03/08/2026
Kupitia mradi wetu wa HER Future unaotekelezwa mkoani Arusha, tunaendelea kuimarisha uwezo wa watoa huduma za afya ili kuhakikisha jamii inapata huduma bora na zenye ubora.
Katika mafunzo haya, washiriki wanajengewa uwezo kuhusu misingi ya uzazi wa mpango, afya ya uzazi wa mama, mabadiliko ya kisaikolojia baada ya kujifungua, pamoja na mzunguko wa hedhi. Vilevile, wanajifunza kutoa elimu na ushauri nasaha kwa wateja, kufanya uchunguzi wa awali kabla ya kutoa huduma za uzazi wa mpango, na kutumia kwa usalama njia mbalimbali za kisasa za uzazi wa mpango ikiwemo IUCD, vipandikizi, sindano na vidonge.
Mafunzo haya yanajumuisha mazoezi ya vitendo, usimamizi wa takwimu, pamoja na kuimarisha utoaji wa Huduma Rafiki kwa Vijana (AYFS) na Comprehensive Post Abortion Care (cPAC), hatua inayochangia kuboresha ubora wa huduma zinazotolewa katika vituo vya afya.
Kwa pamoja, tunaendelea kujenga mfumo wa afya wenye wataalamu wenye ujuzi, huduma zenye ubora, na jamii yenye afya bora.
Pathfinder International Pastoral Women’s Council | Indigenous women-led non-profit 🇹🇿 RS Arusha Wizara Ya Afya Embassy of Ireland in Tanzania