21/12/2021
TAJIRI WA MADINI ALIYETHAMINI DINI.
Alikuwa Ni mtu aliyefahamu UMUHIMU wa utu wa WATU wengine. Shughuli kuu aliyojihusisha nayo ilikuwa uuzaji na ununuzi wa vito vya THAMANI , alinunua ,aliuza na kusambaza MADINI ya dhahabu. Alijaliwa na kumiminiwa BARAKA tele , kufurika kwa neema kubwa kubwa na ndogondogo vyote alijaliwa navyo. Alimiliki majengo ,mashamba ,magari na familia nzuri YENYE mke na watoto wake watatu,
Sikutaka kusubiri wino wa kalamu yangu ikauke na karatasi hii kupeperushwa kabla ya kuyaandika haya unayoenda kuyaaoma kuhusu MTU huyu,
Kwanza kabisa hakujisahulisha kuhusu ugumu wa maisha kwa watu wa hali ya chini, maana kuna MTU akifanikiwa hudhani kuwa watu wote wamefanikiwa na kuamini hakuna MTU mwenye njaa, wasio na nguo , wanaotembea peku pasipokuwa na viatu au hata wajane na yatima wasiofahamu hatima yao na huzuni katika mitima yao. Basi tumwite Hantigaro , Alijihoji na kuwaza utofauti wake wa kiuchumi na watu wengi waliomzunguka na kugundua ulikuwa utofauti mkubwa Sana , lakini Sasa hakutaka kabisa au kusubiri kuambiwa kuhusu majanga yaliyowakabili watu Hawa , Hantigaro aliamka na kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo uhalisia wa ugumu wa maisha ya MTU wa kawaida na kugundua kuwa watu wanaishi katika kuvumilia na sio kujivunia,
Hapa ndio kisa chetu kinanoa nanga na nahodha Makini Sana asiyeyumbishwa na mawimbi ya bahari . Hantigaro alionekana akiagiza chakula , alikula kwa mamantilie chakula Cha mchana , macho ya wengi yalimwelekea na minong'ono ya chini kwa chini zilisikika na sauti za nziii , alikula huku akiwatazama wapishi na wahudumu ,nguo walizovaa na Kanda mbili miguuni hoja si kuwaelezea mwonekano wa watu Hawa Hantigaro yeye aliwangalia kwa jicho la masikitiko na kugundua ugumu wa kipato kiliwasababisha watu wale kuishi maisha yale. Alikuja mdada mwenye ujauzito na kuomba kumhudumia , kwa unyenyekevu mkubwa Hantigaro aliulizia Bei ya chakula akaambiwa wali samaki K**a kawaida elfu moja Mia tano na juisi ya kusaga Mia tano aliagiza akala na