kuwezesha utekelezaji wa malengo yaliyoanishwa kwa mwaka wa fedha 2026/27, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 2,394,423,829,000.00. Moja ya vipaumbele vya wizara ni kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya awali, msingi, sekondari pamoja na ualimu nchini. 🙌🏽
tunapongeza hatua hii muhimu katika kuendelea kuimarisha sekta ya elimu nchini, hususan jitihada za kuandaa Kiunzi cha Kitaifa cha Uboreshaji wa Vituo vya Walimu (Teacher Resource Centers – TRC) ili vitumike k**a kumbi za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) pamoja na Teknolojia za Kidijitali (DigiSTEM Hubs).💡
TEN/MET tutaendelea kuunga mkono jitihada hizi katika kuhakikisha uwepo wa elimu bora, jumuishi na inayomwandaa Mtanzania wa sasa na wa baadaye. 🌍
đź“– ElimuKwaMaendeleo