07/11/2025
SALAMU ZA POLE!
Daraja La Ajira Tanzania tunaungana na maelfu ya wananchi kuwapa pole vijana wote waliopoteza Uhai katika maandamano ya Oktoba 29.
Familia na jamii kwa ujumla zina huzuni juu ya Roho za marehemu ivyo tunaomba kwa Mwenye enzi Mungu awapatie amani na nguvu ya kusonga mbele.
Pia, vijana ni Nguvu kazi ya taifa na kiasharia kikubwa cha ukuaji wa uchumi na wahusika wakuu wa maswala ya Ajira katika taifa.
Tunaomba serikali sikivu iweze kuketi na makundi tofauti ya vijana na kusikiliza kero, maoni na mtazamo ili kujenga taifa moja lenye amani, upendo na mshikamano.
Mungu Ibariki Tanzania
Mh. Peter John
Raisi
Jumuiya ya DAT