23/07/2021
TWENDE CHAKUWAMA KWENYE TAMASHA KUWASAIDIA YATIMA KWENYE CHARITY EVENT.
Shirika la (TSEOT) likishirikiana na Mashirika mengine linapenda kukukaribisha wewe mdau katika tukio muhimu sana la kuwashika mkono Yatima katika eneo la CHAKUWAMA tarehe 30/07/2021, Sinza - Mori Dar es salaam, Tanzania kuanzia saa 9:00Am - 1:00Pm.
Watoto Yatima yaani wahitaji wana umri wa kuanzia miaka 2 hadi 25; Jinsia zote. Hivyo wewe k**a Mtanzania k**a umeguswa na hili unaombwa kufika katika eneo la tukio ili uweze kutoa chochote ulichokuwa nacho kuwasaidia yatima hawa.
Vitu ambavyo unaweza kuchangia au kutoa vikapokelewa ni k**a Nguo za kuvaa zilizo katika hali nzuri, Pedi, Viatu, Sendozi, Vitanda, Vifaa vya shule k**a Madaftari, Kalamu, Rula, Penseli na mabegi ya shule, Vyakula vya aina yoyote ile, Sabuni za kufulia na kuogea, Pesa N.K.
Hivyo wasiliana na uongozi wa shirika la (TSEOT) kusudi uweze kupewa utaratibu wa kushiriki Tamasha hili. Kumbuka watoto hawa hawana Baba, Mama wala Ndugu isipokuwa wanalelewa katika kituo cha CHAKUWAMA.
kARIBU UNGANA NASI, SAIDIA YATIMA, SAIDIA WAHITAJI.
Mawasiliano;
Tel: +2555 783 533 706 (WhatsApp)
+255 627 343 706 (SMS & Calls)
E-Mail: [email protected]
: [email protected]