09/12/2021
بسم الله الرحمن الرحيم
Assalamu 'alaykum warahmatullahi wabarakatuh
Historia ya fupi "FADHWAAILUL AYTAAM GROUP" ni
Kikundi maalumu cha kiislamu kinachojihusisha na kuwasaidia mayatima , walemavu , wasiojiweza na wajane kinachoendeshwa kupitia mitandao ya kijamii kilianzishwa rasmi siku ya jumapili ya tarehe 09/12/2018 kupitia mtandao wa WhatsApp pekee kikiongozwa na viongozi wafuatao:-
1. Maulid Bin Swaleh (Mwenyekiti)
2. Kisandu Bin Kusolwa (Katibu)
3. Mariam Abdulrahman (M/hazina)
4. Abuubakari Saidi (Mratibu wa safari)
Katika kipindi hicho kikundi kilikuwa katika kipindi kigumu sana hususani katika masuala ya kiuchumi pia katika nyoyo za watu ziamini ukweli kuhusu lengo la kikundi hakika kipindi hicho viongozi walijitolea muda wao na bundle(bando) zao ili waweze kuhamasisha jambo la kheri la kuwasaidia yatima, walemavu, wajane na wasiojiweza
Kikundi kilikaa muda mrefu pasipokuwa na safari/ziara ya kikundi kutokana na mapato kuwa chini.
Kikundi kilianza safari/ziara zake katika vituo vya kulea yatima na wahusika wa majumbani wafuatao:-
1. MWANA ORPHANAGE CENTRE kilichopo Vingunguti kwa pelapela.
2. Bibi Fauzia na mjukuu wake Fauzia waliopo Mtongani - Dar es salaam.
3. UMRA ORPHANAGE CENTRE kilichopo Magomeni.
4. UMRA ORPHANAGE CENTRE kilichopo Vikawe - Bagamoyo.
Nimejitahidi kuorodhesha kwa uchache kutokana na waliosaidiwa hususani wa majumbani ni wengi sana sitoweza kuwaorodhesha wote.
Katika kipindi hicho chote cha kuwafikishia walengwa huduma viongozi na wanakikundi wengine walikuwa mstari wa mbele kutumia muda wao na nauli zao pia kuna wakati mwingine kutumia pesa ya kikundi kwenda kuchukua swadaka za walengwa mfano: Nguo n.k
Kipindi chote hicho viongozi walianzisha kikundi kwa lengo la kuwa taasisi rasmi inayotambulika kisheria na mamlaka ya nchi hapo baadae الله atakapotuwezesha.
Tulifanikiwa kuanza mchakato huo wa kuchukua fomu ya maombi ya BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU TANZANIA siku ya jumamosi tarehe 24/04/2020 tulipewa sample ya katiba na hapo baada ya muda tulianza mchakato wa kuifanyia marekebisho sehemu tulizoziona zinahitaji marekebisho alhamdulillah tulimaliza mchakato huo wa katiba siku ya jumapili tarehe 30/08/2020.
Mchakato wa katiba ulivyoisha tuliweza kupata viongozi wengine zaidi wakiwemo wadhamini na wanachama watakaokuwa tayari kujitolea kwa nguvu na mali katika kheri hii.
Tuna kila sababu ya kumshukuru الله kwa kuwapata watu waliokuwa tayari kwa kheri hii na tunamuomba atuongezee wengine zaidi ili tuweze kufikia lengo kuu.
Tunatarajia mwakani inshaallah tuendelee zoezi la kwenda kwa mwanasheria na BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU TANZANIA kwa ajili ya kuendelea na usajili.
Tunapenda kuwashukuru wale wote walioweza kufanikisha kikundi kwa kujitolea muda,pesa,mawazo,maoni,ushauri n.k mpaka kufika sasa الله awalipe malipo manono hapa duniani na kesho akhera.
Tunatumaini tutashikana katika kamba ya الله pasipo kutetereka ingawa katika mambo ya kheri kuna changamoto nyingi sana.
Tunamuomba الله pekee atujaalie tuendelee na mshikamano wetu huu mpaka mwisho wa uhai wetu pia uwe ni urithi kwa vizazi vya sasa na vijavyo katika kheri hii atuepushe na migogoro,vijicho,sihri na vile vyote vitakavyovunja mshikamano wetu na tuwe ni wenye kupendana na pindi mmoja wetu anapokosea tukumbushane kwa nidhamu,heshima na adabu
ALLAHUMMA AAMIIIN THUMMA AAMIIIN
WABILLAHI TAWFIIIQ