26/06/2026
🌍🤝 KUNDUCHI BEACH RUINS HERITAGE & NETWORKING TOUR 2026 - 7.7.2026
Kuna safari ambazo huisha unapofika nyumbani, na kuna safari ambazo hufungua milango ya fursa, maarifa na urafiki mpya. Hii ni mojawapo.
AFRIKA TALII ORGANIZATION inawaalika NGOs, CBOs, CSOs, Makampuni, Taasisi na wadau wa maendeleo kushiriki safari maalum ya kuhamasisha Utalii wa Ndani, Uhifadhi wa Mazingira na Urithi wa Utamaduni kupitia ziara ya Kunduchi Beach Ruins Heritage & Networking Tour.
📅Tarehe: 07.07.2026
📍 Kuanzia: Viwanja vya Sabasaba
🕕 Muda: Saa 6:00 mchana – Saa 12:00 jioni
💰 GHARAMA ZA USHIRIKI 🐦 Early Bird: TSh 35,000/= (Kwa watakaolipia hadi tarehe 30.06.2026)
🎟️ Bei ya Kawaida: TSh 45,000/= (Kuanzia tarehe 01.07.2026 – 06.07.2026)
👧👦 Watoto (Miaka 5–16): TSh 30,000/=
✅ Gharama zinajumuisha:
🚌 Usafiri wa kwenda na kurudi
🎫 Kiingilio cha Kunduchi Beach Ruins
🌳 Kushiriki zoezi la kupanda mti wa kumbukumbu
🤝 Networking na wadau mbalimbali
📸 Picha za kumbukumbu na kushiriki shughuli zote za programu.
🌱 Shughuli kuu zitakazofanyika: ✔️ Kutembelea Magofu ya Kale Kunduchi.
✔️ Kupanda mti wa kumbukumbu kuhamasisha Uhifadhi wa Mazingira.
✔️ Networking na wadau kutoka sekta mbalimbali.
✔️ Kujifunza na kubadilishana mawazo kuhusu fursa za miradi ya Mazingira, Utalii na Climate Change zinazoweza kuleta maendeleo kwa jamii zinazozunguka eneo la urithi.
🛍️ Kabla ya safari kuanza, washiriki watapata nafasi ya kutembelea Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kwa matembezi na manunuzi.
🏅 NGOs zitakazoshiriki kupitia wawakilishi wao zitapatiwa Certificate of Recognition & Appreciation, itakayotolewa na Mhifadhi wa Magofu ya Kale Kunduchi, Afande Victoria Bache.
📩 Tuma Jina la Shirika, Jina la Mwakilishi na Email ya Shirika kwa ajili ya maandalizi ya cheti.
"Utalii wa Ndani ni nguvu ya uchumi. Uhifadhi wa Mazingira ni urithi wa vizazi vijavyo. Tukitembelea, tunajifunza; tukihifadhi, tunalinda historia ya Tanzania." 🇹🇿🌍💚