03/12/2024
Leo tarehe 03 December 2024, Katibu Mkuu wa Education For Disabled Tanzania (EFDT), Bw. Christopher Mwasota (wa kwanza kulia) amehudhuria maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Mgeni rasmi wa maadhimisho haya ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko, ambapo maadhimisho haya yamebebwa na kauli mbiu: “Kukuza uongozi wa watu wenye ulemavu kwa mustakabali shirikishi na endelevu.”
EFDT itaendelea kuhamasisha na kuwekeza katika mipango inayowezesha watu wenye ulemavu kupata elimu bora, ujuzi wa kiuchumi, na nafasi za uongozi ili kuunda jamii jumuishi na endelevu.