Refined

Refined 'A woman of charity, faith and wisdom'

VISSION
Build and establish others on the truth of the Word

09/04/2026

Yeremia 23:23
Mimi ni Mungu aliye karibu, asema BWANA, Mimi si Mungu aliye mbali.
Muite leo naye atakuitikia.

28/02/2026

Hakika wema nazo fadhili, zinatufuata nasi tutakaa nyumbani mwa BWANA siku zote za maisha yetu.

21/01/2026

1Petro1:18-19
Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, k**a ya mwana kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, damu ya Kristo.

Nimekombolewa kwa damu ya Kristo, Ninatamka kuwa huru, ninatamka kusitawi, ninatamka kushinda.

26/12/2025

Tumshukuru Mungu aliyetukumbuka siku zote na kutupa neema ya kuwa salama na afya njema. Kwamsaada wa Mungu tunaelekea kuwaombea na kuwafikia watoto wenye ulemavu. Ikiwa Mungu atakugusa kuungana nasi karibu. Mwenyezi Mungu azibariki familia zote zilizosimama nasi katika hili.

Refined Woman Ministry ( Women of wisdom, faith and charity) -Thanks giving day.

25/12/2025

Yohana 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe pekee ili kila mtu amaaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.
Merry Christmas to you and your family.
Pastor Prisca- The Holy Spirit Arena
(Refined Woman Ministry)

20/11/2025

Upo ujumbe wa Mungu kwa kila mazingira yanayotokea katika safari ya maisha. Naye Mungu bado ni mwema kwa nyakati zote. "A shift is never easy."

Mungu ni Pendo.

08/11/2025

Waweza sema Neno la uzima na libadilishe yote. Kwamaana Wewe ni Mungu na kila kijazacho nchi kilicho hai na kisicho hai ni mali yako. Bwana Tunaomba utusamehe na utupatie mwanzo mpya uliojawa na utukufu wako. Ee Mwenyezi Mungu wa Rehema utuponye na kutuondolea uchungu, uturehemu na utusaidie. Utusamehe kanisa lako tuliposimama kwa ulegevu , Tunanyemyekea kwako Mwenyezi Mungu, utukumbuke. 🇹🇿

06/11/2025

Zaburi 37: 12-15
Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki, Na kumsagia meno yake. BWANA atamcheka, Maana ameona kwamba siku yake inakuja. Upanga wao utaingia mioyoni mwao wenyewe, na nyuta zao zitavunjika.

Mwenyezi Mungu usiikawie kuponya majeraha ya wenye haki wako.

04/11/2025

ZABURI 46:10-11
ACHENI, MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU, NITATUKUZWA KATIKA MATAIFA, NITATUKUZWA KATIKA NCHI.( MAWAZO YANGU SI K**A MAWAZO YA MWANADAMU NA NJIA ZANGU SI K**A ZA MWANADAMU, KWAKUWA BADO KITAMBO KIDOGO SANA, NITAKUJA WALA SITAKAWIA.)

26/10/2025

I am the result of the Cross. "Take all the credits JESUS"🙌
The weight of destiny, the fire and the refining process, obviously our language can differ.(Isaya60:1)

25/10/2025

Apandacho mtu ndicho atakachovuna. Apandaye wema atavuna wema na apandaye uovu atavuna uovu. Majira ya mavuno yanaweza kuchelewa lakini hakika yatafika. Kwa kila utendacho leo ni muhimu kukumbuka matokeo yataleta nini si kwako tu bali na kwa wengine. Maumivu na machozi ya mwingine huachilia laana si kwako tu bali vizazi na hata vizazi. Mwenyezi Mungu aturehemu na kutupatia neema ya kuwa milango ya baraka ya vizazi vyetu.

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255784657279

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Refined posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Refined:

Share