24/09/2026
Tarehe 23 Septemba 2026, TAWASANET kupitia mashirika wanachama, HAPA na TTI, ilishiriki katika kipindi cha redio kupitia Standard Radio FM ya Singida, kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira.
Mazungumzo hayo yalilenga katika masuala mbalimbali, ikiwemo umuhimu wa usafi wa mazingira kwa afya ya jamii, ujenzi na matumizi sahihi ya vyoo bora, madhara ya kujisaidia katika maeneo ya wazi, upatikanaji na matumizi ya maji safi na salama, pamoja na umuhimu wa huduma bora za maji, vyoo na unawaji mikono shuleni na vituo vya huduma za afya.
Uhamasishaji huu ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa “Maji Salama, Usafi wa Mazingira kwa Heshima na Maisha Bora ya Baadaye, unaotekelezwa na TAWASANET katika wilaya za Singida na Ikungi Mkoani Singida.