16/04/2025
Reposted from
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono maazimio yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kimataifa wa Beijing -China (miaka 30 iliyopita) kwa lengo kuwawezesha wanawake na kuhakikisha wanaendelea kufanikiwa kupitia nyanja mbalimbali iwe za kiuchumi, kisiasa, kijamii nk
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha Hamadi Chande alipozungumza k**a mgeni maalum kwenye hafla ya kusherehekea mafanikio ya Beijing 30+ hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam leo, Jumatano Aprili 16.2025
Akizungumza katika halfa hiyo, Chande amesema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mara zote imekuwa ikitafsri kwa vitendo maazimio ya mkutano huo kwani kupitia yeye (Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan) wanawake wamekuwa wakituliwa ndoo kichwani kupitia mpango wa serikali wa kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana karibu na makazi ya wananchi
Kuimarishwa kwa miundombinu ya mawasiliano k**a vile barabara, kuimarisha huduma za afya katika jamii, kusimamia kidete suala la nishati safi nk ni sehemu ya masuala machache yanayoendelea kupewa mkazo mkubwa serikalini, ambapo kuimarishwa kwa sekta hizo kumesawadia wanawake kwa kiasi kikubwa kwani wao ndio waathirika wakubwa pindi huduma hizo zinapokosekana
Katika hatua nyingine, Chande amewaeleza wanaharakati wanawake waliohudhuria hafla hiyo kuwa wanawake kwa ujumla wake wanapaswa kutambua kuwa wana uwezo mkubwa wa kuvumbua vipaji, kwani hata yeye mwenyewe ni mama aliyemuambia kuwa unaweza kuingia kwenye siasa akafanya vizuri, jambo ambalo alilipokea na limempa manufaa
"Kazi yenu ni nzuri sana, na kazi yenu kwa kweli inahitaji motisha kwelikweli, na mimi niwahakikishieni tutakua pamoja, tutafanya yote yanayowezekana kushirikiana kuendeleza harakati hizi" -Chande
"Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi nendeni mkawaambie vijana wasikubali kushawishiwa kuvunja amani ya nchi yao, nendeni mkatoe elimu kwa watu wetu wakina mama na ikiwezekana hata akina baba, wanasema ukimuelimisha mwanamke mmoja basi dunia imeelimika" -Chande.
Reposted from