Community Development Trust Fund

Community Development Trust Fund CDTF has the purpose of complementing efforts of the nation on improving people's social and economi

Tunawatakia Kheri ya Siku ya Karume na siku njema yenye furaha na mafanikio Tuendelee kuthamini umoja,upendo na amani kw...
07/04/2026

Tunawatakia Kheri ya Siku ya Karume na siku njema yenye furaha na mafanikio

Tuendelee kuthamini umoja,upendo na amani kwa maendeleo ya taifa letu

Msimu huu unatukumbusha kitu kimoja kuwa tupo pamoja.Upendo ,matumaini na kusaidiana ndio msingi wa jamii bora Cdtf Trus...
05/04/2026

Msimu huu unatukumbusha kitu kimoja kuwa tupo pamoja.

Upendo ,matumaini na kusaidiana ndio msingi wa jamii bora

Cdtf Trust inaendelea kusimama nanyi kwenye kila hatua .

hope ,changing lives

Wafanyakazi Cdtf Trust ,NGO ,Enterprises wakiwa kwenye picha ya pamoja na washauri kutoka Liheta Consulting Services baa...
20/02/2026

Wafanyakazi Cdtf Trust ,NGO ,Enterprises wakiwa kwenye picha ya pamoja na washauri kutoka Liheta Consulting Services baada ya kikao cha Tathmini , Kilichofanyika katika Ofisi za Cdtf Trust tarehe 19/2/2026

https://www.facebook.com/photo?fbid=122113408659139992&set=a.122113409379139992
16/01/2026

https://www.facebook.com/photo?fbid=122113408659139992&set=a.122113409379139992

Asasi ya Maendeleo ya Jamii na Mabadiliko (CDTF NGO) kwa kushirikiana na watalaamu wa Halmashauri ya Mlimba walihamasisha wanakijiji wa Kijiji cha Tanganyika, kata ya Masagati, wilaya ya Mlimba, Mkoa wa Morogoro kuhusu utunzaji mazingira na ufugaji nyuki ili kutoa fursa kwa vijana wengi kukuza kipato chao kupitia shughuli endelevu zinazolinda mazingira.

Wananchi wakiwemo wakulima, wafugaji wa nyuki, vijana, wanawake, Viongozi wa Serikali ya Mtaa na Kata, pamoja na wadau mbalimbali walihudhuria na walipata fursa ya kujifunza kuhusu umuhimu wa utunzaji mazingira na ufugaji nyuki.Uhamasishaji ulilenga kuwaandaa wananchi hasa vijana kujihusisha na shughuli endelevu za kuwapatia kipato huku wakilinda misitu na mazingira.

Akizungumza na Wanakikijiji waliohudhuria katika Mkutano huo Bw. Justine Chaki, Afisa Ufugaji Nyuki Kata ya Masagati aliwahimiza kutumia mbinu bora za ufugaji nyuki ikiwemo matumizi ya mizinga yenye tija, usimamizi wa mizinga na uvunaji. Aliongeza kuwa ubora wa mazao ya nyuki unatakiwa kuzingatia uvunaji, uchakataji na uhifadhi wake.

Nae Bw. Sakumi Mwikwabe, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Masagati alihimiza wananchi hasa vijana kujiunga kwenye vikundi ili iwe rahisi kutekeleza miradi yao kwa ushirikiano. Aliomba CDTF NGO kutoa mafunzo ya kina ili yawasaidie kufuga, kutafuta masoko ya uhakika wa bidhaa zao.

Bi. Letisia Matikila Mkazi wa Kijiji cha Tanganyika alishukuru elimu aliyoipata iliyowatia hamasa ya kutunza mazingira na kushiriki kwenye vikundi kufuga nyuki. Alianisha changamoto waliyokuwa nayo ni mtaji na masoko katika sekta ya ufugaji nyuki.

Asasi ya Maendeleo ya Jamii na Mabadiliko (CDTF NGO) inafanya kazi na Jamii kubadilisha maisha yao yawe bora. Asasi ilianzishwa mwaka 2005 chini ya Community Development Trust Fund na ilihuisha usajili wake mwaka 2023. Bw. Stanford Kalala, Mkurugenzi Mtendaji wa CDTF NGO alisema asasi inaendelea kuhamasisha rasilimali kutoka kwa wadau wa maendeleo ili kuwezesha vijana washiriki katika maendeleo ya jamii na kubadili maisha yao yawe bora. Kwa sasa asasi unafadhiliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Jamii.

Taasisi ya Maendeleo ya Jamii CDTF Trust inawatakia wadau wake wote na jamii kwa ujumla kheri ya mwaka 2026 , ukawe ni m...
01/01/2026

Taasisi ya Maendeleo ya Jamii CDTF Trust inawatakia wadau wake wote na jamii kwa ujumla kheri ya mwaka 2026 , ukawe ni mwaka wa maendeleo endelevu ,amani na mafanikio katika jamii zetu.

25/12/2025

CDTF Trust inawatakiwa wadau wote na jamii kwa ujumla kheri ya sikukuu ya chrismass .

Asante kwa kuendelea kuwa nasi kwenye kila jambo la kijamii

CDTF Trust kupitia wadau wake wote, inapenda kuutakia watanzania kheri na baraka za Sikukuu ya Uhuru wa Tanzania. Tunawa...
09/12/2025

CDTF Trust kupitia wadau wake wote, inapenda kuutakia watanzania kheri na baraka za Sikukuu ya Uhuru wa Tanzania.

Tunawatakia maadhimisho mema ya Uhuru huku tukiendelea kuunga mkono jitihada za kujenga taifa lenye maendeleo endelevu.


Cdtf Trust inaungana na watanzania wengine kuwatakia kila la kheri kidato cha nne katika mtihani wa Taifa
17/11/2025

Cdtf Trust inaungana na watanzania wengine kuwatakia kila la kheri kidato cha nne katika mtihani wa Taifa

CDTF Trust kwa kushirikiana na Kampuni ya CDTF Enterprises waliweza kutoa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa wanachama wakikun...
12/11/2025

CDTF Trust kwa kushirikiana na Kampuni ya CDTF Enterprises waliweza kutoa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa wanachama wakikundi cha wamama katika Ofisi za CDTF HOUSE zilizopo maeneo ya Uyoga.

Lengo la mafunzo haya ni kuimarisha ujuzi na kuongeza thamani katika sekta ya ufugaji nyuki kwa jamii na vikundi mbalimbali.


Tunawekeza katika ufanisi na uendelevu .Warsha ya wasimamizi wa miradi ya CDTF imeagiza utekelezaji wa mikakati endelevu...
17/10/2025

Tunawekeza katika ufanisi na uendelevu .
Warsha ya wasimamizi wa miradi ya CDTF imeagiza utekelezaji wa mikakati endelevu wa kifedha (FSP) ili kuboresha huduma kwa jamii

CDTF Trust inaungana nawe kuazimisha Siku ya kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa inakutakia mapumziko mema.
14/10/2025

CDTF Trust inaungana nawe kuazimisha Siku ya kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa
inakutakia mapumziko mema.

Picha ikimuonesha mjumbe wa Bodi ya wadhamini Cdtf Trust  Bw.Abel Busalama, akipata maelekezo ya uendeshaji wa bustani y...
18/09/2025

Picha ikimuonesha mjumbe wa Bodi ya wadhamini Cdtf Trust Bw.Abel Busalama, akipata maelekezo ya uendeshaji wa bustani ya mapapai kutoka kwa mtaalamu wa kilimo hai .

Alipotembelea Shule ya Sekondari Sangara iliyopo Wilaya ya ilala Mkoani Dar es salaam.

Kulia ni Mjumbe wa Bodi wa Cdtf Trust Bw. Abel Busalama na Kushoto ni Mtaalam wa kilimo hai Bw. Mugemuzi.

Address

Posta, NIC Investment House, 2nd Floor
Dar Es Salaam
CODE11101P.O.BOX9421

Telephone

+255222131471

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Community Development Trust Fund posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share