The Same Qualities Foundation

The Same Qualities Foundation we value the qualities of all kids

03/09/2026

Kamati ya Afya na Mazingira ya maandalizi ya AFCON imetembelea Hospitali ya ALMC jijini Arusha kwa lengo la kufanya tathmini na kuchagua hospitali itakayohusika katika utoaji wa huduma za afya kuelekea AFCON 2027.

Ziara hiyo imeongozwa na Boubakary Sidiki, ambaye ni Medical Manager / Inspection of all the medical facilities, ambapo kamati imekagua miundombinu pamoja na vifaa vya kisasa vya kitabibu, ikiwemo huduma za imaging na ultrasound, ambapo kamati imerizishwa na miundombinu ya hospitali hiyo.

Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Sidiki amesema ameridhishwa na huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo na kueleza kuwa miundombinu hiyo inaongeza uhakika wa usalama wa kiafya kwa wachezaji na wageni wakati wa AFCON 2027.

"Nimefarijika sana kuona huduma hizi za kisasa za picha za matibabu, imaging na ultrasound. Hii inatupa imani kubwa kuwa miundombinu yetu ya afya imejipanga kikamilifu kuhakikisha usalama na afya za wachezaji pamoja na wageni wote wa kimataifa wakati wa AFCON 2027."

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za ukomo wa bidhaa za mafuta ya petroli kwa...
02/09/2026

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za ukomo wa bidhaa za mafuta ya petroli kwa mwezi Septemba 2026, huku bei za petroli na dizeli zikishuka nchini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bei ya petroli imeshuka kwa Shilingi 102 kwa lita, huku dizeli ikishuka kwa Shilingi 101 kwa lita. Bei hizo mpya zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Septemba 2, 2026 saa 6:01 usiku.

Kwa Dar es Salaam, bei ya rejareja imewekwa kuwa Shilingi 3,796 kwa lita ya petroli, Shilingi 3,877 kwa dizeli na Shilingi 3,713 kwa mafuta ya taa.

EWURA imesema wafanyabiashara wanapaswa kuzingatia bei kikomo zilizowekwa na kuonyesha bei hizo wazi kwenye vituo vyao. Pia, wanatakiwa kutoa stakabadhi za mauzo kwa wateja.

Aidha, wananchi wanaweza kupata taarifa za bei kikomo za mafuta katika maeneo yao kwa kupiga *152*00 # na kufuata maelekezo. Huduma hiyo inapatikana bure kupitia mitandao yote ya simu nchini.

EWURA imeonya kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara watakaokiuka masharti yaliyowekwa.

Msajili wa Hazina ateta na uongozi wa kampuni ya BarrickNa Mwandishi wa OTRDar es Salaam. Msajili wa Hazina, Bw. Nehemia...
02/09/2026

Msajili wa Hazina ateta na uongozi wa kampuni ya Barrick

Na Mwandishi wa OTR

Dar es Salaam. Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Barrick Corporation, mwanahisa mwenza wa Twiga Minerals Corporation Limited (TWIGA), pamoja na uongozi wa TWIGA, kujadili maendeleo na masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa miradi inayosimamiwa na kampuni hiyo.

Mazungumzo hayo yalifanyika Jumanne, Septemba 1, 2026, wakati ujumbe wa Barrick ulipofanya ziara katika Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), jijini Dar es Salaam.

Ujumbe wa Barrick uliongozwa na Roelie G*y Von Pittius, Meneja wa Fedha wa Barrick kwa Afrika na Mashariki ya Kati, akiambatana na Candace Simpson, Meneja wa Kodi wa Afrika na Mashariki ya Kati; Melkiory Ngido, Meneja wa Barrick nchini Tanzania; na Judith Chambua, Meneja wa Kodi wa Barrick Tanzania.

Katika kikao hicho, Serikali, kupitia OTR, na Barrick, ambao ni wanahisa wenza wa TWIGA, walijadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo na uendeshaji wa miradi ya uchimbaji wa dhahabu inayomilikiwa kwa ubia kupitia TWIGA.

Miongoni mwa miradi iliyojadiliwa ni pamoja na migodi ya North Mara na Bulyanhulu, pamoja na Buzwagi, ambao kwa sasa upo katika hatua za mwisho za kufungwa.

Uongozi wa TWIGA pamoja na wataalamu kutoka Barrick walishiriki katika kikao hicho kwa kutoa taarifa na ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo na uendeshaji wa miradi hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Bw. Mchechu alisema Serikali, kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika uendeshaji wa miradi ya TWIGA, kwa lengo la kuhakikisha miradi hiyo inaendelea kwa ufanisi, kuongeza uzalishaji na kuchangia zaidi katika uchumi wa Taifa.

Aidha, Bw. Mchechu alisisitiza kuwa sekta ya madini inaendelea kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa na mapato ya Serikali, ikiwemo kupitia gawio linalotokana na uwekezaji wa Serikali katika kampuni za madini.

Bw. Mchechu alisema Serikali inathamini ushirikiano wake na Barrick na inaendelea kutumia uzoefu uliopatikana kupitia uhusiano huo katika kuimarisha sekta ya madini nchini.

02/09/2026

Watoto, wakiwemo wachanga, wanaripotiwa kuwa miongoni mwa waathirika wa shambulio la Marekani lililotokea wakati wa sherehe ya harusi katika mji wa Sirik, kusini mwa Iran.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Iran, baadhi ya watoto waliojeruhiwa katika shambulio hilo wamepelekwa katika hospitali ya Minab kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Shambulio hilo limeripotiwa kusababisha vifo na majeruhi kadhaa, ingawa taarifa kamili kuhusu hali ya waathirika bado zinaendelea kutolewa.

02/09/2026

Kamati ya Afya na Mazingira ya maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027 mkoani Arusha imeendelea na zoezi la kutembelea na kukagua vituo vya afya vinavyoweza kutumika katika utoaji wa huduma za dharura na matibabu wakati wa mashindano hayo.

Kamati hiyo imetembelea Hospitali ya Selian pamoja na JKCI-ALMC jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuchagua hospitali zitakazokuwa tayari kutoa huduma kwa wageni, wachezaji na mashabiki watakaofika mkoani humo wakati wa AFCON 2027.

Ujumbe huo umepokelewa na Kaimu Mkuu wa Hospitali ya JKCI-ALMC, Gertrude Anderson, ambaye ameueleza kuhusu huduma zinazotolewa hospitalini hapo pamoja na uwezo uliopo katika kukabiliana na wagonjwa wenye mahitaji mbalimbali.

Ameeleza kuwa kamati imeridhishwa na maandalizi yaliyopo katika hospitali hizo, huku ikitoa maeneo machache yanayohitaji kuboreshwa kabla ya mashindano hayo.

Aidha, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura wa JKCI-ALMC, Peter Mabula, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya AFCON 2027 mkoani Arusha, amesema ukaguzi huo ni muhimu katika kuhakikisha mfumo wa huduma za dharura unakuwa tayari kukabiliana na mahitaji yatakayojitokeza wakati wa mashindano.

Ukaguzi huo unaelezwa kuwa sehemu ya maandalizi ya mkoa wa Arusha kuhakikisha miundombinu ya afya, huduma za dharura na mazingira ya hospitali yanakidhi mahitaji yatakayohitajika katika kipindi cha AFCON 2027.

Kamati hiyo imesisitiza umuhimu wa kufanyia kazi maeneo yaliyoainishwa ili kuhakikisha hospitali zitakazoteuliwa zinakuwa tayari kutoa huduma kwa ufanisi na kwa wakati, wakati Tanzania ikijiandaa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

01/09/2026

Kijana anayefahamika kwa jina la Aron Enock Urio, aliyekuwa dereva wa bodaboda eneo la Tengeru kwa Fundi, amefariki dunia baada ya kukutwa ameuawa ndani ya shamba katika Kitongoji cha Madira, Kijiji cha Singisi, Kata ya Sela Singisi, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Aron alikuwa ametoweka kwa siku kadhaa, huku ndugu na marafiki wakiendelea na juhudi za kumtafuta.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mwili wake ulikutwa ukiwa na majeraha mbalimbali, huku macho yake yakidaiwa kutobolewa.

Inadaiwa kuwa mwenye shamba hilo ndiye aliyegundua mwili huo asubuhi alipokuwa akiendelea na shughuli za shambani, ndipo alipowasiliana na mamlaka za eneo hilo.

Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu, ambao ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya taratibu zaidi.

Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha tukio hilo na kuwabaini wahusika, huku wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia uchunguzi wakihimizwa kuwasiliana na mamlaka husika.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha jana Agosti 31, 2026 majira ya usiku lilimkamata Godlisten Elisante Malisa akiwa na mwenza...
01/09/2026

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha jana Agosti 31, 2026 majira ya usiku lilimkamata Godlisten Elisante Malisa akiwa na mwenzake kutokana na tuhuma za jinai zilizokuwa zinachunguzwa dhidi yake.

Aidha baada ya mahojiano wameachiwa kwa dhamana wakisubiri taratibu zingine za kisheria kukamilishwa.

01/09/2026

Mkazi wa Kitongoji cha Katabradik, Kata ya Dareda wilayani Babati, mkoani Manyara, Emmanuel Qamara, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 65–70, anadaiwa kuuawa baada ya kushambuliwa na fisi, katika tukio linalodaiwa kuwa la tatu kutokea katika eneo hilo.

Tukio hilo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia leo, Agosti 31, 2026, ambapo baadhi ya mabaki ya mwili wa marehemu yamekutwa karibu na Shule ya Msingi St. Patrick Winters. Wananchi wameendelea na msako katika eneo hilo kwa ajili ya kutafuta mabaki mengine ya mwili wa marehemu.

Baadhi ya vitu vilivyokutwa katika eneo la tukio, ikiwemo viganja vya mikono, kitambulisho cha NIDA, simu, koti pamoja na rungu, vimetajwa kusaidia katika utambuzi wa marehemu.

Mkazi wa Dareda, Christine Charles, amesema eneo hilo lina vichaka na mashamba ya mbaazi yanayopakana na njia zinazotumiwa na fisi kutoka maeneo ya milimani, hali ambayo imeendelea kuibua hofu miongoni mwa wananchi, hasa kutokana na uwepo wa shule katika maeneo ya jirani.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Seloto, Daniel Wema Duwe, amesema mashambulizi ya fisi yameongezeka mwaka huu na kwamba uongozi umeshatoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika na wanyamapori.

Duwe amezitaka mamlaka hizo kuchukua hatua za kudhibiti wanyama hao, huku wananchi wakihimizwa kuwa waangalifu na kuepuka kutembea katika maeneo hayo nyakati za usiku.

01/09/2026

Rais wa Yanga ukishangiliwa na washabiki wa Yanga baada ya Yanga kuwafunga Fountain gate jijini Arusha

Address

P. O BOX 11641
Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Same Qualities Foundation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share