Kijani App

Kijani App Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Kijani App, Non-Governmental Organization (NGO), Hans Street Arusha, Arusha.

Elimu kwa Wakulima, Wafugaji na Wadau wa Mazingira!

>> Kijani App inapatikana BURE Google Play Store.
>> Jifunze mbinu za asili zitakazokupa matokeo makubwa shambani.

📞 Wasiliana nasi kwa WhatsApp kupata msaada wa kitaalamu

Inasimamiwa na Justdiggit.

KIJANI SHAMBANI: Kutoka Kijiji cha Mwanga, Mkoani Singida, mtumiaji wetu anasema, “App hii imenisaidia kurudisha uoto wa...
25/05/2026

KIJANI SHAMBANI: Kutoka Kijiji cha Mwanga, Mkoani Singida, mtumiaji wetu anasema, “App hii imenisaidia kurudisha uoto wa asili katika mazingira yangu. Maarifa kupitia Kijani yamenisaidia kutunza maji kipindi cha masika shambani kwangu.”

Tuambie namna unavyotumia shambani kwako kwa kutuma ujumbe wa WhatsApp!

18/05/2026

Mapema mwezi huu, Justdiggit ilishiriki kongamano la Global Landscapes Forum lililofanyika jijini nchini Kenya.

Katika kongamano hilo, Natasha alipata nafasi ya kufanya mahojiano kuhusu , ambapo alieleza jinsi wakulima wanavyoweza kutumia simu zao kujifunza mbinu mbalimbali na kuboresha mashamba yao kwa urahisi zaidi.

Asanteni sana We are Tell Media kwa kuandaa video hii nzuri!

ENG:

Earlier this month, Justdiggit participated in the Global Landscapes Forum held in Nairobi, Kenya.

During the event, our very own Natasha had the opportunity to speak about Kijani App, explaining how farmers can use their phones to learn new techniques and improve their farms 🌳🌱more easily.

💚A big thank you to Telling Earth's Life & Legacy for this wonderful video💚

Wakulima wanasemaje kuhusu mafunzo yetu?Mtumiaji mmoja wa   anasema, “Kozi hizi zinanisaidia kutunza mazingira, hasa kup...
14/05/2026

Wakulima wanasemaje kuhusu mafunzo yetu?

Mtumiaji mmoja wa anasema, “Kozi hizi zinanisaidia kutunza mazingira, hasa kupunguza joto na kuvuna maji mashambani. Vitu vilivonivutia kwanza ni njia rahisi kurudisha uoto wa asili, tofauti na miti ya kupanda, kwani hakina gharama kubwa katika kutunza na inawahi kukua.”

Anaeleza zaidi, “Matarajio yangu ni kuona mabadiliko, kuongeza kipato na fursa mbalimbali za biashara ndogondogo zinazotokana na mazao.”

Unafuatilia washirika wetu ndani ya  ?Kwa kufanya hivi, utapata taarifa muhimu kutoka kwao kupitia ujumbe mfupi unaokufi...
05/05/2026

Unafuatilia washirika wetu ndani ya ?

Kwa kufanya hivi, utapata taarifa muhimu kutoka kwao kupitia ujumbe mfupi unaokufikia kwa wakati. Hii itakusaidia kubaki karibu na kile kinachoendelea na kupata fursa mpya bila kuchelewa.

Vilevile, utaendelea kujifunza zaidi kupitia maudhui na taarifa zinazopatikana kwenye ukurasa wetu wa Kikapu. Endelea kuwa karibu nasi! App inakuletea njia rahisi ya kujifunza, kushirikiana na kukua pamoja na washirika wetu.

Kijani App inapenda kuwatakiwa Watanzania wote heri ya Mei Mosi!
01/05/2026

Kijani App inapenda kuwatakiwa Watanzania wote heri ya Mei Mosi!

Kisiki Hai hurejesha miti, lakini mafanikio yake hutegemea usimamizi mzuri. Chagua machipukizi yenye afya na nguvu kweny...
29/04/2026

Kisiki Hai hurejesha miti, lakini mafanikio yake hutegemea usimamizi mzuri. Chagua machipukizi yenye afya na nguvu kwenye kila kisiki, kisha ondoa yale dhaifu ili yaliyo bora yaweze kukua vizuri.

Kupogolea kwa umakini kunasaidia miti kuwa imara, kuboresha afya ya udongo, na kuongeza uzalishaji wa shamba kwa muda mrefu.

Kumbuka, unatakiwa kupogolea kuanzia chini kuelekea juu ili usichubue shina..

Heri ya Siku ya Sayari Dunia!Siku hii itukumbushe kuwa, hatua ndogo tunazochukua kila siku zinaleta mabadiliko makubwa k...
22/04/2026

Heri ya Siku ya Sayari Dunia!

Siku hii itukumbushe kuwa, hatua ndogo tunazochukua kila siku zinaleta mabadiliko makubwa kwa ardhi yetu, jamii zetu, na maisha yetu.

Kwa kutumia mbinu endelevu k**a matandazo, matuta ya kuvunia maji, na tunaweza kuboresha afya ya udongo, kuongeza uzalishaji, na kuwa na mashamba bora zaidi.

Tuendelee kuitunza ardhi inayotutunza. Ni jambo gani unafanya shambani, au katika jamii yako kulinda ?

Jifunze kuhusu   kupitia ushuhuda wa Mkulima aliyefanikiwa kurejesha maelfu ya miti huko Singida.Anaeleza, “Miti hii ime...
17/04/2026

Jifunze kuhusu kupitia ushuhuda wa Mkulima aliyefanikiwa kurejesha maelfu ya miti huko Singida.

Anaeleza, “Miti hii imeleta faida nyingi kwa ardhi na maisha yangu. Hakuna tena mmomonyoko wa udongo, ardhi inashikilia unyevu kwa muda mrefu, joto limepungua, na kuna kivuli cha kutosha.”

Fungua sasa kisha bonyeza Kikapu kusoma zaidi.

08/04/2026

Sasa unaweza kufuatilia mashirika mbalimbali ndani ya Kijani App na kupata taarifa moja kwa moja kutoka kwako.

Angalia video hii na zingatia hatua za kufuata ili kufuatilia mashirika haya na kupata maarifa muhimu.

31/03/2026

Tuna vitu mbalimbali ndani ya App yetu, kuanzia kozi mbalimbali ndani ya sehemu ya Maarifa (sasa Mbinu), shuhuda na simulizi katika ukurasa wa Kikapu, pamoja na vitu vingine vingi..

K**a bado huna App ya Kijani, ipakue bure kwa kutembelea Google Play Store au bonyeza https://t.ly/bBISa

25/03/2026

Unajiuliza hatua za kufuata mara tu unapopakua ? Ni rahisi sana, tazama video hii! Chagua lugha, andika jina lako, ruhusu App kusoma eneo ulipo na kutuma taarifa.

Umekwama na unahitaji usaidizi wetu? Wasiliana nasi kwa kubonyeza kitufe cha WhatsApp katika sehemu yetu ya Msaada.

Address

Hans Street Arusha
Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kijani App posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share