ACEPS/Sange Informations de contact, plan et itinéraire, formulaire de contact, heures d'ouverture, services, évaluations, photos, vidéos et annonces de ACEPS/Sange, Organisation à but non lucratif, Sange, Uvira.

Recevez
15/11/2021

Recevez

KARIBU TUJIFUNZE IMANI YA MSINGI WA KANISA LA MASALIO

MSINGI NAMBA 12/28 YA KANISA

12.

Utangulizi

Kanisa ni jumuiya ya waumini waliokubali kumkiri Yesu k**a mwokozi na Bwana wao. Kwa kuunganika na watu wa Mungu katika Agano la Kale, tumeitwa kutoka ulimwenguni na tunaungana pamoja kwa ibada, ushirika, kufundisha Neno, kusherehekea Meza ya Bwana, katika utumishi kwa wanadamu na katika kutangaza injili duniani kote. Kanisa hupokea mamlaka yake kutoka kwa Kristo ambaye ni Neno aliyefanyika mwili, na katika Maandiko Matakatifu, ambayo ni Neno lililoandikwa. Kanisa ni familia ya Mungu iliyotengenezwa kwa agano. Kanisa ni mwili wa Kristo, jumuia ya imani ambayo Kristo mwenyewe ndiye Kichwa (Kiongozi). Kanisa ni bibi arusi ambaye Kristo alimfia ili apate kumtakasa na kumsafisha. Katika kurudi kwake kwa ushindi, atajiwasilishia kwake mwenyewe likiwa kanisa tukufu, aminifu kwa vizazi vyote, kile ambacho damu yake ilikinunua, likiwa halina doa wala kunyanzi bali takatifu lisilo na waa. (Mw. 12:3, Mdo. 7:38, Efe. 4:11-15, 3:8-11, Mt.28:19,20; Mt 16:13-20; Mt 18:18; Efe. 2:19-22; Efe 1:22,23, Efe 5:23-27, Kol.1:17,18)

Maana ya Kanisa Kibiblia
Kwenye Biblia, neno la Kigiriki lililotafsiriwa kanisa ni ekklesia, likimaanisha kuitwa ili kuondoka/kutoka. Kitabu kiitwacho Septuagint yaani tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale iliyotumiwa nyakati za Yesu, hutafsiri neno la kiebrania qahal iliyomaanisha mkutano, kusanyiko, jamii. (Kumb.9:10, Kumb 18:16; 1Sam.17:47, 1Waf.8:14, 1Nya.13:2). Matumizi ya maana ya kanisa yalipanuka kwenye Agano Jipya ambako maana zifuatazo zinaonekana: -

a) Waumini wanaokutana kuabudu katika mahali fulani maalum (1Kor. 11:18; 14:19, 28)
b) Waumini wanaoishi katika eneo mojawapo kijiografia (1Kor.16:1, Gal.1:2 1Thes.2:14)
c) Kundi la waumini katika nyumba ya mtu (1Kor.16:19, Kol.4:15, Filem. 2)
d) Makundi ya Makusanyiko ya waumini kwenye eneo mojawapo kijiografia (Mdo. 9:31)
e) Kundi linalojumuisha waumini wote ulimwenguni (Mt.16:18; 1Kor.10:32; 12:28; cf. Efe. 4:11-16)
f) Jamii ya waumini waaminifu wote ulimwenguni – duniani na mbinguni (Efe. 1:20-22; Filip. 2:9-11)

Chimbuko la Kanisa

Biblia hulionyesha kanisa kuwa ni taasisi ya kimbingu, ikiliita Kanisa la Mungu (Mdo.20:28), 1Kor.1:2). Yesu aliwekeza mamlaka yake ndani ya Kanisa (Mt. 18:17,18). Twaweza kutambua miz**i ya Kanisa katika Agano la Kale na vielelezo vya Agano Jipya.

Miz**i ya Kanisa

Agano la Kale linadhihirisha kwamba kanisa ni kundi lenye mpangilio la watu wa Mungu. Tangu awali familia zenye kumcha Mungu tangu Adamu, Seti, Nuhu, Shemu na Ibrahimu ziliutunza ukweli. Mungu alitoa ahadi nzito na hatimaye hii nyumba ya Mungu ilikuwa taifa: na jamaa zote zote za dunia watabarikiwa (Mwa. 12:1-3)

Taifa alilolitoa Misri liliitwa Kanisa llililokuwa Jangwani (Mdo. 7:38). Washiriki wake wa Kanisa walitambulika ‘ufalme wa makuhani na taifa takatifu (Kut.19:6), Watakatifu wa Mungu (Kumb.28:9 c/f Law.26:12), Kanisa lake. Aliwaweka Palestina, mahali ambako mabara matatu ya Afrika, Ulaya na Asia hukutana lengo likiwa kuwaita wote waingie (Isa.56:7). Pamoja na uangalizi wa Mungu, Israeli waliendelea kuabudu miungu mingine, kujitenga kiubaguzi, utaifa, kiburi na kujiangalia wenyewe, wakashindwa kutimiza makusudi ya Mungu.

Katika siku za Yesu, Israeli walipata upendeleo wa kufikiwa na Masihi aliyetarajiwa kuwafungua kwenye utumwa wa kujitumainia nafsi. Kwa kumsulibisha Yesu, ilidhihirika jinsi Israeli walivyooza ndani yao. Walipopaza sauti hatuna mfalme ila Kaisari (Yoh. 19:15), walikataa Mungu asitawale juu yao. Kwa kushindwa Israeli, Mungu alianzisha taifa jingine, kanisa jingine, ambalo lingetimiza makusudi yake. (Mt. 21:41,43).

Kanisa katika Agano jipya linaundwa na Wayahudi waumini na watu wa Mataifa mengine (Gal.3:26-29). Wayahudi wasiomwamini Yesu siyo watoto wa Mungu tena (Rum.9:6-8). Mataifa wanaomkubali Mungu wanafananishwa na mzabibu mwitu ulipandikizwa kwenye mzabibu mwema (Rum.11:17-25). Matawi yanaonywa kushik**ana na Mungu wasije wakakatiliwa mbali (Rum.11:16-18). Tofauti na Kanisa kwenye Agano la Kale, Kanisa la Agano Jipya halijifungamanishwi na taifa moja, bali limepangiliwa kuwa la Ulimwengu mzima (Mt.28:19)

Vielelezo vya Agano Jipya Kuhusu Kanisa

1. Kanisa k**a Mwili:
Kanisa k**a mwili ni kielelezo kinachosisitiza umoja wa Kanisa na mahusiano baina ya washiriki. Msalaba huwapatanisha waumini katika mwili moja (Efe. 2:16). Kwa njia ya Roho Mtakatifu hubatizwa katika mwili moja (1Kor.12:13). Mwili unaosemwa hapa ni wa Yesu Kristo (Efe.1:22, 23). Washiriki ni viungo kwenye mwili wa Kristo (Efe.5:30). Kristo ndiye huhuisha mwili wake. Yeye ndiye kichwa (Kol.1:18) kiongozi wa Kanisa (Efe.5:23.)

2. Kanisa k**a Hekalu:
Kanisa ni hekalu, maskani ambako Roho Mtakatifu hukaa. (1Kor.3:9-16, Efe.2:20). Hekalu hili liko hai, kwa kuwa Kristo ni jiwe lililo hai na washiriki mawe yaliyo hai ambayo hufanya nyumba hai. (1Pet.2:4-6). Hekalu halijakamilika, linaendelea kujengwa (Efe.2:22) na zana bora zatakiwa kulijenga ili listahimili majaribu hata hukumu (1Kor.3:12-15). Kielelezo cha hekalu husisitiza utakatifu kwa kuwa atayeliharibu ataharibiwa (1Kor.3:17). Hakuna ushirika baina ya Kristo na Beliari (2Kor. 6:14, 16).

3. Kanisa k**a Bibi Arusi:
Kanisa husemwa kuwa Bibi Arusi wa Bwana Harusi Yesu Kristo. Bwana asema nitakuposa uwe wangu milele (Hosea 2:19), …mimi ni mume wenu (Yer.3:14). Paulo anarudia kielelezo hiki kwa kusema nalimposea Kristo bikira safi (Kol. 1:18, 22-23). Upendo wa Kristo kwa kanisa ni mkubwa kwani alilazimika kufa kwa ajili yake(Efe.5:25) na kwa kafara yake kulisafisha (Efe.5:26) ni sala yake litakaswe kwa neno (Yoh.17:17) ili hatimaye liwe safi na lisilo na mawaa (Efe.5:27).

4. Kanisa k**a Yerusalemu iliyo juu:
Biblia huita jiji la Yerusalemu Sayuni. Humo, Bwana anakaa na watu wake (Zab.9:11), na wokovu hutokea (Zab.14:7, 53:6). Ni furaha ya dunia yote (Zab.48:2). Agano jipya hutambua jiji la Yerusalemu la juu mbinguni (Gal.4:26) na wakazi wa Yerusalemu hiyo wana makazi na uraia wa mbinguni (Wafil. 3:20). Wakazi ni wana wa ahadi, waliozaliwa kwa roho (Gal.4:28, 29; 5:1), hawajitahidi kuhesabiwa haki kwa matendo ya sharia (Gal.4:22,26,31; Gal 5:4) bali kwa imani. Wanatambua kwamba imani itendayo kwa upendo ndiyo huwapa uraia (Gal. 5:5, 6). Waliofika hapo, wako kwenye maskani ya Mungu yenye malaika maelfu na majina yao yameandikwa kuwa ni wenyeji (Ebr.12:22, 23).

5. Kanisa k**a Familia:
Kanisa lililoko mbinguni na duniani huzingatiwa kuwa ni familia (Efe.3:15). Kujiunga na familia hii hutokana na kuzaliwa upya (Yoh.3:8) au kwa kuasiliwa (Rum. 8:14-16, Efe.1:4-6). Kwa njia ya imani katika Kristo na ubatizo, hawatakuwa watumwa tena bali wana wa Baba (Gal.3:26-4:7). Ni wa nyumba ya Mungu (Efe.2:19) na jamaa ya waaminio (Gal.6:10). Washiriki wa familia humwita Mungu ‘Baba’ (Gal.4:6) na hujitambua kuwa ndugu – kaka na dada (Yak.2:15, 1Kor.8:11, Rum.16:1). Ni kweli kutokana na huduma yake, Paulo alileta wengi kwa Kristo hata akasema yeye ni baba yao (1Kor.4:15) aliowahubiria watoto wake (1Kor.4:4, Efe.5:1) hata hivyo, kawaida ya msingi ya kanisa ni kujumuika kwa ushirika (fellowship) katika injili (Wafil. 1:5), kwa kujumuika na Baba, Mwana na Roho Mtakatifu (1Yoh.1:3, 1Kor. 1:9; 2Kor.13:14) pamoja na washiriki wengine (1Yoh.1:3, 7). Mfano wa Kanisa k**a familia hukazia wajibu wa kupendana, kuthaminiana na mahali ambako watu huhitajiana na talanta hukuzwa. Washiriki wanaotofautiana bado waweza kupeana misaada.

6. Kanisa k**a Nguzo na Msingi wa Ukweli:
Kanisa la Mungu ni nguzo na msingi wa ukweli (1Tim.3:15). Hulinda ukweli kutokana na mashambulizi ya adui. Kukitokea fundisho jipya, lapaswa kulinganishwa na maandiko (Isa.8:20). Washiriki wote wapaswa kukubaliana na uamuzi uliosimama katika Biblia kwa kuwa kwa washauri, huja wokovu. (Mith.11:14). Kupitia huduma yake, kanisa huwa chumvi na nuru ya dunia (Mat.5:13-15).

7. Kanisa k**a Jeshi: linalo pambana na lililoshinda
Kanisa ni jeshi linalopambana na giza “Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”(Efe.6:12). Wakristo wapaswa ikuvaa silaha ili waweze kushindana siku ya uovu itakapokuja na wakiisha kufanya yote, kusimama. (Efe.6:13). Maadui wako ndani nan je (Mdo.20:29,30; 1Tim.4:2). Pamoja na kuwapo vitani, bado kanisa lina kasoro zisizo ndogo, ndani yake alikuja adui akapanda magugu akaenda zake (Mt.13:24, 25) na hivyo kuna magugu na ngano yanayoendelea kukua pamoja (Mt.13:29, 30). Vita ya adui wa nje haijakoma, kwa kuwa shetani anaendelea kusumbua (Uf.12:12, 17). Hata hivyo Kristo ataingilia kati na kuokoa kila aliyeandikwa kwenye kitabu chake (Dan.12:1). Yesu amehakikisha kwamba atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka (Mt.24:13). Kristo atakaporejea mara ya pili Kanisa lililoshinda litatokea “kwa kuwa atajiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lo lote, bali takatifu lisilo na hatia” (Efe.5:27)

Muundo na Majukumu ya Kanisa

Kanisa linaloonekana na Kanisa lisiloonekana
Maneno ya linaloonekana na lisiloonekana hutumika kutofautisha hali mbili za kanisa juu ya dunia. Vielelezo vilivyotumika, huzungumzia kanisa linaloonekana.

Kanisa linaloonekana
Kanisa linaloonekana ni kanisa la Mungu lililojipanga kwa ajili ya huduma. Hutimiza agizo la Yesu la kupeleka injili kwa kila kiumbe (Mt. 28:18-20) na hutayarisha watu kwa ujio wa Yesu wa utukufu (Efe.5:27). Mashahidi wa kweli wa Yesu watafanya k**a yeye alivyofanya “‘Roho wa Bwana yu juu Yangu, kwa sababu amenitia mafuta kuwaletea maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru wanaoonewa na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika.” Luka 4:18,19)

Kanisa lisiloonekana
Kanisa lisiloonekana vile vile hujulikana k**a kanisa la ulimwengu wote, huundwa na watu wote wa Mungu kwenye ulimwengu wote, likijumuisha washiriki walioko kwenye kanisa linaloonekana na wengine wengi ambao wameifuata kwa uaminifu nuru waliyopokea (1Yoh.1:9). Hapa liko kundi ambalo halikupata kusikia habari za Yesu bali ndani ya mioyo yao, wakiongozwa na Roho Mtakatifu, wanatii maagizo ya torati (Rum.2:14). Kuwepo kwa kanisa lisiloonekana kunadhihirisha kwamba Mungu huabudiwa katika roho na kweli (Yoh.4:23). Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Mungu huongoza washiriki wa Kanisa lisiloonekana waingie katika Kanisa linaloonekana. “Ninao kondoo wengine ambao si wa z**i hili, inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu, hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja.” (Yoh.10:16). Ni katika kanisa linaloonekana tu, ndipo wanapoweza kupata utimilifu wa ukweli, upendo na ushirika (Efe.4:4-16). Paulo alipojiunga na Kanisa linaloonekana, alipewa kulihudumia (Mdo.9:10-22). Hivyo wanapojiunga, huungana kutimiza utume wa Kristo (Uf.14:12, 18:4, Mt. 24:14). Kanisa lisiloonekana vilevile limeunganisha kanisa la mbinguni na duniani (Efe.1:22, 23) na kanisa lililojificha wakati wa mateso (Uf.12:6, 14)

Muundo
Agizo la Yesu la kupeleka injili kwa ulimwengu wote, limejumuisha kuwatunza wale waliopokea neno. (Mt.28:18,19). Kwa kuwa Mungu siyo wa machafuko bali wa amani (1Kor.14:33), Kanisa linapaswa kuwa na muundo rahisi, lakini wenye kutosheleza.

Washiriki wa Kanisa:
Waongofu wakishakukamilisha sifa kadhaa, huwa washiriki wa jumuiya ya waumini. Ushiriki hujumuisha kukubali aina ya mahusiano baina ya watu wengine, Mamlaka ya Siasa (Serikali, Bunge na Mahak**a) pamoja na Mungu.

a) Sifa ya kuwa mshiriki:
Wanaotaka kuwa washiriki lazima wamkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wao, watubu dhambi na kubatizwa (Mdo.2:36-41 cf. 4:10-12). Wanapaswa kuzaliwa mara ya pili na kukubali agizo la Yesu la kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi (Yoh.3:3,5 na Mt. 28:18-20).

b) Usawa na Utumishi:
Kwa kuzingatia tangazo la Yesu, washiriki wote ni ndugu (Mt.23:8) na wanafursa ya kutumikiana (Mt.23:11). Mahusiano ya washiriki wao kwa wao yanapaswa kufuata kielelezo cha Yesu.

c) Ukuhani wa waumini wote:
Ukuhani wa Walawi ulikoma Yesu alipoanza ukuhani halisi mbinguni (Ebr.8 - 9). Sasa Kanisa limekuwa ukuhani wa kifalme (1Pet.2:5). “Lakini ninyi ni taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu la Mungu, mlioitwa ili kutangaza sifa Zake Yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru Yake ya ajabu.”(1Pet.2:9)

d) Utii kwa Mungu na kwa Serikali:
Biblia hutambua mkono wa Mungu kuhusika kuanzisha mamlaka za kiutawala wa kidunia na huwataka waumini kuziheshimu kwa kulipa kodi, hofu na heshima (Rum.13:4, 7). Katika mtazamo wao kwa mamlaka ya kitaifa, waumini huongozwa na kanuni ya Yesu, kwamba “Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu (Mt.22:21). Ikiwa Serikali itaamua kuingilia amri ya Mungu, mtume alisema “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu” (Mdo 5:29).

Majukumu Makuu ya Kanisa:
Kanisa liliundwa ili kuijulisha dunia utukufu wa Mungu. Ni kanisa linaloonekana tu, ndilo linaloweza kutimiziza jukumu hilo.

a) Ibada na kuhimizana:
Katika historia yote, kanisa ni chombo cha Mungu kukusanya waumini kwa ibada kwenye siku za sabato. “Wala tusiache kukutana pamoja, k**a wengine walivyo na desturi ya kukutana, tuhimizane sisi kwa sisi kadri tuonavyo siku ile inakaribia.” (Ebr.10:25 cf. 3:13)

b) Ushirikiano wa Kikristo:
Kwa njia ya Kanisa, mahitaji ya ushirikiano wa kikristo hukamilishwa. Kushiriki kueneza Injili (Wafil. 1:5) hupita mahusiano mengine yote kwani hutufanya tufahamiane sisi kwa sisi na pia tumjue Mungu.(1Yoh.1:3, 6, 7)

c) Kufundisha Maandiko:
Yesu alilipa Kanisa funguo za ufalme (Mt.16:19). Hizi funguo ni maarifa ya kuingia ufalme wa Mungu (Luk.11:52). Maneno ya Yesu ni roho na uzima kwa wanaoyapokea (Yoh.6:68). Yakihubiriwa, yana mamlaka ya kufunga na kufungua kadiri msikilizaji anavyopokea. Hivyo neno ni harufu ya mauti pia ni harufu nzuri iletayo uzima (2Kor.2:16). Yesu alijua umuhimu ya Neno litokalo kwenye kinywa cha Mungu (Mt.4:4) na ameagiza kwenda kulifundisha ili watu walishike (Mt.28:19,20)

d) Kusimamia uendeshaji wa desturi za Kanisa:
Kanisa ni nyenzo ya kuendesha huduma ya ubatizo na kumpokea mshiriki kanisani. (Mt.28:19, 20 cf. Mk.16:16) Pia, huendesha huduma ya kuoshana miguu pamoja na Meza ya Bwana (Yoh. 13:12-14, Luk. 22:17-20)

e) Kutangaza injili ulimwenguni pote:
Jukumu kubwa ambalo kanisa limepewa ni kuhubiri injili iwe ushuhuda (Mt.24:14) kwa kuwezeshwa na ubatizo wa Roho Mtakatifu. Injili yajumuisha kukumbushana kujiandaa na ujio wa Yesu ( 1Kor.1:7, 8; 2Pet.3:14; Uf.3:14-22; 14:5) na kwa wanadamu wengine (Uf.14:6-12; 18:4)

Uongozi wa Kanisa
Baada ya Yesu kupaa, uongozi wa Kanisa uliachwa kwenye mamlaka ya Mitume. Jambo lao la kwanza ilikuwa kumteua mtume mwingine kuchukua nafasi ya Yuda (Mdo.1:15-26). Kanisa lilipokuwa, ilikuwa vigumu kuhubiri neno na wakati huo huo kuhudumu mezani. Hivyo waliteua waumini wengine kuhudumu mezani (Mdo. 6:1-4). Mashemasi wawili kati ya saba, Stefano na Filipo walijulikana kwa uhodari wao kuhubiri (Mdo. 7 & 8). Kanisa lilipopanuka Asia na Ulaya, Wazee waliwekewa mikono kuongoza makanisa (Mdo. 14:23). Mgogoro mkubwa ulipoanza, umuhimu wa kuwa na halmashauri kuu ya kanisa ulionekana, misimamo ya pande zinazosigana ilizungumzwa na kuamuliwa (Mdo.15:1-29). Maamuzi yalifikiwa kwa uwakilishi wa pande zote zinazohusika (Mdo.15:22, 25). Hivyo kadiri ya mahitaji yalivyojitokeza, Mungu aliongoza kazi yake na Uongozi wa Kanisa ambao ukifutwa leo, utalinda kanisa kutokana na uasi na kuwezesha kutimiza jukumu lake kuu.

Kanuni za Biblia za Uongozi wa Kanisa
1. Kristo ni Mkuu wa Kanisa:
Uongozi wa Kristo unatokana na huduma yake ya upatanisho. Tangu alipomshinda Shetani msalabani, alipewa mamlaka mbinguni na duniani (Mt.28:18). Mungu ameweka yote chini ya miguu ya Yesu (Efe. 1:22, cf. Wafil. 2:10, 11). Na kwa hiyo Kristo ndiye Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme (Uf.17:14). Kristo pia ni kiongozi wa Kanisa kwa kuwa Kanisa ni mwili wake (Efe.1:23, Kol.1:18). Viungo vya mwili wake ndio washiriki wa Kanisa (Efe.5:30). Wanapaswa kuwa na muunganiko wa karibu kwa kuwa kutokana na Kristo, kanisa hulishwa na kufungamanishwa pamoja (Kol. 2:19).

2. Kristo ndiye chanzo cha mamlaka yote ya Kanisa:
Kristo amedhihirisha mamlaka yake kwa Kanisa kwa (a) kuanzisha kanisa (Mt. 16:18), (b) kuanzisha desturi ambazo kanisa lapaswa kuzisimamia (Mt.26:26-30, Mt. 28:19, 20; 1Kor.11:23-27; Yoh.13:1-17); (c) kuachia kanisa mamlaka ya kutumia Jina lake (Mt.16:19; Mt. 18:15-18 Yoh. 20:21-23) (d) Kulipatia Kanisa Roho Mtakatifu aliongoze (Yoh. 15:26; 16:13-15) (e) Kugawa karama ndani ya kanisa yaani mitume, waalimu, manabii na nyinginezo ili kuukamilisha mwili wake (Efe. 4:7-13)

3. Maandiko Matakatifu yana mamlaka ya Kristo:
Pamoja na Kristo kuongoza kanisa kwa Roho Mtakatifu, Maandiko Matakatifu ndicho kiwango pekee cha shughuli za Kanisa. Washiriki wanapaswa kuyatii Maandiko kwa kuwa ndiyo sheria katika uhalisi wake. Desturi, tamaduni, mapokeo yote ya kibinadamu yanapaswa kutiishwa kwa maandiko. (2Tim.3:15-17).

4. Mamlaka ya Kristo na Maofisa wa Kanisa:
Kristo hutumia mamlaka yake kupitia watumishi wake walioteuliwa, lakini kamwe hahamishii kwao mamlaka yake. Hakuna Ofisa wa Kanisa aliye na uhuru wa kutenda apendavyo zaidi ya Kristo na Neno lake.

Maofisa wa Kanisa katika Agano Jipya
Agano Jipya linataja vyeo viwili vya uongozi wa Kanisa – Wazee na Mashemasi. Sifa maalum za kimaadili na za kiroho zimetajwa kwa wanaopaswa kuchaguliwa kushika nafasi hizo. Kanisa linatambua utakatifu wa madaraka ya vyeo hivyo na ndiyo maana huwawekea mikono (Mdo. 6:6; Mdo 13:2, 3; 1Tim.4:14; 5:22)

Wazee wa Kanisa:
(a) Mzee ni nani?
Wazee, kwa kigiriki presbuteros au Maaskofu (episkopos) ndio maofisa wa ngazi ya juu wa Kanisa. Mzee ni kuwa na umri mkubwa ikimaanisha madaraka na heshima. Cheo cha Mzee wa Kanisa kinafananishwa na cha Msimamizi wa Sinagogi. Neno Askofu humaanisha msimamizi. Paulo hutumia Mzee au Askofu kwa kubadilishana akilinganisha wazee na wasimamizi au maaskofu. (Mdo. 20:17, 28; Tit. 1:5, 7). Wazee husimamia Makanisa. Kwa kuwa Mitume nao walijiita Wazee (1Pet. 5:1; 2Yoh.1; 3Yoh.1) hudokeza kwamba walikuwako Wazee wa Kanisa mahalia na wale wanaozuru makanisa kwa ratiba. Aina zote za wazee ni wachungaji wa makutano ya kikanisa.

(b) Sifa za Mzee:
Ili mtu apate sifa za kuwa Mzee lazima asiwe na lawama, mume wa mke moja, mwenye kiasi, tabia njema, ambaye hakuongoka karibuni asije akajikwaa (1Tim.3:1-7; cf. Tit. 1:5-9). Kabla ya kuchaguliwa, mtu anapaswa kuonyesha sifa za uongozi, kwa kusimamia nyumba yake mwenyewe (1Tim. 3:15). Kwa umuhimu wa madaraka ya Uzee, Paulo alionya wasiwekewe mikono upesi (1Tim.5:22).

(c)Majukumu na mamlaka ya Mzee:
Mzee ni kiongozi wa kiroho (Mdo. 20:28). Hujumuisha kuwasaidia walio wanyonge (Mdo. 20:35), akiwaonya wanaopotea (1Thes.5:12), na kuwa chonjo na mafundisho yanayoweza kusambaratisha kundi (20:29-31). Wazee wanapaswa kuishi maisha yanayoweza kuigwa na waumini wengine (Ebr. 13:7; 1Pet.5:3) na kuonyesha mfano wa ukarimu (Mdo. 20:35).

(d)Mtazamo wa waumini kwa Wazee:
Kwa kiwango kikubwa, uongozi wa kanisa hufanikiwa kutokana na utii wa washiriki kwa viongozi. Hivyo waumini wameitwa kuwapa heshima (1Thes. 5:12). Watiini wale ambao wanajitaabisha kwa ajili yenu (Ebr. 13:17 cf. 1Pet.5:5). Wanahimizwa kufuata mwenendo wa kikristo wa viongozi wao (Ebr. 13:7), wakiepuka masengenyo “usikubali mashtaka dhidi ya Mzee ila kwa mashahidi wawili au watatu” (1Tim. 5:19)

Mashemasi wa Kiume na wa K**e:
Neno shemasi kwa kigiriki diakonos humaanisha mtumishi au msaidizi. Mashemasi waliwekwa kusaidia ili mitume wadumu katika sala na huduma ya neno (Mdo. 6:4). Ingawa mashemasi waliwekwa kuangalia ustawi wa washiriki, hawakubaki nyuma kupeleka injili (Mdo. 6:8; 8:5-13, 26-40). Shemasi wa k**e anasomeka kwenye Rumi 6:1. K**a walivyo Wazee, Mashemasi nao huchaguliwa kwa kufaa kwao kwa maadili na kiroho (1Tim.3:8-13).

Nidhamu ya Kanisa
Kristo alilipa Kanisa mamlaka ya kusimamia nidhamu. Anatarajia Kanisa kutekeleza misingi ya nidhamu inapobidi ili kudumisha wito mtwa ukuhani wa kifalme na taifa takatifu (Mt.18:15-18; 1Pet. 2:5, 9). Kanisa linawajibika kushughulikia washiriki wake wanaoasi. Kristo analisifu kanisa la Efeso kwa kutochukuliana na wabaya (Uf. 2:2), anayakemea makanisa ya Pergamo na Thiatira kwa kuvumilia uzushi na zinaa (Uf. 2:14, 15, 20).

Kushughulika na makosa binafsi
Mtu moja akimkosea mwenzake, (Mt. 18:15-17), Kristo anashauri aliyekosewa, kumwendea aliyekosa na kushauriana naye abadilike tabia. Akishindwa kuelewana baada ya mashahidi, Kanisa hujulishwa ili kuliangalia jambo husika. Litakalofungwa au kufunguliwa na Kanisa, hukubalika mbinguni (Mt. 18:18).

Kushughulika na makosa ya wazi
Pamoja na kwamba wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Rum. 3:23) makosa ya wazi na uasi huliabisha kanisa. Kumwondoa mtu kwenye ushirika huondoa chachu ambayo ingeharibu vyote. (1Kor.5:4, 5, 7) Msichangamane na mzinzi, mwenye kutamani, mwenye kuabudu sanamu, mtukanaji mlevi au mnyang’anyi. Mwondoeni aliye mbaya miongoni mwenu. (1Kor.5:11,13)

Kushughulika na anayejitenga:
Wanaojitenga kwa kufanya fitina na kujikwaza wapaswa kuepukwa (Rum. 16:17). Jitengeni nao, jihadharini msimhesabu kuwa adui ila mwonyeni k**a ndugu (2Thes. 3:6, 14, 15). Anayeonywa na kuendelea na msimamo wake hukataliwa (Tit. 3:10, 11).

Kurejesha wakosaji wanaotubu:
Kanisa halipaswi kuwadharau, kuwapuuza au kuwasusia waliotengwa. Juhudi yapaswa kufanywa ili kuwarejesha.(2Kor.2:6-10). Ni katika kuwarejesha wadhambi ndipo uwezo, utukufu na rehema za Mungu hudhihirika. Kwa sasa Kristo kwa njia ya Kanisa anaalika kila mtu aje apate kuwa mwanafamilia (Uf. 3:20).

Mungu akubariki UNAPOFATILIA

Adresse

Sange
Uvira

Téléphone

+243818586145

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque ACEPS/Sange publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Contacter L’organisation

Envoyer un message à ACEPS/Sange:

Partager