05/05/2026
Umoja Tanzania inatangaza nafasi 110 za vijana ambao hawakuweza kuendelea na elimu ya Sekondari kwasababu ya hali mbaya ya kiuchumi.
Tunaamini kuwa kila kijana ana haki ya kuishi maisha huru dhidi ya umaskini, unyanyasaji na unyonyaji, na ili kufanikiwa anahitaji elimu jumuishi, afya bora ya mwili na akili, pamoja na fursa za kujipatia kipato kwa heshima.
Kupitia Kituo cha Umoja kilichopo Arusha, tunatoa huduma muhimu, fursa za elimu na mazingira salama kwa vijana walio katika mazingira magumu, tukilenga kuwajengea ujuzi, kujiamini na uwezo wa kujisimamia maisha yao. Programu zetu zinachangia kuboresha ufaulu wa masomo, kukuza vipaji, na kuwawezesha vijana kupata ajira au kujiajiri, huku tukitoa pia msaada wa kisaikolojia, afya, michezo na sanaa.
Tupigie simu kwenye namba hii 0783009332 na 0785009332 endapo una swali lolote au unahitaji kujua zaidi kuhusu Ufadhili wa Umoja.Tafadhali wajulishe vijana kuhusu UFADHILI HUU KATIKA MASOMO, Bila kusahau kuzingatia vigezo vilivyoorodheshwa hapo juu.
KARIBU SANA UMOJA