02/11/2024
WAJENGEE UWEZO WA KUSOMA
📚Huenda wewe ni msomaji ama siyo msomaji wa vitabu. Je, jamii yako wanasoma vitabu?
Wanapenda vitabu gani?
Wanapata wapi vitabu?
Una mchango wowote kwa wao kusoma kitabu?
📚Unaweza kuwawezesha watu wa mahali fulani kwa kusoma vitabu.
Zaidi vitabu vya riwaya fupifupi na Stadi za maisha. K**a kuhusu kilimo, ufugaji, malezi, imani n.k
1. Nunua kitabu peleka shule katika hilo eneo
2. Nunua kitabu peleka serikali ya mtaa/kijiji waambie unataka kisomwe na kiwafikie
3. Nunua kitabu peleka zahanati ya Kijijini
📚Kunaweza kuwa na meza ndogo ya vitabu hata 10 tu ambavyo wanaohitaji huduma watajisomea wanapokua hapo kusubiri huduma. Inapunguza hata ile kero ya foleni.
Pia kuna wagonjwa ambao hawana starehe yoyote zaidi ya kusoma lakini hata hicho kitabu hawana.
📚Unaweza pia kuanzisha klabu ya usomaji kijijini ama mtaani kwako ambapo watu watakutana mahali kusoma vitabu.
📚Vitabu vipo na wasomaji wapo ila namna ya kuwafikia.
📚Mwaka 2022 Tulivifikia vijiji vya mbali sana kutoka Dar, Katesh, Ngudu, kuna kijiji kipo Mtwara, tulipeleka vitabu vilisomwa na tulipata simu nyingi za mrejesho.
Wanunulie hata kitabu kimoja tu, ni sadaka pia.
Madam CEO
Kitabu Initiative
02112024
KITABU KIPYA. Sh. 1500 tu nakala tepe (softcopy)