23/11/2025
Naitwa Ezekiel John Mollel (25), mkazi wa Kigamboni, DSM. Mnamo tar 25/1/2025, saa 3 usiku nikiwa natoka kibaruani, nilichukua bodaboda maeneo ya Feri ili inifikishe nyumbani. Bahati mbaya tulipata ajali ambapo wote wawili (dereva na abiria) tuliumia. Mimi nilivunjika mfupa wa mguu wa kushoto (fibula na tibia). Nilikimbizwa hospitali ya Wilaya kwa matibabu lakini nikapewa rufaa kwenda MOI. Nilifanyiwa upasuaji na kuwekewa chuma kwa ndani.
Hata hivyo, mguu haukupona. Nilipata maambukizi ndani ya mfupa. Kidonda kilibaki kibichi na kutoa usaha. Nikalazimika kurudi MOI ambapo nilirudia upasuaji na kuondolewa chuma kilichowekwa ndani, nikawekewa vifaa maalum (cement beads) ndani ya mfupa ili kutibu maambukizi yaliyokuwepo. Pia niliwekewa kifaa cha nje (external fixator). Namshukuru Mungu matibabu hayo yamenisaidia kwani mguu uliacha kutoa usaha na maumivu yakapungua.
Tar 15/11/2025 nilifanyiwa X-Ray, na ikaonesha kuwa kidonda kinaendelea vizuri. Tar 24 Novemba 2025 natakiwa kufanyiwa tena upasuaji wa kuondoa “cement beads” nilizowekewa kwa ajili ya kutibu infections. Upasuaji huo pia unahitaji kuwekewa mifupa bandia (artificial bone graft) katika eneo la mfupa ulioondolewa kwa kuoza kutokana na infection.
Gharama za jumla zinazohitajika ni takribani TZS 2M lakini kwa bahati mbaya hali yangu kiuchumi kwa sasa ni ngumu sana. Kwenye kiwanda (kwa wahindi) nilipokuwa nafanya kazi nilikua kibarua, sikua na mkataba wa ajira. Kwa hiyo sikupata msaada wowote kutoka kwa mwajiri. Kwa kipindi chote cha kujiuguza nimetumia akiba yangu yote pamoja na kusaidiwa na ndugu na marafiki.
Kwa unyenyekevu naomba msaada kwa Watanzania wenzangu ili niweze kusimama tena. Mimi ni baba wa familia na kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu nipate ajali tumepitia kipindi kigumu sana. Naomba msaada niweze kusimama tena na kujitegemea. Natanguliza shukurani.
Ikiwa umeguswa kumsaidia Ezekiel, tuma sadaka yako kupitia M-PESA: 0752581983 Tigo Pesa: 0719744954 CRDB: 0150633516500 NMB: 24110012109 Gifted H