07/05/2026
Leo ni hatua muhimu kwa Liberty Sparks baada ya kusaini rasmi Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) na Tanzania National Chamber of Commerce (TNCC).
Ushirikiano huu unaonesha dhamira ya pamoja katika kuendeleza uwezeshaji wa kiuchumi, ukuaji wa sekta binafsi, ujasiriamali, tafiti, mijadala ya sera, pamoja na ubunifu wa vijana nchini Tanzania. Kupitia makubaliano haya, taasisi hizi mbili zitashirikiana kuimarisha mafunzo na kujenga uwezo, kuongeza fursa jumuishi za kiuchumi, kusaidia ushiriki wa wadau mbalimbali, wanawake na vijana katika biashara, pamoja na kuunda majukwaa yanayounganisha mawazo, sera, na matokeo yenye impact kwa jamii.
Makubaliano haya pia yanafungua fursa mpya za mafunzo ya pamoja, forums, tafiti, ushirikishwaji wa wadau, na shughuli za utetezi wa sera zinazolenga kukuza maendeleo endelevu ya kiuchumi na kuimarisha mazingira ya biashara nchini Tanzania.
Makubaliano haya yameongozwa na Evans Exaud, Mkurugenzi wa Liberty Sparks, pamoja na Oscar Kisanga, Mkurugenzi wa TNCC.
Tunaamini ushirikiano wa kimkakati ni msingi muhimu katika kujenga taifa lenye ubunifu, uhuru wa kiuchumi, na ustawi wa pamoja.