Masafa Early Childhood Foundation

Masafa Early Childhood Foundation We are a child centered not for profit organization that advocates for a holistic Early Childhood Development in Tanzania. MASAFA means DISTANCE in Swahili.

We aspire to see children reach far distances. We are located in Madale, Dar es Salaam- Tanzania "Together for a better world, where children can find unlimited possibilities in realizing their desired future"

Masafa is a Swahili word meaning “distance”. We are committed to providing the best early childhood awareness to communities in both disadvantaged rural and peri urban setting. We love to s

ee all children enjoy best moments in their childhood as an important bridge to make them reach far distances as future adults. The founders of Masafa have traveled far distances geographically and intellectually because of various opportunities they were privileged with. We would love children achieve the best. Our office environment is a good example in promoting the independence of each child by unleashing his/her inner tendency to learn, through a supportive learning environment.

Mei 11, 2026 – Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Masafa Early Childhood Foundation umefanya kikao cha tathmini y...
11/05/2026

Mei 11, 2026 – Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Masafa Early Childhood Foundation umefanya kikao cha tathmini ya utekelezaji wa PJT-MMMAM kwa robo ya kwanza (Januari–Machi) katika Halmashauri ya Ubungo.

Kikao hiki kimewakutanisha maafisa kutoka idara mbalimbali zikiwemo Ustawi wa Jamii, Afya, Lishe, Elimu, Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto, Maendeleo na Mwandishi wa Habari Kinara.

Katika majadiliano hayo, washiriki walipitia maazimio na mikakati iliyowekwa katika kikao kilichopita, pamoja na kutathmini utekelezaji wake. Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya idara, kushirikisha wadau kikamilifu, na kuendelea kutoa elimu jumuishi kwa jamii ili kuboresha ustawi wa mtoto na familia kwa ujumla.

Tarehe 5 Mei 2026, Mkoa wa Dar es salaam kwa kushirikiana na Masafa Early Childhood Foundation tumefanya kikao cha mapit...
06/05/2026

Tarehe 5 Mei 2026, Mkoa wa Dar es salaam kwa kushirikiana na Masafa Early Childhood Foundation tumefanya kikao cha mapitio ya utekelezaji wa PJT-MMMAM robo ya January mpaka March Katika Halmashauri ya Jiji na Halmashauri ya Kigamboni.

Kikao kimehudhuriwa na maafisa kutoka idara ya ustawi wa Jamii, Afya, Lishe, Elimu na Maendeleo.

Tumepitia Maazimio na mikakati tuliyopanga kikao kilichopita na utekelezaji wake ikiwemo ufanyaji kazi kwa kushirikiana idara zote, Kushirikisha wadau na kuendelea kutoa Elimu kwa Pamoja kwa Jamii.

30/04/2026

Tunaendelea kuhimiza umuhimu wa malezi yenye mwitikio kutoka kwa Wazazi/walezi kwenda kwa watoto. Malezi ni jukumu la mzazi na jamii kwa ujumla hivyo tushurikiane kwa pamoja kuhakikisha mtoto wa miaka 0-8 anafikia utimilifu wake.

30/04/2026

Tunaendelea na utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (PJT-MMMAM) .Leo tumeshiriki kipindi cha Hello Tanzania kupitia uhuru fm .Tumeendelea kuhimiza umuhimu wa wazazi kushiriki katika malezi ya watoto, Kuangalia na kuboresha mazingira ili watoto wapate uchangamshi katika mazingira salama. Hasa watoto wa miaka 0-8. Pia kuhakikisha watoto wanapata vifaa vya uchangamshi ambavyo vinaweza kutengenezwa nyumbani.

27/04/2026

Tunaendelea kufanya uchechemuzi kuhusiana na Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM), shirika la Masafa Early Childhood Foundation kwa kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine, tulipata fursa ya kuelimisha jamii kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya mama mjamzito na mtoto, kwa kuangazia madhara yake pamoja na njia bora za kutokomeza vitendo hivyo, Kupitia Uhuru FM.

Tarehe 22 April, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa kushirikiana na Masafa Early Childhood Foundation tuliandaa ...
24/04/2026

Tarehe 22 April, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa kushirikiana na Masafa Early Childhood Foundation tuliandaa kikao cha Wadau wa masuala ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya mtoto kilichofanyika Katika Ukumbi wa Mkoa wa Dar es salaam.

Tumejadili jitihada zinazofanywa na Serikali na Wadau Katika kufanikisha Utekelezaji wa PJT-MMMAM na kutoa mapendekezo na Mikakati. Kwa Pamoja tumekubaliana kufanya kazi kwa kushirikiana Katika maeneo ya Lishe, Afya, ujifunzaji wa awali, Ulinzi na usalama na Malezi yenye mwitikio. Kuhakikisha mtoto wa 0-8 anafikia ukuaji timilifu.

Kikao hiki kilifunguliwa na Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam, akiambatana na Kaimu Mganga Mkuu. Pia tulipata wageni kutoka Ofisi ya waziri Mkuu-Tamisemi, Mtandao wa kitaifa wa Malezi na Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto(TECDEN).

Tunawashukuru wadau wote kwa kushiriki na kipekee Tunawashukuru waliofanikisha maandalizi ya kikao hiki Children in CrossfireD-tree Macho Kwa Jamii na Christian Religious Services (CRS).

23/04/2026

Tarehe 22 April, Tumeshirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuandaa Kikao cha Wadau wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto.

Tumeendelea kuhimiza ushirikiano baina ya serikali na wadau katika kutekeleza Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ili kuhakikisha afua zote tano muhimu zinaenda sambamba ikiwemo Lishe, Afya, Ulinzi na usalama, Malezi yenye mwitikio na ujifunzaji wa awali zinafikiwa na mtoto wa umri 0-8 anafikia ukuaji timilifu.

Tarehe 20-23 Aprili 2026, Masafa kupitia mradi wa Mtoto kwanza ambayo unachangiza utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Ta...
23/04/2026

Tarehe 20-23 Aprili 2026, Masafa kupitia mradi wa Mtoto kwanza ambayo unachangiza utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi Makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto tumeshiriki katika ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa PJT-MMMAM Mkoa wa Dar es salaam ambayo imeongozwa na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI (Idara ya Afya, ustawi wa Jamii na Lishe pamoja na Idara ya Elimu awali na msingi), Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na wenye ulemavu, (TECDEN na Children in Crossfire.

Katika utekelezaji wake, timu ya kitaifa imefanya usimamizi shirikishi kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa programu katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri. Kwa kufanya vikao na uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam.

Pia kufanya Ufuatiliaji katika Halmashauri ya manispaa ya Temeke na Halmashauri ya manispaa ya Kigamboni .

kufanya ufuatiliaji katika vituo vya kulelea watoto wadogo mchana cha 4real daycare cha manispaa ya Temeke na Kituo cha Little Doves kilichopo Manispaa ya Kigamboni kwa lengo la kuona ni jinsi gani Programu hii inatekelezwa vituoni hasa kwa walengwa wakuu ambao ni Watoto.

Tumebaini ili kufikia ukuaji timilifu wa mtoto wa miaka 0–8 unategemea ushirikiano wa sekta mbalimbali. Ni lazima serikali, wadau wa maendeleo, na sekta binafsi tushikane mikono ili kumpa mtoto wa Kitanzania msingi imara. Hii ni pamoja na kuendelea kutenga na kuongeza bajeti kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 8.

​"Kuwekeza kwa mtoto leo, ni kujenga Taifa imara la kesho."

Katika kuhakikisha kila mtoto wa Dar es Salaam anafikia ukuaji wake timilifu; Siku ya leo tumekaa kikao cha maandalizi y...
15/04/2026

Katika kuhakikisha kila mtoto wa Dar es Salaam anafikia ukuaji wake timilifu; Siku ya leo tumekaa kikao cha maandalizi ya kikao cha Wadau Mkoa wa Dar es salaam (ECD stakeholders meeting) .

kikao hiki kinatarajiwa kufanya tafakari ya Mkoa kuhusu utekelezwaji wa Programu Jumuishi yaTaifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto.

Pichani ni Mkurugenzi wa Masafa Early Childhood Foundation pamoja na Afisa Ustawi wa mkoa wa Dar es Salaam.


Happy Easter to you All. Lets ensure Children 0-8 years are well protected, fed, parented during this Holiday season.
05/04/2026

Happy Easter to you All. Lets ensure Children 0-8 years are well protected, fed, parented during this Holiday season.

Address

Nyakasangwe Street, Close To Madale Police Station/Off Bagamoyo Road/Madale Dar Es Salaam
Dar Es Salaam
P.O.BOX68224

Opening Hours

Monday 07:30 - 16:30
Tuesday 07:30 - 16:30
Wednesday 07:30 - 16:30
Thursday 07:30 - 16:30
Friday 07:30 - 16:30

Telephone

+255738452120

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Masafa Early Childhood Foundation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Masafa Early Childhood Foundation:

Share