02/02/2026
MH. GODIAN WENSESLAUS MWANA WA MAKOYE HISTORIA YA KATA YA VIDUNDA ITAKUANDIKA KWA WINO WA DHAHABU.
Na:Mc Bahati Cyprian
Tabata, Dar es salaam
0713647034
Kazi ya Maendeleo iliyokwishafanyika hapo Vidunda chini ya Uongozi wako Mheshimiwa Diwani Godian Wenseslaus Mwana wa Makoye ni Kubwa sana...Miaka Mitano iliyopita wengi tulikuwa tunaiota Vidunda Mpya..Binafsi sikujua k**a Vidunda Mpya tutaipata kwa Kasi na haraka kiasi hiki.
Tulitamani kuikomboa Vidunda..Na Sasa chini ya Uongozi wako ni hakika Tumeipata Vidunda Mpya.
Binafsi ninakupatia tuzo ya heshima kwa Uongozi Uliotukuka na k**a Mdau Mahiri na mashuhuri kwa ukombozi wa Vidunda.(Siku Moja nitakukabidhi tuzo hii inshallah)
Miaka 10 ya Uongozi wako na hasa muhula wa Miaka 5 iliyopita umeweza kusimamia mambo makubwa ya Miundombinu ya Barabara, Umeme na Mawasiliano.Nathubutu kusema wewe na Mheshimiwa mbunge Denis Londo mwana mwema wa Vidunda ndio Musa na Haruni waliowaongoza Wana wa Vidunda kwenda nchi ya Ahadi tuliyofika Sasa.
Mheshimiwa Diwani Godian mwana Wa Makoye historia ya Vidunda itakuandika wewe na ndugu Yetu Denis Londo kwa wino wa dhahabu.
Vidunda haina cha kuwadai..Yake mliyoahidi ambayo yalikua ni ndoto za Wana wa Vidunda kwa muda mrefu tangu kuumbwa kwa ulimwengu mmetekeleza.Mungu atawalipa kwa Mchango wenu katika Mustakabali mzima wa kufanikisha agenda ya Vidunda Mpya.
Hata hivyo yamebaki mambo machache ambayo pengine Si ya kimiundombinu Bali ni ya Maendeleo na Ustawi wa watu.
Mimi binafsi ninaona hapo ndipo tunapoelekea ni rai yangu kwamba Sasa Nguvu kubwa ihamie huko.
Mifumo ya kiuongozi ikawe sawasawa..Rasilimali watu na Fedha zisimamiwe ipasavyo Ili kuleta Maendeleo endelevu Vidunda.
Naleta kwako ombi maalumu la kuhakikisha Vidunda inapata Afisa Elimu wa Kata badala ya nafasi hiyo kukaimiwa.
Aidha Maafisa wengine wote wanaohitajika basi waweze kupatikana k**a inavyopaswa.
Ujenzi wa Hostel au Mabweni imekua ni ndoto yetu kwa Miaka mingi ninadhani Sasa baada ya kukamilika kwa miradi ya ukombozi basi tuhamie kwenye mabweni
Mwisho lakini si kwa umuhimu ninakupongeza tena kwa jitihada zako binafsi katika sekta ya Elimu..Nilikuepo Vidunda likizo ya Desemba na niliona mchango wako kwa wazazi wa vifaa vya shule kupitia hati ya punguzo au ruzuku ya mh Diwani.Nikitaja kwa uchache kati ya mengi ambayo umefanya na unaendelea kufanya.
Jicho lako naomba liangazie hapo sekondari kwa ukaribu zaidi ndipo tunapoandaa kizazi kijacho Cha Vidunda.Tunataka tujisikie fahari kuwaacha watoto wetu wasome Vidunda sekondari badala ya kufikiria kuwapeleka sekondari za binafsi au zilizo mbali.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Vidunda.