13/06/2026
Tarehe 12 Juni 2026, SCCULT (1992) LTD ilishiriki katika Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Kagera lililowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya ushirika kutoka ndani na nje ya Mkoa.
SCCULT (1992) LTD iliwakilishwa na Bw. Emmanuel Nestory, Afisa TEHAMA, Mtaalamu na Msaidizi wa Mifumo, ambapo alipata fursa ya kuwasilisha kuhusu Mfumo wa Kidijitali wa SOMA na mchango wake katika kuimarisha utendaji wa Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa.
Mgeni rasmi wa jukwaa hilo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Kanali Yahya R. Kido, akisindikizwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson O. Ndiege.
Katika hotuba yake, Dkt. Ndiege alizihimiza vyama vya ushirika kutoa huduma bora kwa wanachama kwa kuzingatia misingi ya ushirika na kutumia mifumo ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi, uwazi na utoaji wa huduma kwa wakati. Aidha, Mhe. Kanali Yahya R. Kido alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirika k**a chachu ya maendeleo kuanzia ngazi ya familia hadi taifa kwa ujumla.
SCCULT (1992) LTD inaendelea kuimarisha ushirikiano na wanachama pamoja na wadau mbalimbali kwa maendeleo endelevu ya sekta ya ushirika.
(1992)ltd