18/03/2026
✊🏽🔥
Leo, tumepata fursa ya kipekee kushiriki katika kikao cha kujifunza na kubadilishana mawazo kati ya vijana kutoka asasi za kiraia na viongozi wa Wizara ya Vijana.
Katika kikao hicho, tulikutana na Mheshimiwa Waziri wa Vijana pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, ambapo tulijadili juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kukuza ajira, ubunifu, na fursa kwa vijana nchini.
Majadiliano haya yameendelea kuimarisha uelewa wa pamoja na kufungua njia mpya za ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo ya vijana.
Tunaamini kuwa kupitia ushirikiano, ubunifu, na hatua madhubuti, tunaweza kusukuma mbele ajenda ya vijana na kuleta mabadiliko chanya yenye tija kwa Taifa.
Tunaendelea kujifunza, kushirikiana, na kuchukua hatua. 💡🇹🇿
AgendaNiVijana