23/04/2026
Anaandika Jemedari Said 👇👇
HAKI ITENDEKE HATAKAMA MBINGU ZITAANGUKA.
Soka si mchezo tu, ni heshima.
Mwaka 1984, Young Africans SC ilipokutana na Gor Mahia kwenye mashindano ya CAF, kulitokea tukio lililotikisa misingi ya haki kwenye mchezo.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Issa Makongoro, alihusishwa na jaribio la kuwahonga marefa kutoka Ethiopia ili kupindisha matokeo ya mchezo.
CAF wakatoa ujumbe mzito bila kificho—kufungiwa maisha.
Kumekuwa na shutuma nyingi kwenye kupanga/kujaribu kupanga matokeo kwa njia mbali mbali, ajabu Mamlaka mpaka sasa hazijachukua au hata kujaribu kuchukua hatua yoyote. Shutuma zimetoka kwenye vyanzo mbalimbali vya uhakika, wachezaji, vilabu, wadau, etc etc.
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora aliwahi kupatikana na hatia kujaribu kupanga matokeo na wachezaji wa Fountain Gate na ushahidi ukapatikana, akafungiwa maisha “KIMAIGIZO MAIGIZO” baadae akaachiwa na akagombea tena uongozi wa Mkoa akafeli kwenye boksi. Lakini mshirika wake yuko jela ya soka mpaka sasa.
Swali linabaki:Je, ushindi wa namna hii una thamani gani?
⚽ Unaweza kushinda mechi, lakini ukapoteza heshima⚽ Unaweza kufurahia leo,lakini historia ikakuhukumu milele.
⚽ Soka bila haki si ushindi… ni doa
Historia inakumbusha: Mchezo safi hauhitaji njia chafu.
Haki itendeke hatak**a Mbingu zitaanguka (Fiat Justitia Ruat Caelum)
Natoa rai kwamba Wilson Oruma asihukumiwe, asikilizwe kwanza huenda akawa chanzo cha kuondokana na tatizo akageuka shujaa.
NB: Hii vita bado mbichi yaani 😂😂🙌
Follow ukurasa wetu Mnyasa Media