07/11/2024
Uongozi wa Chuo cha Misitu unayo furaha
kuwaalika wahitimu wote wa zamani wa
Chuo cha Misitu kushiriki kwenye Mahafali ya
84, yatakayofanyika tarehe 15 Novemba 2024,
katika viwanja vya chuo.
Hii ni fursa maalum ya kuungana tena na
kusherehekea mafanikio yetu ya pamoja.
Mahafali haya yataangazia urithi na
mchango wa chuo chetu katika sekta ya
misitu, pamoja na kujenga mshikamano
miongoni mwa wahitimu. jiunge nasi
katika tukio hili la kihistoria.
Karibu sana