16/06/2026
TUFICHE WAPI WATOTO WETU
Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, tunashiriki shairi lililoandikwa na Sharifa Mohamed na kughaniwa na Iddy Ninga likibeba ujumbe mzito wa kupinga ukatili dhidi ya watoto.
Kila mtoto ana haki ya kuishi salama, kupendwa, kusikilizwa na kukua katika mazingira yenye ulinzi na matumaini. Tushirikiane kukomesha ukatili dhidi ya watoto na kujenga jamii inayoweka maslahi yao mbele.
Mtoto Salama, Taifa Imara.✊🏿