Shujaa Cancer Foundation

Shujaa Cancer Foundation Shujaa Cancer Foundation aspires to improve the lives of reproductive cancer survivors in transition

Mashujaa wakisikiliza kwa makini mafunzo muhimu toka kwa wataalamu.
12/06/2026

Mashujaa wakisikiliza kwa makini mafunzo muhimu toka kwa wataalamu.

Mashujaa walipata nafasi ya kusikia mada mbali mbali katika mtoko wao:- Ufuatiliaji wa Afya Baada ya Matibabu ya Saratan...
12/06/2026

Mashujaa walipata nafasi ya kusikia mada mbali mbali katika mtoko wao:-

Ufuatiliaji wa Afya Baada ya Matibabu ya Saratani
Dkt. Sarah Nyagabona, Daktari Bingwa wa Saratani kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, alisisitiza umuhimu wa ufuatiliaji wa afya mara kwa mara baada ya kumaliza matibabu ya saratani.
Washiriki walielimishwa kuhusu umuhimu wa kuhudhuria miadi za kliniki k**a ilivyopangwa, kufuata ushauri wa wataalamu wa afya, na kutambua mapema dalili zinazoweza kuashiria kurejea kwa ugonjwa. Pia walihamasishwa kuzingatia mtindo bora wa maisha ili kuimarisha afya, ustawi na ubora wa maisha baada ya matibabu.

Msaada wa Kisaikolojia na Kijamii katika Usimamizi wa Saratani
Safari ya saratani haiathiri mwili pekee, bali pia hisia, mahusiano na ustawi wa kiroho.
Kupitia mjadala huu, washiriki walipata nafasi ya kujibiwa maswali kuhusu changamoto za kihisia, kisaikolojia, kijamii na kiroho zinazoweza kujitokeza wakati na baada ya matibabu ya saratani.
Wataalamu walisisitiza umuhimu wa ushauri nasaha, msaada wa familia, vikundi vya usaidizi vya mashujaa wa saratani (Cancer Support Groups), pamoja na huduma za afya ya akili katika kuwasaidia wagonjwa na mashujaa kuendelea kuishi kwa matumaini, nguvu na ustawi.

Saratani na Lishe
Bi. Rebeca Lebi alitoa elimu na mwongozo wa vitendo kuhusu umuhimu wa lishe bora katika safari ya saratani na maisha baada ya matibabu.
Washiriki walijifunza namna ya kuchagua vyakula vyenye virutubisho muhimu, kudumisha lishe yenye uwiano sahihi, na kukabiliana na changamoto za lishe zinazoweza kujitokeza kutokana na matibabu ya saratani.
Lishe bora ni sehemu muhimu ya kuimarisha afya, kuongeza nguvu za mwili na kuboresha ustawi wa mashujaa wa saratani.

Afya bora huanza na uchaguzi bora wa chakula kila siku.

Tulianza maadhimisho ya Siku ya Mashujaa wa Saratani Duniani kwa kupata kufungua kinywa ( breakfast)
09/06/2026

Tulianza maadhimisho ya Siku ya Mashujaa wa Saratani Duniani kwa kupata kufungua kinywa ( breakfast)





08/06/2026
Tukiwa tunasubiria mabasi kufika
08/06/2026

Tukiwa tunasubiria mabasi kufika

Maadhimisho ya Sikukuu ya Mashujaa wa Saratani Duniani yaliyofanyika Kijiji Beach Resort ikiwa mtoko maalum wa Mashujaa ...
08/06/2026

Maadhimisho ya Sikukuu ya Mashujaa wa Saratani Duniani yaliyofanyika Kijiji Beach Resort ikiwa mtoko maalum wa Mashujaa kusherehekea maisha.





Njiani kuelekea Kijiji Beach Resort
07/06/2026

Njiani kuelekea Kijiji Beach Resort





Imebaki siku 1 tu ! Kwa pamoja,  tunasheherekea maisha 💪🏽
06/06/2026

Imebaki siku 1 tu !

Kwa pamoja, tunasheherekea maisha 💪🏽





Zimebaki siku 2 .....Karibu Tusheherekee Maisha Pamoja Kijiji Beach Resort Kigamboni
05/06/2026

Zimebaki siku 2 .....Karibu Tusheherekee Maisha Pamoja Kijiji Beach Resort Kigamboni





Zimebaki siku 4 tu ........Pamoja Tunasheherekea Maisha na Kunarudisha Tabasamu !
04/06/2026

Zimebaki siku 4 tu ........Pamoja Tunasheherekea Maisha na Kunarudisha Tabasamu !





Address

Mwai Kibaki Road
Dar Es Salaam
14111

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 10:00 - 15:00

Telephone

+255768116346

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Shujaa Cancer Foundation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Shujaa Cancer Foundation:

Share