THE TANZANIA YOUTH ELITE COMMUNITY
Ni jumuiya/taasisi ya vijana wa kitanzania isiyo ya kiserikali inayo jishughulisha na maswala ya vijana .ikiwamo uchumi ,kijamii na maswala mengine yahusuyo vijana wa Tanzania .Jumuiya hii ni ya kiraia yenye makao makuu yake mjini Arusha Tanzania . inaamini katika utu ,unaotafuta thamani ya kutambuliwa ,kuheshimiwa na kuthaminiwa kwa binadamu we
nye kipato cha chini kundi kubwa likiongozwa na vijana wenye uchumi mdogo katika jamii ya kitanzania waundao takribani asilimia 67% kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002.(T.Y.E.C) Inalenga zaidi kuwainua vijana kiuchumi na kuwawezesha vijana kiuchumi ,kwani ndilo swala kubwa zaidi lililo tawala na kukwamisha maisha ya watanzania na vijana wasomi wa kitanzania. (T.Y.E.C)Inaazimia kuhakikisha kuwa kipato cha kijana msomi wa kitanzania inafanana na kulingana na elimu stahiki aliyonayo kijana wa kitanzania wanao hitimu katika fani mbalimbali Tanzania.(T.Y.E.C) Inalenga kwa makusudi kabisa kuwawezesha vijana wa kidato( iv) waliomaliza masomo yao lakini kwa bahati mbaya hawajaweza kuendelea na masomo yao kwa kadri ya mategemeo yao ili kujipatia elimu na kuboresha maisha yao .Sasa T.Y.E.C inalenga kuwaunganisha wasomi hawa na wasomi wengine wa kitanzania ili waweze kutafakari kwa pamoja ,na kitoa majibu ya maswali magumu yanayo wakumba vijana wasomi wakitanzania wanaohitimu katika taaluma mbalimbali bila kupata mafanikio stahiki ya kiuchumi licha ya Tanzania kuwa na utajiri mkubwa wa kupindukia .Ni wazi kuwa swala la ajira kuwa ni tatizo kubwa kwa vijana wengi wa kitanzania tangu uhuru yaani miaka 50 iliyopita lakini bila kuonekana misingi yoyote inayo tarajiwa kuleta mapinduzi ya haraka kabisa ili kufanya vijana wa kitanzania wenye elimu kuanzia kidato(iv) na ngazi zingine kubwa za elimu kujivunia kuzaliwa kwao katika ardhi ya Tanzania .Vilele (TYEC)Inaunga mkono jitihada za (YALDA),(AYA),(TAYOA) na jumuiya zingine zote ndani na nje ya bara la Africa zilizo jikita kwa muda mrefu kwenye namna ya kuwawezasha vijana wa kitanzania waliokosa mwelekeo kwenye maswala ya ajira na kijamii kwa muda mrefu. Vilevile (T.Y.E.C) inaunga jitihada za taasisi mbalimbali zilizotangulia katika kuwaelimisha vijana,kutoa elimu kuhusu maambukizi ya ukimwi na majanga mengine ya kijamii yanayoitesa jamii kwa muda mrefu sasa kundi kubwa likiongozwa na vijana (T.Y.E.C) sasa inatoa kwa taasisi zingine kuungana na (T.Y.E.C) ili kusukuma gurudumu la kuhakikisha kuwa vijana wanaepuka utegemezi na kujitegemea kiuchumi na kijamii ili waweze kujenga taifa la kujitegemea. Kwa hivyo basi( T.Y.E.C) inatoa wito kwa vijana wote wa kitanzania kujiunga na jumuiya ili waweze kujiinua kiuchumi kwa kusudio la kujenga taifa linaloepuka utegemezi.(T.Y.E.C) inawakumbusha vijana kuwa uzalendo wa dhati kwa Tanzania utakuja pale vijana wake watakapokubali kuungana kwa pamoja na kujenga hoja ya pamoja iliyokosekana kwa miaka mingi sasa hali kadhalika (T.Y.E.C) inatoa wito kwa vijana kushika nyadhifa mbalimbali katika jumuiya kwa ngazi mbalimbali kulingana na mikoa wanayotoka vilevile( T.Y.E.C )inatoa wito kwa watu binafsi,taasisi mbalimbali na serikali kuunga jitihada za kufanikisha vijana wa kitanzania kufikia malengo yao. Na mwisho vijana kote nchini wenye vigezo k**a ilivyotafsiriwa kwenye katiba ya( T.Y.E.C) sehemu ya (uwanachama) wanaaswa kujiunga mapema iwezekanavyo ili kufikia azma ya kujenga hoja ya pamoja na kuleta mabadiliko ya haraka kwao binafsi na taifa la Tanzania kwa ujumla
(VIJANA TUNALIANGAZA TAIFA)