Legal and Human Rights Centre

Legal and Human Rights Centre Legal and Human Rights Centre (LHRC)
is the Tanzania’s human rights advocacy organization.

Legal and Human Rights Centre
is the Tanzania’s human rights advocacy organisation established in 1995 as a non-governmental, voluntary, non-partisan and not-for-profit sharing organisation, with the purpose
of protecting and promoting human rights. LHRC was established in 1995 as a non-governmental, voluntary, non-partisan and not-for-profit sharing organization, with the purpose
of working to empower and conscientize the people of Tanzania on legal and human rights.

Mapema wiki hii Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)  kilishiriki mhadhara wa umma ulioandaliwa na Chuo Kikuu Mzu...
04/06/2026

Mapema wiki hii Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilishiriki mhadhara wa umma ulioandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam, uliolenga kuongeza uelewa wa wanafunzi kuhusu nafasi ya haki za binadamu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Katika mhadhara huo ulioongozwa na mada isemayo “Haki, Biashara na Huduma: Mtazamo wa Haki za Binadamu katika Utoaji wa Huduma za Kijamii na Kiuchumi Tanzania,” LHRC iliwakilishwa na Afisa wa Haki za Binadamu na Biashara, Bw. Clay Mwaifwani, ambaye aliwasilisha mada na kuongoza majadiliano kuhusu umuhimu wa kuzingatia haki za binadamu katika utoaji wa huduma za kijamii na utekelezaji wa shughuli za kiuchumi.

Akizungumza wakati wa mhadhara huo, Mwaifwani alieleza kuwa maendeleo ya kiuchumi yanapaswa kuzingatia haki za binadamu ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wananufaika kwa usawa huku akisisitiza juu ya wajibu taasisi za umma na binafsi kuzingatia misingi ya uwajibikaji, ushirikishwaji na usawa katika utoaji wa huduma na utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

Hatahivyo, Mwaifwani aliwahimiza wanafunzi kutumia elimu na maarifa wanayoyapata chuoni kuchangia maendeleo ya jamii kwa kuzingatia misingi ya haki, maadili na uwajibikaji, akibainisha kuwa vijana wana nafasi muhimu katika kuhamasisha na kutetea haki za binadamu kupitia taaluma na ushiriki wao katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Kupitia ushirikiano na taasisi za elimu ya juu, LHRC inaendelea kuhamasisha mijadala kuhusu haki za binadamu na biashara, na uwajibikaji wa wawekezaji pamoja na ulinzi wa walaji wa bidhaa na hudumakwa maendeleo jumuishi na endelevu.

LHRC inawakaribisha wadau wote kushiriki mkutano kwa njia ya Zoom kuhusu tathmini ya Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na ...
28/05/2026

LHRC inawakaribisha wadau wote kushiriki mkutano kwa njia ya Zoom kuhusu tathmini ya Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (NCCRS 2021-2026) utakaofanyika kesho, Mei 29, 2026, kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana.

Jisajili hapa ili uweze kushiriki. https://us06web.zoom.us/webinar/register/WN_Ip9282sTRamoeyg5CBrPHg

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinawatakia Kheri ya Siku ya Hedhi Duniani 2026 “Pamoja kwa Dunia Rafiki kwa...
28/05/2026

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinawatakia Kheri ya Siku ya Hedhi Duniani 2026

“Pamoja kwa Dunia Rafiki kwa Hedhi” tuendelee kuvunja ukimya, kuondoa unyanyapaa na kuhakikisha kila
msichana na mwanamke anapata elimu, heshima na huduma salama za hedhi.

Hedhi ni jambo la kawaida, si aibu.
🇹🇿

Mabadiliko ya tabianchi ni suala la haki za binadamu.Jiunge nasi kwenye mjadala muhimu kuhusu tathmini ya utekelezaji wa...
26/05/2026

Mabadiliko ya tabianchi ni suala la haki za binadamu.

Jiunge nasi kwenye mjadala muhimu kuhusu tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (NCCRS 2021–2026).

📅 Ijumaa, 29 Mei 2026
🕔 Saa 5:00 Asubuhi – Saa 7:00 Mchana
💻 Kupitia Zoom jisajili kwa link hii
👇🏾👇🏾👇🏾https://us06web.zoom.us/webinar/register/WN_Ip9282sTRamoeyg5CBrPHg

TAARIFA KWA  UMMAKituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) tunalaani na kupinga vikali kurejea kwa kasi kwa matukio ye...
22/05/2026

TAARIFA KWA UMMA

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) tunalaani na kupinga vikali kurejea kwa kasi kwa matukio yenye sura ya utekaji nchini, kwani ni tishio kwa uhuru wa raia, usalama wa wananchi pamoja na utawala wa sheria.

Tunatoa wito kwa vyombo vya dola kuhakikisha sheria, taratibu za ukamataji na haki za msingi za binadamu zinazingatiwa ili kurejesha imani ya wananchi na kulinda misingi ya demokrasia na haki nchini.

TAARIFA KWA UMMA.Leo, Mei 5, 2026, LHRC inalaani vikali kuibuka kwa matukio ya kuokotwa kwa miili ya watu waliopoteza ma...
05/05/2026

TAARIFA KWA UMMA.

Leo, Mei 5, 2026, LHRC inalaani vikali kuibuka kwa matukio ya kuokotwa kwa miili ya watu waliopoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha. Aidha, LHRC inaonesha wasiwasi mkubwa juu ya ukimya wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu matukio haya. |

K**a ilivyoelezwa katika tamko rasmi, hatua za haraka, za uwazi na uwajibikaji zinahitajika ili kulinda haki ya kuishi ya kila Mtanzania.

Heri ya Siku ya Wafanyakazi Duniani – Mei Mosi, 2026Leo tunaadhimisha nguvu, mchango, na ustahimilivu wa wafanyakazi dun...
01/05/2026

Heri ya Siku ya Wafanyakazi Duniani – Mei Mosi, 2026

Leo tunaadhimisha nguvu, mchango, na ustahimilivu wa wafanyakazi duniani kote. Kazi yenye staha, mazingira salama na yenye afya ya kisaikolojia ni haki ya msingi kwa kila mfanyakazi.

LHRC tunaungana na wafanyakazi duniani kote kuendeleza utu, usawa na haki mahali pa kazi.

Kwa jamii yenye haki na usawa.

Wanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wakiwa katika banda la LHRC wakitoa msaada wa kisheria na kuto...
30/04/2026

Wanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wakiwa katika banda la LHRC wakitoa msaada wa kisheria na kutoa elimu ya haki kwa wadau mbalimbali waliofika katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani jijini Arusha.

Dkt. Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), akiwa katika banda la LHRC akitoa m...
30/04/2026

Dkt. Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), akiwa katika banda la LHRC akitoa msaada wa kisheria na kusambaza machapisho ya haki za binadamu kwa wadau mbalimbali waliofika kupata huduma hiyo, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani jijini Arusha, ambapo msisitizo wake mkubwa umekuwa ni umuhimu wa kulinda na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini.

“Ni muhimu kwa serikali kuhakikisha mazingira salama na huru kwa vyombo vya habari. Hofu na vitisho vinawazuia wanahabari kutekeleza majukumu yao ipasavyo, hivyo kuna haja ya kufanya marekebisho ya sheria na sera ili wanahabari wafanye kazi bila hofu,” — Dkt. Anna Henga.

Wadau mbalimbali wakiendelea kutembelea banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) katika kilele cha maadhimis...
30/04/2026

Wadau mbalimbali wakiendelea kutembelea banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yanayoendelea leo tarehe 30 Aprili 2026 jijini Arusha katika Hoteli ya Mount Meru.

Kupitia banda hilo, LHRC imeendelea kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa umma, sambamba na kusambaza machapisho ya haki za binadamu na kutoa elimu ya uelewa wa sheria, ikiwa ni juhudi za kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu haki zao, utawala bora na upatikanaji wa haki.

Wito wa LHRC: Kuna haja ya kuchukua hatua za haraka katika kulinda na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini, ikiwa ni pamoja na kufanya marekebisho ya sheria na sera ili kuweka mazingira salama na wezeshi kwa wanahabari kutekeleza majukumu yao bila hofu.

Address

Justice Lugakingira House/Kijitonyama
Dar Es Salaam
75254

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Telephone

+255222773038

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Legal and Human Rights Centre posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Legal and Human Rights Centre:

Share