Judai001 Da'awa Group

Judai001 Da'awa Group This page is for all muslim brother and sisters to help us preach Islam to all.

WAKRISTO RUKENI NAHII YESU ANATHIBITISHA YEYE SIOMUNGU "Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, MTU ambaye nimewaambia iliyo ...
25/04/2026

WAKRISTO RUKENI NAHII YESU ANATHIBITISHA YEYE SIOMUNGU

"Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, MTU ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo."

Yohana 8:40

Katika andiko hilo YESU kwa kinywa chake yeye mwenyewe amejiita kuwa ni "MTU". K**a kuna mtu ana ushahidi wowote katika biblia YESU akijiita MUNGU, basi nami hapo nitaamini kuwa YESU Mungu.

Hata hivyo, mnaweza kusema pia, kuwa YESU alikuwa Mungu na Pia alikuwa mtu. Hata hivyo tukitazama sifa mbalimbali za mungu k**a zilivyo tajwa au ainishwa na biblia, utaona hata kiduchu YESU hana sifa hizo.

Mathalani.

"Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza.."

Hesabu 23:19

Tumeona katika Yohana 8:40 Yesu akijiita Mtu, na hapa katika hesabu tunaambiwa Mungu si mtu, sasa wewe unayemuita Yesu Mungu umepata wapi?

NANI KAFUNDISHA YESU NI MUNGU?

"tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; "

Tito 2:13

Hayo maneno katika kitabu cha Tito, kimsingi ni barua ya kimisionari aliyo andika Paulo kwa watu wa Tito, k**a tuonavyo katika barua hiyo, pamoja na mambo mengine Paulo anawaambia watu wa Tito kuwa Yesu ni Mungu Mkuu, maneno haya ya Paulo yanakwenda kinyume kabisa na maneno ga Yesu mwenyewe aliyo yasema katika Yohana 8:40 lakini kinyume kabisa na mafundisho ya kinabii kutoka katika kitabu cha Hesabu 23:19.

YESU ANASEMAJE KUHUSU PAULO?

Awali ya yote Paulo hakuwahi kuwa mwanafunzi wa Yesu na hakuwahi kumuona Yesu Kristo. Yesu kabla hajapaa kwenda mbinguni aliwahi kusema maneno haya.

"Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi"

Yohana 16:1-3

Hapa Yesu anatabiri kuwa wanafunzi wake watakuja kuuliwa, anatabiri wakristo na wafuasi wa kanisa lake watakuja kuuliwa, na akasisitiza huyo atajaye wauwa wanafunzi wake hamjui yeye wala Baba(Mungu)

Nani huyo aliyeua wanafunzi wa Yesu? Jawabu ni Sauli ambaye ni Paulo.

"Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu."

Matendo 9:1-3

Kwa hivyo Mtu aliyetajwa na Yesu katika injili ya Yohana 16:1-3 kuwa atawaua wanafunzi wa Yesu si mwingine Paulo, na katika kitabu cha matendo tunaoneshwa ukatili wa Paulo kwa wanafunzi wa Yesu. Hata hivyo, Bwana Yesu anaendelea na utabiri wake juu ya Paulo katika aya hii.

"Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo"

Yohana 8:44

Katika aya hiyo Bwana Yesu anasema huyo Paulo si kwamba ni muuaji tu, lakini pia mtu muongo sana. Na uongo mkubwa alio ufanya Paulo ni pale aliposema kakutana na Yesu na kisha akajifanya kipofu.

"Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda"

Matendo 9:3-7

Baaada ya Paulo kuwaua sana wanafunzi wa Yesu na kuwatesa sana ili waache mafunzo ya Yesu, lakini wanafunzi wa Yesu waligoma na walikataa katakata kuachana na mafunzo Yasu. Pia naomba mjue, mafunzo ya Yesu yalikuwa mwiba kwa serikali(Dola ya Rumi) na Paulo alikuwa anatumiwa na serikali katika kuhakikisha wanafunzi wa Yesu wanaachana na ukristo/uyaudi.

Pamoja na juhudi hizo za Paulo lakini alishindwa, hivyo njia aliyo amua kuitumia si nyingine bali ni kujiunga na wanafunzi wa kristo. Na ili aaminike ndipo hapo alipotengeneza stori ya kumuona Yesu na maagizo ya upofu, lakini kubwa zaidi alimnunua Anania ili msaidie kufanikisha lengo lake. Kwa kumtumia Anania na kwa kudanganya kwake kuwa kamuona Yesu, wanafunzi wa Yesu walimkubali.

Na hapo ndipo Paulo alipoanza kuyachakua mafunzo ya Yesu, na ndio maana ukristo wa sasa si ule alio ufundisha Yesu.

YESU NA MFARISAYO.

"Ewe FARISAYO KIPOFU, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote."

Mathayo 26:23

Paulo msomi mkubwa alikuwa Farisayo, lakini Yesu alisema nini juu mafarisayo? K**a tulivyo ona, Yesu anawaona mafarisayo k**a vipofu, lakini kubwa katika andiko hili Yesu anamtabiri pia Paulo na maigizo yake ya upofu.

"Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu"

Matendo 23:6

Kwanza Paulo amekiri kwa kinywa chake kuwa yeye ni farisayo. Lakini hiyo haitoshi Paulo alijitia upofu a*o kuwa nao.

"Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi."

Matendo 9:8-9

Katika aya hizi tunaona kuwa Paulo amekiri kuwa Farisayo lakini pia tunaona Paul yuko katika maigizo ya upofu. Yote haya mawili yanakamilisha unabii wa Yesu pale aliposema

"Ewe farisayo kipofu.."

Mathayo 26:23

Katika aya hizo inatajwa sifa kuu au tabia kubwa ya Mafarisayo, na ambayo imethibiti(ilitimia) kwa Paulo. Sifa hiyo si nyingine bali UNAFIKI.

Paulo alikuwa mnafiki, yaani alijifanya muumini wa mafundisho Yesu ili mradi apate kuwapotosha wanafunzi wa Yesu, na hili kwakweli kafanikiwa sababu hakuna hata kanisa moja ambalo linafuata mafunzo ya asili ya Yesu. Kila kanisa lina kituko chake.

MWISHO.

Kwa kifupi huku nikizingatia maelezo yangu yote ya huko juu, kuwa YESU SI MUNGU, lakini hakumaanishi kuwa hakuna wanao muita au wanao amini Yesu Mungu. La kuzingatia k**a tukiambiwa kauli ipi ya kushika kati ya YESU mwenyewe na ya Paulo kwa vyovyote vile tunatakiwa kushika kauli ya Yesu.

Kauli zote za Paulo ambazo hazipingani na za Yesu, kauli hizo tutazifuata, lakini kauli yoyote ya Paulo inayo pingana na Yesu, kauli ya Paulo itapuuzwa na kuanguka, alafu watu wote wanatakiwa wafuate kauli ya Yesu.

Hakuna kauli ya Yesu anayo alijiita Mungu, lakini zipo nyingi akijiita Mtu au mwana wa adamu. Na siku zote alijitafautisha na Mungu. Yesu anakata mzizi wa fitina katika andiko hili.

"Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma"
Yohana 17:3

Nasema YESU SI MUNGU, na Paulo ana kesi ya kujibu kwa kudanganya ulimwengu, na kwa kuharibu mafundisho ya Yesu na kubwa zaidi kwa kuwatesa na kuwaua wanafunzi wa Yesu na wafuasi wake.

Katika kuendeleza urongo wa Paulo, watu wameambukizwa urongo, sasa wanatusambazia picha na sanamu za wacheza sinema na kisha wanataka tuziheshimu k**a Yesu, kweli watu wanaangamia kwa kukosa maarifa.

Tukutane katika coment

Wazee wa povu

05/04/2026

DON'T RISK YOUR LIFE TO DIE IN CHRISTIANITY!!!!!!!!
Below is what Jesus said about himself
1. I am a man (John 8:40)
2. I am a son of man (Matthew 11:19)
3. God sent me ONLY to the LOST SHEEP OF
ISRAEL (Matthew 15:24 and Matthew 10:5-6)
4. God is GREATER than me (John 14:28)
5. God sent me to proclaim to the Israelites
that He is one and ONLY (Mark 12:29 and
John 17:3)
6. God sent me to tell the Israelites that He is
the ONLY one to be served and worshipped
(Matthew 4:10, Mark 12:30)
7. God didn't send me as a God to be served
and worshipped but to serve and worship Him
only. (Matthew 20:28)
8. ANYBODY who worship me, is wasting his/
her precious critical time. (Matthew 15:9)
9. I never ever claimed to be God because I
have God to whom I cried and prayed (Matthew
Matthew 26:39)
10. I can't do ANYTHING on my own. I do only
what God commands me to do. (John 5:19, 30)
If, still with what Jesus said about himself
above, someone continues to say Jesus is God,
then there are at least TWO Gods. Jesus and
the God he cried and prayed to in Matthew
John 11:35 and Matthew 26:39!
And if that's true, then Jesus must be lying in.
And everyone knows that Jesus never lied about himself. Be he said he was sent
John 17:3 because he said God is one and
only.
(18:29) sΕ«rat l-kahf (The Cave)
: And say, "The truth is from your Lord, so whoever wills - let him believe; and whoever wills - let him disbelieve." Indeed, We have prepared for the wrongdoers a fire whose walls will surround them. And if they call for relief, they will be relieved with water like murky oil, which scalds [their] faces. Wretched is the drink, and evil is the resting place.
And [beware the Day] when Allah will say, "O Jesus, Son of Mary, did you say to the people, 'Take me and my mother as deities besides Allah ?'" He will say, "Exalted are You! It was not for me to say that to which I have no right. If I had said it, You would have known it.

PASTOR KASINA AHEPA MADA NA KULA KICHAPO UKUNDA K**A KAWAIDA
27/02/2026

PASTOR KASINA AHEPA MADA NA KULA KICHAPO UKUNDA K**A KAWAIDA

JE HIVI NDIVYO YESU ALIFUNDISHA NAMNA YA KUSUJUDU??? πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡ PASTOR KASINA HAJIELEWI KABISA 🀣🀣🀣🀣
26/02/2026

JE HIVI NDIVYO YESU ALIFUNDISHA NAMNA YA KUSUJUDU??? πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡ PASTOR KASINA HAJIELEWI KABISA 🀣🀣🀣🀣

PASTOR KASINA APATA KIPIGO CHA MAANDIKO UKUNDA
24/02/2026

PASTOR KASINA APATA KIPIGO CHA MAANDIKO UKUNDA

24/02/2026

Watch, follow, and discover more trending content.

DA'AWA UKUNDA DAY TWO
23/02/2026

DA'AWA UKUNDA DAY TWO

DA'AWA UKUNDA DAY ONE MAA SHAA ALLAH UJUMBE UMEFIKA
23/02/2026

DA'AWA UKUNDA DAY ONE MAA SHAA ALLAH UJUMBE UMEFIKA

Address

Kisauni~Bamburi Street Old Malindi Road Mtopanga Opposite Posta Behind Mewa Rehab
Mombasa
MOBI+254721818787

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Judai001 Da'awa Group posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Judai001 Da'awa Group:

Share