Tanzania Women Chamber of Commerce

Tanzania Women Chamber of Commerce 20 Years of Women Economic Empowerment �
Our services:
�Capacity Building & Advocacy
�Financial Linkages & Marketing
�Networking �

�Website: www.twcc-tz.org

Members are only Women and Women owned & Led Companies

13/05/2026

TWCC MWANZA WASHEREHEKEA MIAKA 20 YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

JE ULIKUWA BADO HUJAKAMILISHA MALIPO YAKO KUSHIRIKI MAFUNZO🔥 USIKOSE NAFASI YA KUJIFUNZA NA KUANZA KUSHINDA ZABUNI! 🔥⚠️ ...
13/05/2026

JE ULIKUWA BADO HUJAKAMILISHA MALIPO YAKO KUSHIRIKI MAFUNZO

🔥 USIKOSE NAFASI YA KUJIFUNZA NA KUANZA KUSHINDA ZABUNI! 🔥

⚠️ *Muda Umeongezwa kwa Nafasi chache zilizobaki , lipia sasa kabla siku kuisha.*

Mafunzo ni kesho , hivyo baada ya leo usajili utafungwa ili kutoa nafasi kwa washiriki waliokamilisha malipo mapema.

✅ Ukishafanya malipo:
• Tuma uthibitisho wa malipo mara moja
• Hakikisha nafasi yako kwenye mafunzo
• Pata nafasi ya kujifunza mbinu za kushinda zabuni kwa vitendo

🎯 Nafasi ni chache na wanaolipa mapema ndio watakaopewa kipaumbele.

📞 Mawasiliano:
0757 823 982

💳 MALIPO YAFANYIKE LEO KUPITIA:

1️⃣ CRDB Bank
Jina la Akaunti: Tanzania Women Chamber of Commerce
Namba ya Akaunti: *01J1029021100*

2️⃣ M-Pesa: 0757823982
Jina: Tanzania Women Chamber of Commerce

3️⃣ Lipa Namba Vodacom
*50924801*
Jina: Tanzania Women Chamber of Commerce

TWCC – Tunakuwezesha kufikia fursa na kushinda zabuni.

🚨 MAFUNZO KWA WANAWAKE NA VIJANA KUSHIRIKI FURSA ZA ZABUNI 🚨Changamkia fursa ya kujifunza jinsi ya kuomba na kushinda za...
12/05/2026

🚨 MAFUNZO KWA WANAWAKE NA VIJANA KUSHIRIKI FURSA ZA ZABUNI 🚨

Changamkia fursa ya kujifunza jinsi ya kuomba na kushinda zabuni (tenda) kwa ufanisi.

TWCC inakuletea mafunzo maalum ya vitendo yatakayokupa ujuzi wa:
✔️Usajili kwenye mifumo ya zabuni k**a NeST na mifumo mingine ya nje ya nchi
✔️Kutafuta na kuomba zabuni kwa usahihi,
✔️Kuandaa nyaraka za zabuni bila makosa
✔️Mbinu za bei shindani na kushinda zabuni
✔️Kuepuka makosa yanayokatisha maombi na kushinda zabuni za serikali, binafsi na kimataifa.

📅 Tarehe 14–15 Mei 2026
📍 Mahali: Dar es Salaam
💰 Ada: TZS 50,000/-

👉Bofya link hii kujiunga na group kwa ajili ya taarifa zaidi https://chat.whatsapp.com/GVp92ZVf0ekLO2913nQ2ZH

📝 Jisajili kupitia: https://forms.gle/UrGYeaXoQndwi27g9
⏳ Mwisho wa usajili: 12 Mei 2026

📞 Kwa Mawasiliano zaidi: 0757 823 982

Usikose nafasi ya kukuza biashara yako kupitia fursa za zabuni!

12/05/2026

MADA KUU | FURSA NA CHANGAMOTO YA BIASHARA NA UWEKEZAJI AFRIKA

Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Biashara Tanzania TWCC, Dkt. Mwajuma Hamza akichangia mada TBC kuonesha fursa zilizopo kwenye Biashara na Uwekezeji barani Afrika na kwa kiasi gani TWCC imejidhatiti kuwawezesha wanawake Kiuchumi na kutumia fursa kikamilifu zinazojitokeza.

11/05/2026

ZIARA ZA MARAIS WAWILI WA AFRIKA MASHARIKI JE, KUNA MANUFAA GANI KWA WATANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Biashara Tanzania TWCC, Dkt. Mwajuma Hamza akichangia mada kuonesha fursa zilizopo kwenye ziara hizi za Marais wawili wa Afrika mashariki ndani ya Kipindi cha Kipima Joto kinachorushwa na ITV.

TWCC YAONGOZA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA JUKWAA LA BIASHARA TANZANIA NA KENYATarehe 4, Mei 2026DAR ES SALAAM: Rais wa C...
07/05/2026

TWCC YAONGOZA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA JUKWAA LA BIASHARA TANZANIA NA KENYA

Tarehe 4, Mei 2026
DAR ES SALAAM:

Rais wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Biashara Tanzania TWCC, CPA Mercy Silla, amewaongoza wanawake wajasiriamali nchini kushiriki Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Kenya, lililofanyika tarehe 4 Mei 2026 katika ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam.

Kongamano hilo lililobeba kaulimbiu ya "Kufungua Ukuaji wa Sekta Binafsi na Uwekezaji," lilikusanya wadau wa kibiashara na viongozi wa kitaifa kutoka Tanzania na Kenya kwa lengo la kujadili fursa za biashara na uwekezaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika kongamano hilo, alikumbusha kuwa ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa haya mawili ni muhimu zaidi kuliko ushindani usio na manufaa. Kwa upande wake, Rais wa Kenya, Mhe. Dkt. William Ruto, alisisitiza kuwa nchi hizi zina uwezo wa kukuza thamani ya biashara kufikia dola bilioni moja zikifanya kazi k**a mfumo mmoja. Viongozi wote wawili walibainisha kuwa sekta binafsi ndiyo mhimili mkuu wa kukuza uchumi katika nchi hizi mbili.

Katika hatua nyingine, kupitia kongamano hili imehimizwa uimarishaji wa miundombinu ya nishati, mawasiliano, na sera za kodi zinazotabirika ili kurahisisha ufanyaji biashara.

Katika kuelekea utekelezaji wa vitendo, kongamano hilo limefungua ukurasa mpya kwa kuoanisha mifumo ya ukaguzi wa ubora kupitia mashirika ya TBS na KEBS, pamoja na kuanzisha Baraza la Biashara la Pamoja. Miradi ya kimkakati, ukiwemo ujenzi wa bomba la gesi kuelekea Mombasa na kuunganisha reli ya kisasa (SGR), ilitajwa k**a vipaumbele vya kuchochea kasi ya uchumi.

Aidha, washiriki walishuhudia kusainiwa kwa Tamko la Pamoja la Makubaliano (Joint Communique) na mikataba ya ushirikiano kati ya Taasisi mbalimbali za uwezeshaji biashara kutoka Tanzania na Kenya. Mikataba hiyo inaweka mkakati madhubuti wa kuongeza ushindani wa bidhaa za Kitanzania nchini Kenya na kanda nzima ya Afrika Mashariki, huku ikipunguza gharama za mawasiliano kupitia mfumo wa "One Network Area."

📊 NGUVU YA BIASHARA YAKO NI UWEZO WA KUTUNZA DATA NA KUMBUKUMBUJe, unataka biashara yako iwe na usimamizi wa kisasa, tak...
02/05/2026

📊 NGUVU YA BIASHARA YAKO NI UWEZO WA KUTUNZA DATA NA KUMBUKUMBU

Je, unataka biashara yako iwe na usimamizi wa kisasa, takwimu sahihi, na faida inayoonekana wazi? Sasa inawezekana kupitia mfumo wa TunzaDuka – suluhisho rahisi na bora la kurekodi mauzo, matumizi, na kufuatilia mwenendo wa biashara yako kila siku. 💼📈

👩🏽‍💼👨🏽‍💼 Wapendwa wafanyabiashara, mnakaribishwa kuanza kutumia mfumo huu ambao utakusaidia kusimamia biashara yako kwa ufanisi zaidi.

🔰 Hatua Rahisi za Kuanza

🌐 Jisajili sasa: tunzaduka.twcc-tz.org

Tembelea tovuti ya TunzaDuka na ujaze taarifa za biashara yako.
Chagua aina ya biashara k**a Retail, Wholesale, au nyingine inayofanana na biashara yako.

💳 Chagua Kifurushi Kinachokufaa

🥈 Silver – Tsh 10,000
• Hifadhi taarifa za bidhaa 500
• Inaruhusu Watumiaji 3

🥇 Gold – Tsh 15,000
• Inahifadhi hadi bidhaa 2,000
• Watumiaji 10
• Advanced Analytics

💎 Premium – Tsh 20,000
• Bidhaa Unlimited
• API Access kwa matumizi ya juu zaidi

🎁 Pata Punguzo Maalum
Ukilipia kuanzia miezi 3 (punguzo la 7–8%) hadi miezi 12, utapata punguzo kubwa zaidi na kuokoa gharama za uendeshaji wa mfumo. 💰

⭐ Kwanini Utumie TunzaDuka?

✅ Inarekodi mauzo yote kiotomatiki na kupunguza stock papo hapo
📦 Inatoa tahadhari pale stock inapokuwa imepungua
📊 Inachambua bidhaa zinazouza zaidi
💹 Inakupatia ripoti sahihi za faida na hasara ili kufanya maamuzi bora ya biashara

🚀 Chukua hatua leo – simamia biashara yako kwa weledi na takwimu sahihi kwa kutumia TunzaDuka!

Kwa maelezo na Msaada zaidi: 0757 823 982

TUNZA KUMBUKUMBU ZAKO ZA MAUZO, MANUNUZI FAIDA NA MATUMIZI KWA URAHISI KUPITIA MFUMO WA KIDIGITALI💼📊

Ndugu Wanachama, Wakurugenzi na Menejimenti ya TWCC,Tuungane kwa pamoja kumpongeza mfanyakazi hodari wa TWCC kwa mwaka 2...
01/05/2026

Ndugu Wanachama, Wakurugenzi na Menejimenti ya TWCC,

Tuungane kwa pamoja kumpongeza mfanyakazi hodari wa TWCC kwa mwaka 2025/2026 🎉👏

Hongera sana kwa juhudi zako, kujituma na mchango wako mkubwa katika kuendeleza malengo ya taasisi yetu. Umeonyesha weledi, ubunifu pamoja na nidhamu ya hali ya juu katika utekelezaji wa majukumu yako, sifa zinazokutofautisha na kukufanya ustahili heshima hii.

Tunakutakia mafanikio zaidi katika majukumu yako na tunaamini utaendelea kuwa chachu ya mafanikio ndani ya TWCC 🌟

TeamWork

🌍 Heri ya Siku ya Wafanyakazi Duniani! 💼✨Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wanachama wote wa Chemba ya Wanawake Wafany...
01/05/2026

🌍 Heri ya Siku ya Wafanyakazi Duniani! 💼✨

Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wanachama wote wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) tunawatakia Watanzania wote heri ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.

Tunaendelea kuthamini mchango mkubwa wa wafanyakazi katika kukuza uchumi na maendeleo ya taifa letu 🇹🇿

🤝 Endelea kufuatilia kwa karibu kazi na juhudi zinazofanywa na TWCC katika kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia majukwaa yetu ya mitandao ya kijamii na tovuti:

📸 Instagram: https://www.instagram.com/tzwomenchamber_twcc?igsh=MW5vMDNhejVlYjhqMw==

▶️ YouTube: https://youtube.com/live/dRw1mgUvWx4?feature=share

📘 Facebook: https://www.facebook.com/share/17xqsT9qPT/

💼 LinkedIn: https://www.linkedin.com/in/tanzania-women-chamber-of-commerce-twcc-88578a339?utm_source=share&utm_campaign=share_via&utm_content=profile&utm_medium=android_app

🌐 Website: [www.twcc-tz.org](http://www.twcc-tz.org)

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Women Chamber of Commerce posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share