Ruge Mutahaba Foundation

Ruge Mutahaba Foundation |Creativity|Innovation|Excellence|Perseverance|Empathy|

GenZERO Sicklecell 2050 GenZero Sickle Cell 2025 Tanzania ya Ruge Mutahaba Foundation π—₯π—¨π—šπ—˜ 𝗠𝗨𝗧𝗔𝗛𝗔𝗕𝗔 π—™π—’π—¨π—‘π——π—”π—§π—œπ—’π—‘ imesaini ...
18/08/2026

GenZERO Sicklecell 2050 GenZero Sickle Cell 2025 Tanzania ya Ruge Mutahaba Foundation π—₯π—¨π—šπ—˜ 𝗠𝗨𝗧𝗔𝗛𝗔𝗕𝗔 π—™π—’π—¨π—‘π——π—”π—§π—œπ—’π—‘ imesaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) na KAI, Kesho Angavu Initiative Kesho Angavu Initiative , kwa ajili ya kutoa elimu ya Siko Seli ikiambatana na upimaji wa hiari wa vinasaba, mapema kabla ya maamuzi ya ndoa na uzazi.

Hesabu ni simpo. Wazazi wawili wenye kinasaba cha Siko Seli, kila mimba ina uwezekano wa asilimia 25 wa mtoto kuzaliwa na ugonjwa wa Siko Seli. Lengo la MoU hii ni kuhakikisha hesabu hiyo inajulikana kabla haijatokea. Ndiyo maana Siko Seli inazuilika, kwa sababu inatabirika.

Kabla ya kurasimisha ushirikiano huu, GenZERO na KAI tumeshafanya kazi pamoja katika matukio 3, ambapo vijana 286 walipima vinasaba vyao baada ya kupata elimu sahihi. Mkataba huu haukuanza kwenye karatasi, bali kwenye utekelezaji ambao umezaa dhamira ya kuwafikia vijana 3,000 kwa mwaka 2026/27.
Sasa KAI rasmi ni GenZERO Komando πŸ’ͺ🏾

GenZERO Komando si cheo cha heshima peke yake. Ni jina la yeyote anayechukua hatua tatu: kujifunza, kupima, na kisha kuiongoza jamii yake kufanya vivyo hivyo. Ni watu na taasisi wanaobeba ujumbe huu kwenye jamii zai wenyewe. KAI wamefanya hivyo, na sasa wanaelekea kufikia lengo muhimu la vijana 1,000 wa kwanza, itakayowapatia tuzo ya heshima.

Taasisi yako inataka kuwa GenZERO Komando? Tuandikie kupitia genzerosicklecell2050.tz

Kwa ushirikiano, elimu na hatua madhubuti, tunaweza kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa na Siko Seli ifikapo 2050.
GenZero Sickle Cell 2025 Tanzania

 


Shine Sokoni ya Ruge Foundation Yashinda TEHAMA AWARDS 2026Ruge Mutahaba Foundation kupitia mradi wa Shine Sokoni Shine ...
10/08/2026

Shine Sokoni ya Ruge Foundation Yashinda TEHAMA AWARDS 2026

Ruge Mutahaba Foundation kupitia mradi wa Shine Sokoni Shine Sokoni imeshinda nafasi ya kwanza kwenye kategoria ya β€œICT Skills Development Initiative” katika Tuzo za TEHAMA 2026 zilizoandaliwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Kamisheni ya TEHAMA. Ikiongozwa na utafiti uliofanyika kwa wanafunzi zaidi ya 500 kutoka vyuo mbalimbali nchini, Shine Sokoni inawasaidia wanafunzi kuzielewa taaluma zao na kubobea kwenye maeneo mahususi (specialization), kuwakutanisha na washauri wa kitaalamu (mentors), na kuwaunganisha na taasisi mbalimbali wakiwa bado wanasoma, lengo kuu likiwa kuwaandaa kujiajiri na kuajirika.

Hadi sasa, Shine Sokoni imewafikia zaidi ya wanafunzi 750; wanafunzi 250 wakiwa wamekamilisha mafunzo ya uwekezaji kwenye soko la hisa, 30 wakikutanishwa na mabalozi wastaafu na wa sasa kujifunza diplomasia, na 30 wanaosoma masomo ya udaktari wakijifunza ubunifu wa mawasiliano kupitia programu ya β€˜Medical Communication’ ili kuleta mchango katika kuboresha afya ya jamii (public health) hasa kwa magonjwa yatokanayo na mtindo wa maisha.

Maono ya Ruge Mutahaba Foundation kupitia Shine Sokoni ni kuimarisha nguvu kazi ya vijana na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050.

Pamoja na ushindi huu, Ruge Mutahaba Foundation ilikuwa inawania tuzo nyingine kupitia programu yake ya GenZero Sickle Cell 2050 GenZero Sickle Cell 2025 Tanzania

Tuzo hizi za TEHAMA 2026 zilizofanyika Tar 9 Agosti 2026, Johari Rotana zinaonyesha nia ya Wizara na Serikali kuchochea na kusaidia matumizi ya teknolojia katika kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii zetu.





10/08/2026

Project yetu ya pili iliyopata nomination ya TEHAMA Awards ni Shine Sokoni Shine Sokoni , platform ya kidijitali inayowawezesha wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati kujifunza ujuzi wa vitendo, kupata mentorship kutoka kwa wataalamu wa sekta mbalimbali, na kuunganishwa na fursa za kushirikiana na taasisi mbali mbali kuwajengea uwezo, vyote hivi wakiwa bado wako vyuoni.

Shine Sokoni inaamini kwamba kizazi cha sasa cha wanafunzi wa Tanzania kina uwezo mkubwa. Kinachohitajika ni mfumo unaowasaidia kubadilisha ndoto zao kuwa hatua za kweli, wakiwa bado masomoni.





09/08/2026

Huu ni mradi wetu wa kwanza ulioteuliwa kuingia katika Tuzo za TEHAMA; GenZERO Sickle 2050 GenZero Sickle Cell 2025 Tanzania

Tunatumia teknolojia na mifumo ya kidigitali kubadili jinsi tunavyokabiliana na Siko Seli: kufikisha elimu na upimaji wa vinasaba kwa vijana ambao bado hawajafanya maamuzi ya ndoa na uzazi.

Msingi wa yote ni : Siko Seli inazuilika, kwa sababu inatabirika.

Asante kwa kila aliyeamini, kila aliyepima, na kila anayeiongoza jamii yake.




Ruge Mutahaba Foundation leo inashiriki TEHAMA Awards TEHAMAwards ikiwa na miradi miwili, GenZERO Sickle Cell GenZero Si...
09/08/2026

Ruge Mutahaba Foundation leo inashiriki TEHAMA Awards TEHAMAwards ikiwa na miradi miwili, GenZERO Sickle Cell GenZero Sickle Cell 2025 Tanzania na Shine Sokoni Shine Sokoni, iliyoingia top 3 ya subcategories mbili: Social Impact na Made in Tanzania.

Ni heshima kuona miradi yetu ikitambuliwa, na Serikali ikionesha dhamira ya kuunga mkono ubunifu na kuchochea matumizi ya teknolojia kwa ajili ya kugusa jamii na maendeleo ya Tanzania.





23/06/2026

Washiriki wa Your Art Your Power workshop wamekuwa na siku mbili muhimu kwa ubunifu wao ambapo wamekumbushwa na kufundishwa kuwa

1. Kwenye uchumi unaoendeshwa na mawazo , ubunifu na ugunduzi; thamani ya bunifu inalindwa kwa kusajili Miliki Bunifu au Intellectual Property (Hakimiliki / Copyright, Hataza / Patents, Trademarks, Servicemarks, Industrial Design, nk.)

2. Unapolinda ubunifu wako, unalinda uwekezaji wako na wa wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye biashara yako (IP is part of your business Asset)

3. Unapolinda Miliki Bunifu yako inakutengenezea vyanzo vya mapato ikiwepo Mirabaha / Royalties, Licensing, nk.

4. Unapolinda Miliki Bunifu yako hata kazi yako unapoiuza au kulipwa kutokana na kazi yako, haki yako ya kutambuliwa (Moral Right) inabaki…. Mfano Kumtaja mwandishi wa Nyimbo, au Camera man kwenye Filamu Credits

5. Miliki bunifu zilizolindwa kwa Usajili wa BRELA au COSOTA haziwezi kuporwa na wajanja wajanja; ikitokea sheria inaweza kukupatia haki yako.

Washiriki takribani 50 walishiriki midahalo, mafunzo na kushare uzoefu wao. Walijifunza kutoka BASATA, COSOTA, BRELA jinsi ya kurasimisha kazi zao.

Tutaendelea kushare Tips zaidi za Kulinda Miliki Bunifu yako; baki nasi hapa hapa.

Imeandaliwa na Jakaya M. Kikwete Foundation, NexLaw Advocates na π—₯π—¨π—šπ—˜ 𝗠𝗨𝗧𝗔𝗛𝗔𝗕𝗔 π—™π—’π—¨π—‘π——π—”π—§π—œπ—’π—‘

Unataka kuipeleka Sanaa na Ubunifu wako Next Level?Karibu uombe kushiriki mafunzo ya β€œYOUR ART, YOUR POWER” yatakayofany...
12/06/2026

Unataka kuipeleka Sanaa na Ubunifu wako Next Level?

Karibu uombe kushiriki mafunzo ya β€œYOUR ART, YOUR POWER” yatakayofanyika Tar 18 & 19 June 2026, Hotel Splipway, Dar Es Salaam

Mafunzo haya yanalenga kukusaidia wewe msanii kuelewa ulinzi wa miliki bunifu (Intellectual Property) hasa Hakimiliki za kazi zako, kuitofautisha brand yako, matumizi ya teknolojia za kisasa ikiwemo AI kuboresha uzalishaji wa sanaa yako na kuimarisha mfumo wa biashara na masoko.

Tunatafuta washiriki walioko Dar Es Salaam, ambao tayari wanajihusisha na shughuli za ubunifu/sanaa kwenye maeneo ya Visual Arts and Crafts (Uchoraji, Uchongaji, Ubunifu wa Bidhaa, Kazi za Mikono n.k.), Performing Arts and Music (Muziki, Uigizaji, Ngoma, Theatre, Ushairi n.k.) na Media and Digital Content Creation (Filamu, Photography, Videography, Podcast, Content Creation n.k.)

Scan QR Code au Click link kwemye bio yetu kuomba. Muda wa kujaza fomu: Dakika 5–10. Nafasi ni 50 tu, Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tar 16 Juni 2026. Changamkia fursa!!!

Imeandaliwa na Jakaya M. Kikwete Foundation NexLaw Advocates π—₯π—¨π—šπ—˜ 𝗠𝗨𝗧𝗔𝗛𝗔𝗕𝗔 π—™π—’π—¨π—‘π——π—”π—§π—œπ—’π—‘

Wakati dunia ikisherehekea   siku ya wafanyakazi; familia na marafiki wa   walikuwa na sababu moja ya zaida kukutana kwa...
01/05/2026

Wakati dunia ikisherehekea siku ya wafanyakazi; familia na marafiki wa walikuwa na sababu moja ya zaida kukutana kwa ajili ya ibada ya kushukuru zawadi ya maisha ya Ruge, kazi aliyoifanya na matunda ya kazi yake.

Ibada ya shukrani ya Birthday ya ilifanyika katika kanisa la KKKT Kijitonyama.

β€œPambana kuwa jua ukifeli utakuwa kipande cha nyota kilichoshindikana” Ruge Mutahaba


Applications za   zinaendelea kupokelewa. Application na Course hii ni BURE, unatakiwa tu kuwa mwanafunzi wa elimu ya ju...
24/02/2026

Applications za zinaendelea kupokelewa. Application na Course hii ni BURE, unatakiwa tu kuwa mwanafunzi wa elimu ya juu unaesoma ndaki za Afya uliyepo mwaka wa pili na kuendelea na mwenye passion ya β€˜Public Health storytelling’ kwenye focus areas zilizotajwa.

Kwa maelezo zaidi tembelea https://shinesokoni.tz/application/medical_communication_program au bonye za link kwenye bio yetu.


Address

#1436 Block C Mikocheni B
Dar Es Salaam
34202

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ruge Mutahaba Foundation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ruge Mutahaba Foundation:

Shortcuts

Share