29/11/2025
NGUZO MBILI ZINAZO LINDA HEKALU LA MFALME SULEMAN.
ππΏUlimwengu wa ajabu wa mafumbo wa Freemasonry umejikita zaidi katika ishara na mafumbo, huku tabaka nyingi za maana kuhusu alama hizo zikisubiri kugunduliwa na wanachama wake. Miongoni mwa alama nyingi ambazo zimeteka akili za Freemasons katika historia ni alama ya Nguzo mbili zinazo linda hekalu la Mfalme Suleman ambazo zimebeba nafasi ya kipekee na ya kuvutia katika Freemasonry.
Lakini vipi kuhusu alama hii ya ajabu yenye muundo mkubwa ambayo imeweza kuk**ata mawazo ya waashi tangu karne nyingi zilizo pita? Kwanini alama hiyo maarufu inashikilia nafasi kubwa katika mafundisho na desturi za Freemasons?
Tunaanza safari yetu kufunua siri na mafumbo yanayo izunguka alama hiyo ya nguzo mbili ( nguzo ya boaz na yakini), kwa kuchunguza asili yake ya kihistoria, uhusiano wake wa kimafumbo na mbunifu mkuu Hiram Abiff, pamoja na tafsiri nyingi mbalimbali kuhusiana na umuhimu wa alama hiyo ndani ya Ulimwengu wa kuvutia wa Freemasonry.
Jiandae kuelimika kadri tutakavyo chunguza undani ulio fichwa wa alama hii ya kuvutia ya kimasoniki, na kufichua maarifa ya kina yaliyo ndani yake.
NGUZO YA BOAZI NA YAKINI.
Kiini cha hadithi kuhusu ujenzi wa Hekalu la Mfalme Suleman, nguzo mbili za Boaz na Yakini zina nafasi kubwa na muhimu katika alama za Kimasoniki. Kwa mujibu wa Biblia nguzo hizo kuu mbili zilijengwa kwa shaba na zilisimama wazi mbele ya ukumbi wa Hekalu la Mfalme Suleman huko Yerusalemu. Zikiwa zimejengwa kwa ustadi wa hali ya juu, nguzo hizo hazikuwakilisha tu ubunifu wa ajabu pia zilikuwa zimebeba maana kubwa ya kiroho.
Biblia inahusisha ujenzi wa nguzo hizo na Fundi stadi aitwaye Hiram, ambaye ni mtu muhimu sana katika mafundisho ya kimasoniki. Hiram huyo si mwingine bali ni Hiram Abiff, mbunifu mkuu mwenye kuheshimiwa wa Hekalu la Mfalme Suleman. Msomi mroma wa kiyahudi aitwaye Josephus alieleza kwamba nguzo ya Boaz ilisimama upande wa kushoto kwenye maingilio ya ndani ya Hekalu, na nguzo ya Yakini ilisimama upande wa kulia.
Boaz na Yakin hazikuwa nguzo za kawaida, kwasababu vipimo vyake vilikuwa ni vyenye kustaajabisha kwelikweli. Biblia inaeleza kwamba unene wake nguzo hizo ulikuwa karibia futi sita na urefu wake ulikuwa futi 27. Kwa bahati mbaya nguzo hizo nzuri zenye kuvutia hazikupona ziliharibiwa wakati wa vita iliyo pelekea uharibifu wa Hekalu la kwanza na hakuna kumbukumbu zinazo onesha ya kwamba ziliwahi kubadilishwa au kujengwa upya wakati wa Hekalu la pili lilipo jengwa.
Majina ya nguzo hzo mbili, Boaz na yakini, yana maana kubwa pia. Jina Boazi linatafsiriwa kumaanisha "in him is stregth" yaani ndani yake kuna nguvu, wakati huohuo jina Yakini hutafsiriwa "He will establish" yaani Ataimarisha. Yanapo unganishwa kwa pamoja, majina hayo yanachukuliwa k**a ukumbusho kwamba Mungu angesimamisha Hekalu na ibada ya jina lake kwa nguvu. Kupitia kazi ya Hiram Abiff, nguzo za Boaz na Yakini zilikuja kuashiria nguvu na uthabiti wa ahadi za Mungu na kuonyesha Ufundi wa ajabu wa mtu huyu mkuu (Hiram Abiff) wa Freemasonry.
HIRAM ABIFF NA UJENZI WA HEKALU LA MFALME SULEMAN.
Hadithi ya ujenzi wa Hekalu la Mfalme Suleman inakuwa haijakamilika bila kutajwa kwa mbunifu wake mkuu, Hiram Abiff. Hiram Abiff anatambulishwa katika Biblia k**a mfanyakazi stadi wa shaba aliyeletwa kwa Mfalme Suleman kutoka Tiro. Alikuwa ni mwana wa mjane wa kabila la Naftali, na Baba yake alikuwa mtu wa Tiro (Wafalme wa Kwanza 7:13-15). Hiram Abiff alijaaliwa Hekima, Ufahamu na Ustadi wa kipekee katika kazi za shaba, mambo ambayo yalimfanya kuwa mtu wa thamani katika ujenzi wa Hekalu..
Hadithi ya kutisha kuhusu mauaji ya Hiram Abiff ni sehemu muhimu katika mafundisho ya Freemasonry. Aliuawa kikatili ndani ya Hekalu alilo buni mwenyewe kupitia mikono ya majambazi watatu, ambao walitaka kupewa password za siri za mwalimu mkuu wa masons. Kupitia uaminifu wake usio yumba wa Hiram Abiff na azimio lake la kulinda siri za ufundi huo, ilisababisha kifo chake, lakini matendo yake yaliacha athari na alama ya kudumu kwa Freemason.
UMUHIMU WA MAJINA NGUZO (BOAZI NA YAKINI) NA UWAKILISHI WAKE
Majina ya nguzo hizo mbili Boaz na Yakini, yamebeba maana ya kina na ni muhimu sana katika kuelewa uwakilishi wake kwenye mafundisho ya Kimasoniki., k**a nilivyo eleza hapo awali Jina Boaz lina maanisha "Ndani yake mna nguvu", huku jina Yakin lina maanisha " ataimarisha" . Majina hayo mawili yanapo zingatiwa kwa pamoja yanaashilia wazo la kwamba Mungu angesimamisha Hekalu na ibada ya jina lake kwa nguvu.
Pia inaelezwa ya kwamba, nguzo hizo zinawakilisha nguvu na uthabiti wa ahadi za Mungu, zikitumika k**a ukumbusho kuhusu ufundi wa kipekee ulio fanywa na Hiram Abiff. Nguzo hizo sio tu sehemu ya ushuhuda kuhusu ufundi wa kipekee alio kuwa nao Hiram Abiff, pia nguzo hizo zina maana ya kina ya kiroho na katika alama na ishara ndani ya jumuiya ya Freemasonry.
Freemasons wanachukulia nguzo mbili za Boaz na yakini k**a uwakilishi wa jozi zinazo kinzana ama nguvu mbili kinzani (nuru na giza), mara nyingi katika Freemasonry nguzo hizo zinahusishwa na falsafa za mashariki (Yin na Yang). Inaelezwa ya kwamba dhana hii kuhusu nguzo mbili inawafundisha waashi (Freemasons) kusawazisha nguvu zao kinzani za asili ndani yao wenyewe kupitia kuoanisha mawazo, hisia na matendo yao na mpango mkuu - The Great Work. Nguzo hizo pia zinawakilisha mgawanyiko wa Nuru na Giza au maisha na kifo, inaelezwa ya kwamba kifo wakati mwingine ni muhimu ili kuondoa kitu cha zamani na kuzuia ili kutengeneza njia kwa upya na yenye ustawi.
Tafsiri mbalimbali juu ya alama hii ya nguzo mbili zinaonyesha umuhimu wake katika mambo mbalimbali mengi ndani ya mafundisho ya Freemasonry. Ingawa maana zake halisi hutofautiana baina ya wanachama wa Freemasonry binafsi lakini maana yake kuu ni uwakilishi wa Uwili (asili ya uwili - duality) na nik**a ushuhuda juu ya Fundi stadi katika Freemasons mwenye kuheshimika HIRAM ABIFF na hizo ndio maana mbili ambazo zinabaki kuwa thabiti. Hatimaye, nguzo za Boaz na Yakin zinatumika k**a alama ya kudumu katika Freemasonry, zikisimama k**a ukumbusho juu ya nguvu za maadili na masomo yanayo tokana ma hadithi za Hekalu la Mfalme Suleman na mbunifu wake mkuu, Hiram Abiff.