04/06/2026
Ardhi yenye rutuba na maji safi ni muhimu kwa uzalishaji wa chakula. Miradi inayoharibu mazingira inaweza kusababisha njaa au kupanda kwa gharama za chakula, kwenye maeneo ya vijijini kutokana mpango duni wa mradi kuamisha wanakijiji
Utalii huzalisha ajira nyingi zisizo za kitaalamu pekee mfano Waongoza watalii, madereva, wapishi, wauza vinyago, hoteli na wafanyakazi wa usafiri wote hunufaika kupitia mazingira yaliyohifadhiwa vizuri. Baadhi ya mazingira yanaharibiwa na mradi wa EACOP
Mafuta ni rasilimali inayokwisha, mazingira yanaweza kudumu milele. Mafuta yakisha, mradi huisha. Lakini misitu, maziwa na ardhi vinaweza kuendelea kutoa faida kwa karne nyingi ikiwa vitalindwa.
Uchafuzi wa mafuta utaharibu vyanzo vya maji. Endapo kutatokea uvujaji wa mafuta, mito na visima vinaweza kuathirika, jambo litakalogusa afya ya wananchi, mifugo na kilimo.
Utalii huongeza biashara nyingi hata biashara ndogo ndogo k**a Mama lishe, mafundi, wauza bidhaa za asili na wasanii hunufaika na watalii kwa kiwango kikubwa kuliko miradi ya muda mfupi ya ujenzi.