Riyadh Swaliheen Kisw

Riyadh Swaliheen Kisw Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Riyadh Swaliheen Kisw, Arusha, Arusha.

DUA YA KUTOKA NYUMBANI.
22/02/2026

DUA YA KUTOKA NYUMBANI.

DAIMA USIACHE KUSALI
25/01/2026

DAIMA USIACHE KUSALI

06/05/2025

Dua ya kutoka nyumbani
Transliteration:
Allahumma inni a‘udhu bika an adhilla aw udhalla, aw azilla aw uzalla, aw azlima aw uzlama, aw ajhala aw yujhala ‘alayya.

Maana kwa Kiswahili:
Ee Mola wangu, najikinga Kwako nisije nikapotea au nikapotoshwa, nikateleza au nikatelekezwa, nikafanya dhulma au nikadhulumiwa, nikafanya ujinga au kufanyiwa ujinga.

04/05/2025

1. Dua ya Kuamka Asubuhi

Kwa Kiarabu:

> الْـحَمْـدُ لِلَّهِ الَّذِي أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا وَإِلَيْهِ النُّشُورُ

Transliteration (matamshi):

> Alhamdu lillaahil-ladhi ‘ahyaanaa ba’da maa amaatanaa wa ilayhin-nushoor.

Maana kwa Kiswahili:

> Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Ambaye ametufufua baada ya kutufisha (usingizini), na kwake ndiko kufufuliwa (siku ya mwisho).

09/01/2025

:

Assalaama alaykum, naomba jawabu k**a kuna wakati maalum na siku maalum au mchana au usiku kumeelezwa kuwa bora katika kufanya kitendo cha kujaamiiana kati ya mume na mke katika mafundisho ya uislamu na k**a kuna siku ama makruh au haramu na k**a kuna maelezo yanayoshauri kufanya kitendo hicho. Kwani kuna misemo k**a hiyo inatembea katika baadhi ya mitandao lakini nahofia huenda sio ya kiislamu thabiti
Shukran



:

Sifa zote njema Anastahiki Allah Mtukufu, Swalah na salamu zimfikie kipenzi chetu, Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Ahli zake na Maswahaba zake (r.a.) na Watangu Wema na waliowafuata kwa kheri mpaka Siku ya Kiyama.

Shukrani kwa swali hilo lenu kuhusu wakati unaofaa wa tendo la ndoa baina ya mume na mke.

Kwa hakika hakuna wakati maalumu uliowekwa kwa ajili ya kustarehe baina ya wanandoa. Wakati wowote ambao mutakuwa muko tayari munaweza kukutana, mchana au usiku, Jumamosi, Jumatatu au siku nyingine yoyote.

Na kwa hakika Mtume (s.a.w.w.) amewahimiza wake wawe ni wenye kuwatekelezea waume zao haja hiyo ya kindoa hata k**a mwanamke alikuwa akipika, aache na amtimizie mumewe matamanio yake.

Na ameeleza ikiwa mwanaume ametoka nje ya nyumba na akakutana na mwanamke na akavutiwa naye sana basi arudi haraka kwa mkewe ili apate kumtosheleza na hivyo kuondoa ile dhamira mbaya moyoni mwake.

Na Allah Anajua zaidi.

08/01/2025

: Je Mke Anapata Dhambi Akimkatalia Mumewe Kitendo Cha Ndoa Kwa Ajili Ya Machofu Ya Kazi..?
; ✍comment ya Kwanza👇

Address

Arusha
Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Riyadh Swaliheen Kisw posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share