14/08/2026
Katika kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani, MyLEGACY ilipata fursa ya kushiriki katika maadhimisho yaliyoandaliwa na Sauti ya Jamii Kipunguni, mmoja wa washirika wetu muhimu katika ngazi ya jamii.
Ushirikiano wetu na Sauti ya Jamii Kipunguni unalenga kuimarisha juhudi za pamoja katika masuala ya mazingira, uwezeshaji na haki za vijana, pamoja na kuibua fursa zinazowapa vijana nafasi ya kushiriki na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Tunathamini mwaliko na ushirikiano huu unaoendelea, na tunaamini kuwa kupitia nguvu ya pamoja tunaweza kuendelea kujenga jamii yenye vijana wenye uelewa, sauti na nafasi katika maendeleo endelevu.