15/07/2026
Empowering Girls with Knowledge, Confidence, and Life Skills
Today, as we commemorate World Youth Skills Day 2026, TASI recognises that empowering young people goes beyond vocational skills. Health education and life skills are equally important in enabling young people, especially girls, to participate fully in education and community life.
As part of the continued commemoration of World Menstrual Hygiene Day, TASI, in collaboration with the management of the UMISETA training camp under Mtama District Council, conducted a sanitary pad distribution activity at Mahiwa Secondary School. A total of 80 female students attending the UMISETA preparation camp received sanitary pads. The students also benefited from health education sessions delivered by qualified health professionals on proper menstrual hygiene management, the correct use of sanitary pads, and ways to address common menstrual health challenges.
Together, we are building a future where every young person has the knowledge, skills, confidence, and support needed to reach their full potential.
…………………………………………………………………………………
Tunapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya Stadi kwa Vijana 2026, TASI inatambua kuwa kuwawezesha vijana hakuishii tu kwenye stadi za ufundi na mafunzo ya kazi. Elimu ya afya, kujiamini, kujitunza na stadi za maisha ni muhimu pia katika kuwawezesha vijana, hususan wasichana, kushiriki kikamilifu katika elimu, michezo na maisha ya kijamii.
K**a sehemu ya mwendelezo wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Afya na Usafi wa Hedhi, TASI, kwa kushirikiana na uongozi wa kambi ya maandalizi ya UMISETA chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, ilifanya zoezi la kugawa taulo za k**e katika Shule ya Sekondari Mahiwa. Jumla ya wanafunzi 80 wa k**e waliokuwa wakishiriki kambi ya maandalizi ya UMISETA walipatiwa taulo za k**e. Aidha, wanafunzi hao walipata elimu kutoka kwa wataalamu wa afya kuhusu usimamizi sahihi wa afya na usafi wa hedhi, matumizi sahihi ya taulo za k**e, pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa hedhi.
Happy World Youth Skills Day 2026!
#