30/07/2026
Maoni yako ni muhimu ama ni story tu? Ni muhimu bana.
Kila mwaka, serikali ya county hupanga budget ya vile pesa za wananchi zitatumika kwa maendeleo na huduma tofauti. Kabla hiyo budget ipitishwe, wewe pia uko na chance ya kusema vile unataka mambo yafanywe.
Public participation si kuenda meeting tu na kukaa kimya. Ni chance yako ya:
• Kuuliza budget ilitengenezwa aje.
• Kuhoji mbona priorities fulani zilichaguliwa.
• Kuongelea mahitaji ya wasee wa mtaa, especially vijana.
• Kushikilia viongozi accountable kwa maamuzi wanamake.
Sauti yako inaweza kubadilisha ni projects gani zitafanywa, huduma gani zitaboreshwa, na pesa zitatumika aje kwa county yako.
Ukiona notice ya public participation, jitokeze, ongea, usiogope kuuliza maswali, na uwe part ya kujenga Kenya unataka kuona.
Sauti yako ni muhimu. Ushiriki wako ni muhimu. Future yako ni muhimu.