31/12/2023
SALAMU ZA MWAKA MPYA 2024
Bwana Yesu asifiwe ! Leo ni tarehe 1 mwezi January 2024 kwa mujibu wa kalenda ya Gregorian .Nasema hivi kwa sababu zipo kalenda nyingine ,mfamo ya kiyahudi ,ya kichina na Ile ya Kiislamu . Tunamshukuru sana Mungu kwa upendo wake na upendeleo wa kupata neema ya kuona mwaka mwingine .Mwaka 2023 ulikuwa mwaka mzuri kwa wengine na mbaya kwa wengine .Kwa vyovyote vile k**a unasoma ujumbe huu haijalishi upo katika hali gani mshukuru Mungu katika Kristo Yesu .Hakuna maisha tambarare na hakuna mahali Mungu ameahidi kuwa maisha yatakuwa rahisi ,hapana ! Bali Yeye anatupa nguvu za kustahimili na kushinda kwa Roho wake . Kimsingi unaweza usiwe mwaka wa tofauti sana kulingana na fikra na mtazamo wako .Fikra njema na mtazamo mzuri unakufanya kuona na kutazama mambo kwa upeo tofauti .Binafsi nimejifunza kuomba na kumtegemea Mungu hata k**a nitabaki peke yangu na msimamo wangu .Kauli mbiu yangu ni ,Heri kufa mikononi kwa Mungu kuliko kutumaini miungu mingine .Nakuandikia ujumbe huu kwa upendo ,hebu tuangalie maandiko yanasema nini Mwanzo 1:3
[3]Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
Mungu ni Mungu wa nyakati zote ,Yeye ndiye aliyeumba muda kwa sababu kabla ya kuwa chochote Yeye yupo ,ni alpha na omega .Nuru haichangamani na Giza ,Nuru hufukuza Giza .Mwaka 2024 ,kuwe na Nuru kwenye maisha yako ,kila nyanja/sekta au eneo lolote LA maisha yako .Giza lisikushinde .Kila ninaposoma mstari huu ,ufunuo ninaoupata ni mkuu sana ,Kwanin Mungu alisema kuwe Nuru ? Tafakari wewe Binafsi . Yesu anasema "Ninyi ni Nuru ya Ulimwengu " hii ni habari njema iliyoje ? Mungu aangaze maisha yako kwa Nuru ya uso wake !!Zaburi 44:3
[3]Maana si kwa upanga wao walivyoimiliki nchi,
Wala si mkono wao uliowaokoa;
Bali mkono wako wa kuume, naam, mkono wako,
Na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwaridhia. Unajua kuwa ni mkono wa Bwana umekuvusha ? Jihadhari usije kusahau jambo hilo ,ni mkono wake umekuvusha .Habari hii inawahusu wana wa Israel Mungu alivyowavusha kwa mkono wake . Mwaka 2024 ni mwaka wa Bwana ,ni mwaka wako .Na huu ndio unabii wa mwaka 2024
Isaya 61:2-3
[2]Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
To proclaim the acceptable year of the LORD, and the day of vengeance of our God; to comfort all that mourn;
[3]kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.
To appoint unto them that mourn in Zion, to give unto them beauty for ashes, the oil of joy for mourning, the garment of praise for the spirit of heaviness; that they might be called trees of righteousness, the planting of the LORD, that he might be glorified........
Huu ni mwaka wa Bwana ! Ni mwaka wako ! Utafanya kazi na kuhesabu faida ,Afya yako itastawi ,Ndoa yako itastawi , biashara na miradi yako ,Watoto wako watasoma na kufaulu ,Utapakata mtoto na Utaitwa Heri na mbarikiwa . Umngojee Bwana usiwe na haraka .
*Kumbuka pamoja na kwamba umeomba muda mrefu ,hii haimaanishi lazima ajibu sawasawa na mapenzi yako ,No! ,Yeye anajibu maombi yako k**a ni mapenzi yake*
Jambo hili ni Muhimu sana ili usimkasirikie Mungu ,Yeye anatizama ahadi zake azitimize kwetu .Ni ombi langu Mungu akuepushe na hatari zote na mitego ya yule mwovu .
Mwanzo 22:17
[17]katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako k**a nyota za mbinguni, na k**a mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;
Mungu akupe kumiliki mlango wa adui zako .
Wewe ni mshindi na zaidi ya mshindi ,Mungu akubariki sana sana ,Amen +++
*Happy New year 2024*
Barakael Willium Teti
Raisi wa huduma ya "Send the gospel international ministries "
Tell:+255756951275
Whatsapp :+255756951275
E-mail : [email protected]
YouTube channel
Baraka Teti