Neema ya Kristo ya tosha

Permanently closed.
11/04/2026

VITU 5 VINAVYOWEZA KUKUFANYA UKAFANIKIWA KIMAISHA.

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

◼️Kuna vitu vingi vinaweza kukufanya ukafanikiwa kiroho na kimwili.

3 Yohana 1:2 "Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, k**a vile roho yako ifanikiwavyo."

◾vitu 5 kati ya vingi vinavyoweza kukufanya ufanikiwe kimaisha ni hivi;

1. Karama.

Karama ni nini?

◼️Karama ni zawadi za Neema ambazo ROHO MTAKATIFU anakupa baada ya wewe kumpokea YESU KRISTO ili umtumikie MUNGU.

◼️Karama ni kipaji cha ROHO MTAKATIFU anachopewa mtu na ROHO MTAKATIFU.

➡️K**a una karama usiache kuitumia karama yako maana wakati Mwingine mafanikio Yako yanaweza kuambatana na karama Yako.

1 Petro 4:10-11 ''kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; k**a mawakili wema wa neema mbalimbali za MUNGU. Mtu akisema, na aseme k**a mausia ya MUNGU; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na MUNGU; ili MUNGU atukuzwe katika mambo yote kwa YESU KRISTO. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina. ''

◼️Karama inaweza kukufanya ukafanikiwa kiroho na kimwili.

➡️Ziko karama nyingi sana na inawezekana zingine unazo na wewe, itumie karama yako vyema na kwa utakatifu na utafanikiwa katika Maisha Yako.

◼️ Zingatia tu kuitumia karama yako kwa utakatifu na adabu kwa MUNGU wa Mbinguni.
◼️Tumia karama yako huku ukiishi Maisha Matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

2. Ujuzi.

Ujuzi ni nini?

◼️Ujuzi ni elimu inayotokana na kufundishwa.

Waefeso 1:7-9 " Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. NAYE ALITUZIDISHIA HIYO KATIKA HEKIMA YOTE NA UJUZI; akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo."

◼️K**a una ujuzi katika mambo fulani mema usiache kuutumia ujuzi wako maana ujuzi wako unaweza kukufanya ukafanikiwa kiroho na hata kimwili.

Je Wewe una ujuzi katika Nini?
Je ni katika biashara au kazi gani njema?

Unaweza kuutumia ujuzi wako na MUNGU akakupa kufanikiwa katika Maisha Yako.

Yako mambo mengi ya kimafanikio yanahitaji tu ujuzi.

◼️Utumie ujuzi wako katika mambo mema ya ki MUNGU na utafanikiwa kiroho na kimwili.

Danieli 1:17 "Basi, kwa habari za hao vijana wanne, MUNGU aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danielii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto."

Akina Danieli kwa ujuzi wao wa kutafasiri ndoto waliopewa na MUNGU uliwafanya hadi wakawa Viongozi katika Nchi ile.

◼️Usiwe k**a watu wake ambao huishia tu kusema "Mimi Nina ujuzi fulani" lakini yupo tu amekaa na ujuzi wake, Ndugu ni MUNGU alikupa huo ujuzi hivyo Fanya kazi kulingana na ujuzi wako na MUNGU atabariki Maisha Yako.

Kumbuka MUNGU katika mazingira mengine huwa anabariki kazi za Mikono Yako uliyeomba.

Kumbu 28:12 "Atakufunulia BWANA hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe."

➡️K**a huna hizo kazi za Mikono Yako uwe na uhakika hata ukiomba miaka MUNGU akubariki hatakubariki eneo hili linalohitaji kazi za Mikono Yako maana anasubiri kazi njema za Mikono Yako ili akubariki.

◼️ Hakikisha tu unatumia ujuzi wako kwa utakatifu na adabu mbele za MUNGU.
◼️Tumia ujuzi wako huku ukiishi Maisha Matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

3. Kipaji.

Kipaji ni nini?

◼️Kipaji ni kitu cha alichonacho mtu ambacho wengine hawana.

Mfano ni huu.
Kutoka 31:2-5 " Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; nami nimemjaza roho ya MUNGU, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote."

◼️Kipaji ni kitu cha rohoni kinachotenda kazi kimwili ambacho ni wewe unacho huku wengine hawana.
Kipaji ni baraka ya MUNGU hivyo sio Kila Mtu anacho kwa ajili ya kazi k**a Yako.

Nakumbuka Wakati mfupi baada ya Kuokoka nilitamani sana kujua kupiga kinanda Kanisani.
Nilichokifanya ni kumlipa pesa Mtumishi wa MUNGU Mmoja ili anifundishe na wenzake.
Mtumishi yule alifundisha lakini kwangu niliona darasa lile gumu sana,

nilijitahidi kuelewa ila sikuelewa lakini wenzangu ilikuwa kazi rahisi kwao, nikagundua MUNGU hakunipa kazi hiyo nikaacha na kuanza kufanya kazi zile ambazo kipaji changu kilionekana.

Mfano mmoja ni siku Moja Mtumishi mmoja anayesoma chuo Cha Biblia Ulaya Walipewa mada ya kiroho ili Kila mmoja aandike kitabu au aombe Watumishi anaowajua wamsaidie kuandika kitabu kile kulingana na mada waliopewa, ambapo vitabu vyao vitakuja kukusanywa na kutengenezwa vitabu vitakavyosaidia kuenea kwa Injili Afrika.

Mtumishi yule akaniomba nimsaidie.
Mimi nilitumia masaa 4 kuandika kitabu kizima Cha kiroho chenye maarifa mengi ya Biblia Kisha nikaenda stationary kukiandika Kisha siku hiyo hiyo nikamtumia.
Alishangaa uharaka ule, na kitabu kile sikuchukua maandishi kutoka kokote zaidi ya Biblia na Mimi mwenyewe huku ROHO MTAKATIFU akinisaidia na kunifundisha Nini Cha kuandika.
Hiyo nayo ni kipaji maana sio Kila Mtu anaweza.

Kipaji chako kinaweza kuwa chanzo cha kufanikiwa kwako kiroho na kimwili.

◼️ Ndugu Hakikisha tu kipaji chako hakikutoi kwa YESU KRISTO.

◼️Tumia kipaji chako kwa utakatifu na ucha MUNGU wa kweli.

Kitumie kipaji chako katika mambo mema yampendezayo MUNGU na utafanikiwa kiroho na kimwili.

4. Ubunifu.

Ubunifu ni nini?

◼️Ubunifu ni aina ya kufanya kitu ambacho wengine hawana.

Mithali 22:29 "Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo."

◼️Bidii na ubunifu unaweza kumfanya Mtu kusimama mbele ya watu wakuu na kufanikiwa katika Maisha Yake.

Mfano ni huu

1 Samweli 16:18 "Ndipo akajibu mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama, nimemwona mwana mmoja wa Yese, Mbethlehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena ni mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye BWANA yu pamoja naye."

◼️Kulikuwa na Wapiga vinubi wengi katika Israeli ila ubunifu wa Daudi katika kupiga Kinubi chake kilimfanya kuonekana na watu na baada ya muda mfupi habari zake zikafika Ikulu na hiyo ikapelekea kufanya kazi Ikulu.

Daudi akatoka kuwa Mchunga Kondoo na kwenda kufanya kazi Ikulu, na hiyo ilikuwa ni njia tu maana Baadae akawa mkuu wa Nchi kabisa.

◼️Ubunifu wako unaweza kukufanya ukafanikiwa sana kiroho na kimwili.

◼️ Hakikisha tu ubunifu wako unaufanya Ukiwa na ROHO MTAKATIFU huku ukiishi Maisha Matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO.

➡️Tafuta ubunifu mzuri na wa kitakatifu na utafanikiwa kiroho na kimwili.

Mambo hayo 5 ni ya muhimu sana katika kufanyia kazi wewe mteule wa MUNGU.

Inawezekana una kazi au biashara, hiyo inahitaji ubunifu au ujuzi ndipo utafanikiwa sana.

Inawezekana una mtaji au wewe una kipaji au karama, ukifanya kwa ubunifu na ujuzi mziri unaweza kufanikiwa kiroho na kimwili.

Fanya tu kwa haki, utakatifu nidhamu na maombi ya kina mbele za MUNGU.

5. Kufanya kazi halali inayokubalika mbele za MUNGU.

2 Wathesalonike 3:10-12 " Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula. Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine. Basi twawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana YESU KRISTO, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe."

◼️Ndugu usiye na kazi Tafuta kazi Fanya.

◼️Hakika tu fanya kazi huku ukiishi Maisha Matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO huku ukimtegemea MUNGU Kwa Maombi.

Labda tu k**a ni MUNGU amekukataza kufanya kazi fulani ili tu ufanye kazi yake iliyo katika kusudi lake hapo unaweza usifanye kazi na hutapungukiwa maana MUNGU ataagiza watu usiotarajia watakupa mahitaji Yako.
Mfano ni k**a Eliya na kunguru.

1 Wafalme 17:5-6 " Basi akaenda akafanya k**a alivyosema Bwana; kwa kuwa akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani. Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito."

◼️Lakini awe ni MUNGU amekuambia na sio vinginevyo.
K**a MUNGU hajakuambia usifanye kazi basi hata k**a Wewe ni Mchungaji unaweza kufanya kazi hata kwa masaa kadhaa ili pia upate muda wa kufanya kazi ya MUNGU katika KRISTO YESU.

Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma,

nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO k**a Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

Ubarikiwe.

11/02/2026

ZINAA HAITAKIWI KUWAKO KWA WATU WA MUNGU.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibu sana tujifunze Neno la MUNGU la uzima.

◼️Zinaa haitakiwi kuwapo kwa wateule wa MUNGU waliookolewa na YESU KRISTO Mwokozi.

2 Kor 6:18 '' Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.''

Zinaa ni nini?

➡️Zinaa ni tendo la uasherati au uzinzi.

✔️Uzinzi na uasherati ni tabia ya kuzini.

✔️Uzinzi na uasherati kwa jina lingine unaitwa ukware.

✔️Ukware ni tamaa ya kupenda kufanya tendo la kujamiana.

◼️Uzinzi na uasherati kwa jina lingine unaitwa uzinifu.

Katika Kanisa la MUNGU hakutakiwi kuwako wazinzi wala waasherati wala wakware wala wazinifu lakini leo kuna baadhi ya watu walio Kanisani ni wakware, wazinzi, waasherati na wazinifu.

◼️Uzinzi na uasherati ni moja ya dhambi kuu zilizowafanya Sodoma na Gomora kuchomwa moto.

Yuda 1:7 ''K**a vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.''

◼️Njia mojawapo ya mtu kuepuka zinaa ni kuoa au kuolewa na mtu huyo akawa mwaminifu kwa mwenzi wake wa Ndoa.

1 Kor 7:2 '' Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.''

Lakini wapo pia baadhi ya wanandoa sio waaminfu katika ndoa zao maana husaliti ndoa zao, hivyo hata kuwa ndani ya Ndoa hakujawasaidia kuacha zinaa hivyo jehanamu kuwangoja kwa spidi kali wasipopata neema ya kutubu na kuacha uzinzi.

◼️Kumbuka sku zote kwamba siku zote Mshahara wa dhambi zote zikiwemo dhambi za uzinzi na uasherati ni jehanamu.

Warumi 6:23 ''Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU Bwana wetu.''

◼️Biblia inakataza kila mtu kufanya uzinzi na uasherati.

Waefeso 5:3 '' Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, k**a iwastahilivyo watakatifu; ''

Wazinzi ni watu gani?

✔️Wazinzi ni watu waliooa au kuolewa wanapotoka kingono nje ya ndoa zao.

✔️Waasherati ni watu ambao hawajaoa au kuolewa wanapofanya ngono na mtu yeyote.

◼️Biblia inamtaka kila aliye Kanisa la MUNGU kuikimbia zinaa yaani kuukimbia uzinzi na uasherati.

2 Kor 6:18 '' Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.''

◼️Hivyo hakuna Mtu mwenye ruhusa ya kufanya uzinzi au uasherati.

Mama mmoja Mume wake kwa muda wa mwaka mmoja na nusu alikuwa anaumwa amepooza mwili, Mama huyu ni Mtumishi wa MUNGU kabisa lakini baada ya miezi kadhaa alisema neno la ajabu sana, alisema anahitaji kuhudumiwa kingono maana Mume wake hawezi tena kushiriki tendo la Ndoa, na aliyekuwa anamwambia hivyo ni Mtumishi mwingine na ana Mke na Watoto, yaani alitamani mara moja moja yule Mtumishi awe anaenda kuzini na Mama yule kwa sababu tu Mume wake hawezi tena, nilitamani kulia niliposikia kauli hiyo mbaya na chafu sana.

Baba mmoja alipoona Mke wake hazai aliamua kwenda kutafuta Mtoto nje ya Ndoa na huko akapata ukimwi ulioangamiza hadi Ndoa yake.

Baba mmoja kwenye ndoa yake alipata watoto wa kiume tu na yeye alitamani Mtoto wa k**e hata mmoja hivyo aliamua kwenda nje ya ndoa yake na huko aliangukia kwa wakala wa shetani ambaye alifanya hadi mipango ya kuua Mke na Watoto.

Inawezekana uko pia hapa unayetamani kufanya uzinzi kwa kigezo cha mwenzi wako anaumwa n.k

◼️Ndugu, ni dhambi kuisaliti ndoa yako.

K**a unaitaka mbingu huruhusiwi kuzaa nje ya Ndoa yako kwa kigezo kwamba mwenzi wako wa Ndoa hana uwezo wa kuzaa.

K**a unaitaka mbingu huruhusiwi kuoa Mke wa pili kwa sababu Mke wa kwanza kuna kitu unaona amepungukiwa.

Ndio maana kila mtu kabla ya kuoa au kuolewa huwa yuko makini sana maana mkifunga Ndoa ni huyo tu ndio wa kwako, mpende na madhaifu yake na heshimu Ndoa yako, ulimchagua mwenyewe kwa umakini mkubwa, ulimuona ni huyo tu miongoni mwa vijana au mabinti wengi hivyo ukaridhika kabisa kwamba ni huyo atakufaa kwa ajili ya Ndoa Takatifu ambayo huwa haitenganishi na chochote isipokuwa kifo.

Marko 10:7-9 ''Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
Basi alichokiunganisha MUNGU, mwanadamu asikitenganishe.''

◼️K**a unaitaka mbingu huruhusiwi kufanya mapenzi na mchumba wako kabla ya kufunga ndoa.

◼️K**a unaitaka mbingu huruhusiwi kufanya uzinzi na uasherati.

Inawezekana Kanisani kwenu sio wote wameikimbia zinaa ila wewe jitahidi kuikimbia dhambi hiyo.

Inawezekana katika familia yenu sio wote wameukimbia uzinzi na uasherati lakini wewe unayesoma ujumbe huu hakikisha unaukimbia uzinzi na uasherati.

Inawezekana sio wanandoa wengi unaowafahamu wamejitenga mbali na uzinzi lakini wewe jitenge mbali na dhambi hiyo.

Waebrania 13:4 ''Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. ''

Inawezekana kwenye ukoo wenu sio wote wameukimbia uzinzi na uasherati lakini wewe unayesoma ujumbe huu hakikisha unaikimbia dhambi hiyo inayonajisi mwili na roho.

Inawezekana sio marafiki zako unaowafahamu wamejitenga mbali na uzinzi au uasherati au ngono kinyume na maumbile lakini wewe hakikisha dhambi hizo chafu hazikuhusu.

Inawezekana katika mtaa wenu au katika eneo lako la kazi sio wote wamejitenga mbali na dhambi ya uzinifu lakini wewe unayesoma ujumbe huu nakuomba ikimbie dhambi hiyo.

◼️Jitenga na dhambi hizo ili uepukane na laana.

2 Petro 2:14 '' wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana; ''

Leo kuna hadi watumishi wa Kanisani ambao badala ya kuikimbia zinaa wao wameikaribisha na wanaiishi siku zote.

Leo kuna mpaka Wachungaji ni wazinzi,ni hatari sana sana.

Leo kuna mpaka wa Mama Wachungaji ni wazinzi, hiyo ni hatari sana na ni kujipoteza.

Leo mpaka kuna waimbaji au wahubiri ni wazinzi na waasherati kuliko hata makahaba.

Leo kuna mabinti ambao hawajaolewa wamekuwa waasherati na watoa mimba, ni mbaya sana na ni laana.

Inawezekana kabisa katika baadhi ya jamii za leo ni nadra sana kukutana na Binti ambaye hajatoa mimba, ni hatari sana na kutoa mimba ni kujitafutia laana maana chanzo kimoja wapo cha laana kibiblia ni kumwaga damu isiyo na hatia.

Mwanzo 4:10-12 ''Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.''

Sasa wanaotoa mimba wanaingia katika kundi lililolaaniwa maana wameua mtu asiye na hatia, katika jamii ya leo wapo wengi sana waliomwaga damu isiyo na hatia kwa sababu ya kutoa mimba. Na laana ni laana tu hivyo usipojua namna ya kuifuta laana hiyo ujue kuna maeneo mengi ya maisha yako yataathiriwa na laana hiyo.

Wapo watu hadi wametoa mimba zaidi ya mbili yaani ni laana iliyobeba laana na juu ya laana yenye laana.

Na laana ya kuua damu isiyo na hatia sio laana ya kuifuta tu kwa kusema ''Kwa imani naifuta laana ya kuua mtu asiye na hatia'' k**a ni hivyo tu tambua haifutiki.

Waone watumishi wa MUNGU wakusaidie na uwe na kiapo moyoni mwako kwamba hutatoa mimba tena.

Lakini kwanini ipelekee laana?
◼️Ni kwa sababu ya uzinzi na uasherati.

◼️Kumbe ukiepuka uzinzi na uasherati umeepuka madhara mengi sana kiroho na kimwili.

Uasherati na uzinzi unaweza kukuondolea haki zako kiroho na ukawa mtu wa majanga na mikosi na kuadhalaulika na vifungo vya giza, Mfano ni huu Ezekieli 23:29-30 '' nao watakutenda mambo kwa chuki, watakuondolea kazi zako zote, watakuacha uchi, huna nguo na aibu ya mambo yako ya kikahaba itafunuliwa, uasherati wako na uzinzi wako. Utatendwa mambo hayo kwa sababu umezini na hao wasioamini, na kwa sababu umetiwa unajisi kwa vinyago vyao.''

➡️Ndugu, hakikisha uzinzi na uasherati haupo kwako.

◼️Hakikisha unalitii Neno la MUNGU kuanzia leo kwa kuacha zinaa.

◼️Okoka na anza kuishi maisha matakatifu.

◼️Kumbuka zinaa inaweza kukufarakanisha na MUNGU na ukakosa hata mbingu au ukakosa baraka zako.

Hosea 5:4 ''Matendo yao hayatawaacha kumgeukia Mungu wao; maana roho ya uzinzi imo ndani yao, wala hawamjui BWANA.''

Inawezekana wewe una mchumba na akili yako inakutuma kwamba kwa sababu huyo mtaoana hivyo hata mkizini sio tatizo sana, ndugu kuzini ni dhambi na dhambi hiyo itatengeneza matatizo makubwa sana hivyo acha uzinzi na uasherati.

Kwanza uzinzi na uasherati ni sehemu ya ibada ya sanamu.

Wakolosai 3:5-6 '' Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya MUNGU.''

Je hufanyi ibada ya sanamu wewe?
Kwa sababu ya uzinzi au uasherati?

Ndugu, zinaa haitakiwi kuwako katika watu wa MUNGU.

◼️Uwe ni mwanaume au mwanamke hakikisha unajitenga mbali na dhambi ya uzinzi na uasherati.

"Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. -Ufunuo 2:11''

Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO k**a Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima

Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

02/02/2026

TUPATE WAPI MTU MWENYE ROHO WA MUNGU?

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

Tupate wapi MTU mwenye Roho wa MUNGU?

Mwanzo 41:38 "Farao akawaambia watumwa wake, TUPATE WAPI MTU K**A HUYU, MWENYE ROHO YA MUNGU NDANI YAKE?"

◼️Swali hili alijiuliza Siku Moja Farao baada ya kukosa kabisa Mtu mwenye ROHO wa MUNGU katika Taifa la Misri hadi alipotokea Yusufu.

Zamani kabla ROHO MTAKATIFU haijaanza kufanya kazi na watu walio na KRISTO ilikuwa vigumu sana kumpata Mtu mwenye ROHO wa MUNGU ingawa walikuwepo wachache na aliowapa Neema yeye.

◼️Leo watu wenye ROHO wa MUNGU ni wengi maana ni wakati wa ROHO MTAKATIFU.

Yohana 14:26 "Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye BABA atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia."

✓✓Zamani za akina Yusufu kwa sababu taifa Zima la Misri walikuwa wanaabudu miungu ni Yusufu Pekee aliyekuwa na ROHO wa MUNGU.
Kuabudu miungu kunaweza kumuondoa ROHO MTAKATIFU kwa Mtu

◼️Ukiwa na ROHO MTAKATIFU ujue kibali Cha MUNGU kitakuwa juu Yako ndio maana tunaona baadhi ya Sheria za kiungozi katika taifa la Misri akizileta Yusufu.

Mwanzo 47:26 "Yusufu akaifanya sheria kwa habari ya nchi ya Misri hata leo, ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao."

◼️Watu wenye ROHO MTAKATIFU ni watu wa Muhimu sana kwa watu wote na wamebeba misaada mingi ya kiroho kwa watu wengi.

Kuna faida kubwa nyingi za kuwa na ROHO MTAKATIFU, baadhi ni hizi

1. Paulo akijaa ROHO MTAKATIFU alimjua Mchawi Elima na akamzuia kuwaroga watu.

Matendo 13:8-11" Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa ROHO MTAKATIFU, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za BWANA zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa BWANA u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza."

✓✓ROHO MTAKATIFU anaweza akukupa kulijua jambo kiroho ambalo kwa macho ya kimwili usingelijua.

2. Stefano akijaa ROHO MTAKATIFU alipaona Mbinguni na aliuona utukufu wa MUNGU na Stefano pia alikuwa akifanya Miujiza

Matendo 7:55 "Lakini yeye akijaa ROHO MTAKATIFU, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa MUNGU, na YESU akisimama upande wa mkono wa kuume wa MUNGU."

✓✓ROHO MTAKATIFU anaweza kukupa kuona mambo makubwa ambayo hukuwa unayajua.

✓✓Ukiwa na ROHO MTAKATIFU ni rahisi kufanya Miujiza ya ki MUNGU.

3. Petro akijaa ROHO MTAKATIFU alihubiri watu wengi wakaokoka.

Matendo 4:8 "Ndipo Petro, akijaa ROHO MTAKATIFU, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,"

✓✓ROHO MTAKATIFU anatupa ujasiri wa kufanya kazi ya MUNGU ambapo bila ROHO MTAKATIFU tusingeweza.

✔️✔️Wewe Mhubiri mhitaji sana ROHO MTAKATIFU.

✔️✔️Wewe mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi unamhitaji sana ROHO MTAKATIFU ili ufanye kazi ya MUNGU katika KRISTO YESU.

✔️✔️Wewe muimbaji wa nyimbo za Injili unamhitaji sana ROHO MTAKATIFU ili ufanye kazi ya MUNGU inayoishi.

4. Yusufu akiwa na ROHO MTAKATIFU alitafasiri ndoto.

Mwanzo 41:25 "Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; MUNGU amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu."

✓✓ROHO MTAKATIFU anayo maarifa ya ki MUNGU ambayo Ukiwa naye anaweza kukupa.

Ndugu mhitaji sana ROHO MTAKATIFU ili siku Moja watu waseme "TUPATE WAPI TENA MTU K**A HUYU MWENYE ROHO WA MUNGU?"

Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO k**a Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

Barikiwa.

24/12/2025

MWANZO WA SIKUKUU YA CHRISTMAS

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu zangu wote.
Tunapoelekea kusherekea sikukuu ya Christmas naomba pia nijibu swali hili ambalo rafiki yangu mmoja aliniuliza December 2023.

◼️Ni swali kuhusu Mwanzo wa sikukuu ya Christmas.

Christmas ninatokana na neno la kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani Misa au Ibada ya KRISTO. Wengine Christmas huita Noeli, ni sawa kabisa

Noeli inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokewa kutoka Lugha ya Kifaransa "noël". Hilo ni ufupisho wa Kilatini "Natalis " yaani (siku ya) kuzaliwa".

◼️Kuhusu tarehe ya kuadhimisha sikukuu ya Christmas ni kwamba
tarehe hiyo iliwekwa na Viongozi wa Kanisa Karne za Mwanzoni ili kuwahamisha watu kutoka kuabudu miungu tarehe 25 December na Sasa kwa tarehe hiyo hiyo waitumie kumtukuza MUNGU wa Mbinguni aliyejifunua Pekee katika KRISTO YESU Mwokozi wetu.

✓✓Narudia Tena ni kwamba tarehe 25 December ya Christmas ni tarehe ya kubuni ili kuhamisha watu wasiitumie siku hiyo ya December 25 kuabudu miungu kwani katika utawala wa Rumi wakati ule ambao ulikuwa utawala mkuu duniani, kulikuwa na maagizo ya kiserikali watu kuabudu miungu ambao waliita mungu Jua, na dola nzima ya Rumi walikuwa wanaitumia siku hiyo kufanya Ibada za shetani kwa agizo la serikali ya kirumi hivyo Kanisa wakaona waivunje nguvu siku hiyo kwa kuihamisha kuwa siku ya kuzaliwa kwa YESU na baada ya miaka michache baadae Watu hata wasiomcha MUNGU wakaacha kuabudu miungu katika siku hiyo na kuanza kuitumia siku hiyo kwa utukufu wa MUNGU katika KRISTO.

Ingawa kwa baadhi ya maeneo hata leo shetani amepanda uongo mwingi wa watu kufanya maovu mengi katika siku hii

Ukisoms Warumi 14:5-6 sio kosa kuadhimisha siku yeyote k**a ni unaiadhimisha kwa MUNGU na unampa utukufu yeye, Biblia inasema ''Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa BWANA; naye alaye, hula kwa BWANA, kwa maana amshukuru MUNGU; tena asiyekula, hali kwa BWANA, naye pia amshukuru MUNGU.''

◼️K**a ulikuwa hujui ni kwamba Wakati Bwana YESU anazaliwa katika Utamaduni wa Wayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa. Ndio maana haikutunzwa siku kamili ya kuzaliwa Bwana YESU, baada ya hapo Ukristo ulienea katika Dola la Rumi ambako huko ni kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake KRISTO.
Ndiyo asili ya sikukuu ya Krismasi ingawa walishindwa kujua tarehe halisi ya kuzaliwa Bwana YESU

Baadae Kuanzia mwaka 200 AD (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus) wataalamu nchini Misri waliona tarehe 14 Nisan ya kalenda ya Kiyahudi ambayo ni sawa na 25 Machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake KRISTO na pia siku ya utungaji mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba k**a tarehe ya kuzaliwa, haya ni makadirio tu ya watu hawa, ingawa lengo lao ipatikane siku ya kuzaliwa Bwana YESU, sikubaliani nao maana Biblia haisemi tarehe ya kutungwa mimba Bwana YESU, hata Maria Mariamu alijikuta tu yuko Mimba sijui ni muda gani baada ya kupewa taarifa na Malaika.

Chanzo kingine cha Kanisa kupachika sikukuu ya Christmas kwenye tarehe hiyo ni kwa nia ya kufanya ichukue nafasi ya sikukuu ya miungu ambayo iliitwa sikukuu ya mungu jua "Sol invictus" (yaani "Jua lisiloshindika").

Wataalamu wa Biblia kwa kuwaaminisha watu walijaribu kuhususisha YESU na jua la haki kimaandiko Kuwa Jua ni ishara ya KRISTO; katika sehemu mbalimbali za Biblia KRISTO alifananishwa tayari na Jua wakitumia Mifano ya ni Luka 1:78, Ufunuo 21:23 na Malaki 4:2 hivyo katika mashindano na dini ya kuabudu Jua iliyokuwepo wakati ule Wakristo wao waliamua kutumia lugha ya Biblia kwa kudokeza KRISTO ndiye Jua la Haki hivyo waache ibada ya jua, Wamwabudu KRISTO kupitia sikukuu hiyo ya tarehe 25 iliyokuwa na Nguvu sana wakati ule.

Kanisa walifanikiwa kwa wakati ule ingawa baadae shetani aliingiza uongo katika sikukuu hiyo ili kuwahamisha baadhi ya watu katika kuitumia siku hiyo kumwabudu MUNGU aliye hai.

Maoni yangu Kanisa wakati ule walitaka tarehe 25 December iwe birthday ya YESU na hata Kanisa la leo baadhi ya maeneo maeneo kwenye ibada ya Christmas hufundisha kwamba "Leo ni Birthday ya YESU" haipaswi kuwa hivyo, hatuadhimishi Birthday bali tunakumbuka tukio la kuja kwa ukombozi wetu, sio Birthday ya YESU. Tunaitumia siku hiyo kuuambia ulimwengu wote kwamba YESU alikuja kwa ajili ya Wanadamu wote ndio maana nilianza na andiko la Warumi 14 la kuiadhimisha siku ila ni katika MUNGU tu.

✓✓Itumie siku hii kwa Bwana YESU KRISTO kwa utakatifu wote bila kuweka michanganyo ya kidunia.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

24/12/2025

KAZI 12 ZA DAMU YA YESU KRISTO.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

Kuna mamlaka nne za MUNGU kwa Mkristo ambazo mamlaka hizo humfanya Mkristo kuwa mshindi daima.
Mamlaka hizo ni Jina la YESU KRISTO, Nguvu za ROHO MTAKATIFU, Damu ya YESU KRISTO na Neno la MUNGU la ufunuo wa ROHO MTAKATIFU.

Leo nazungumzia Damu ya YESU KRISTO Katika kipengele kiitwacho Kazi za Damu ya YESU KRISTO.

Kwanza kabisa ni muhimu kila mtu kujua kwamba Damu ya YESU KRISTO ni kwa ajili ya Watu wote duniani, cha kufanya tu ni kumpokea YESU KRISTO k**a Mwokozi.

Ufunuo 5:9 "Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe(YESU) kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia MUNGU kwa DAMU yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,"

Damu ya YESU KRISTO ina kazi kubwa mno katika ulimwengu wa roho na matokeo ni makubwa sana katika ulimwengu wa mwili kwa Wateule wa MUNGU.

Wakolosai 1:19-20 " Kwa kuwa katika yeye(YESU) ilipendeza utimilifu wote ukae; na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa DAMU ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni."

Lengo la somo hili ni wewe uwe unaomba katika jina la YESU KRISTO huku ukitumia Damu ya YESU KRISTO ili uwe huru na uwe mshindi dhidi ya nguvu za giza.
Pia lengo la somo hili ujue kazi za damu ya YESU KRISTO maana hata ujasiri tu wa kupaingia patakatifu, huo ujasiri utakuwa nao ukiwa tu na Damu ya YESU KRISTO.
Waebrania 10:19 "Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa DAMU YA YESU,"

Kuna kazi nyingi za Damu ya YESU KRISTO kwa Mkristo aliye na YESU KRISTO na anajua kuomba maombi akitumia damu ya YESU KRISTO.

Hivyo ukiona Watu au dhehebu wanajitenga mbali na damu ya YESU KRISTO ujue upo mahali pasipo sahihi.
Waebrania 13:20 "Basi, MUNGU wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu YESU,"

Damu ya YESU KRISTO sio vitu vya duniani , hivyo mtu asikudanganye lakini damu ya YESU KRISTO ipo tayari kwenye ulimwengu wa roho kwa ajili yako.
Damu ya YESU KRISTO ni ya muhimu Sana maana hata Mbinguni watakatifu walioko huko ni wale tu waliosafishwa Kwa damu ya YESU KRISTO.
Ufunuo 7:14 "Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika DAMU YA Mwana-Kondoo(YESU KRISTO)."

Baadhi ya kazi za Damu ya YESU KRISTO.

1. Damu ya YESU KRISTO hutengeneza agano jipya kati ya MUNGU na Mwanadamu aliyemwamini KRISTO.

Marko 14:24 "Akawaambia, Hii ndiyo DAMU YANGU YA AGANO, imwagikayo kwa ajili ya wengi."

Agano maana yake ni patana au kupatana hivyo tunapatana na MUNGU muumbaji wetu kwa damu ya YESU KRISTO.
Kuna maagano ya kabla ya YESU KRISTO kuja duniani lakini ni MUNGU mwenyewe ndiye aliyezungumzia agano jipya ambalo atalileta.
Yeremia 31:31-33 " Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya AGANO JIPYA na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema BWANA. Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa MUNGU wao, nao watakuwa watu wangu."

Kwa hiyo ni kwamba kwa sasa sisi tuko katika agano jipya katika damu ya YESU KRISTO na hili agano jipya linaenda hadi kurudi kwa Bwana YESU mara ya pili.

2. Damu ya YESU KRISTO hufuta dhambi zote za mtu anayetubu kwa MUNGU katika KRISTO YESU.

Mathayo 26:28 "kwa maana hii ndiyo DAMU YANGU YA AGANO, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi."

Yaani Damu ya YESU KRISTO ina uwezo wa kulipa madeni yote ya dhambi ya Watu wote duniani wanaoamua kuokoka.

Ufunuo 1:5 "tena zitokazo kwa YESU KRISTO, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika DAMU YAKE,"

3. Damu ya YESU KRISTO huleta upatanisho kati ya Mwanadamu anayeokoka na MUNGU.

Warumi 3:25 "ambaye MUNGU amekwisha kumweka AWE UPATANISHO KWA NJIA YA IMANI KATIKA DAMU YAKE,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa."

MUNGU amemweka YESU KRISTO ili awe upatanisho kwetu kwa njia ya imani katika damu yake ya agano jipya.
Hivyo k**a unahitaji upatanisho ujue unaihitaji damu ya YESU KRISTO ya upatanisho.

Wakolosai 1:20 "na kwa yeye(YESU) kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa DAMU YA MSALABA WAKE; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.

4. Damu ya YESU KRISTO husafisha Dhamiri, nafsi na mioyo yetu.

Waebrania 9:13-14 " Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake KRISTO, ambaye kwamba kwa ROHO wa milele alijitoa nafsi yake kwa MUNGU kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu MUNGU aliye hai?"

Damu ya YESU KRISTO husafisha dhamiri.

Dhamiri ni nini?

Dhamiri ni nia ya kufanya jambo.

Watu wengi wana nia mbaya tu Katika nafsi zao, hao wana dhamiri mbaya.
Inawezekana moyoni mwako unawaza mabaya tu, hutaki kuyawaza lakini uajikuta unayawaza, ndugu dhamiri yako inatakiwa kusafishwa kwa damu ya YESU KRISTO.

Ndugu, Omba maombi leo katika Jina la YESU KRISTO huku ukitumia damu ya YESU KRISTO kukusafisha dhamiri yako, ili uwe na dhamiri njema kuanzia sasa.

1 Yohana 1:7 "bali tukienenda nuruni, k**a yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na DAMU yake YESU, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote."

5. Damu ya YESU KRISTO inaleta ulinzi katika mwili, afya, familia, biashara, ndoa n.k kulingana na maombi ya mkristo mhitaji anayeomba.

Ufunuo 12:11 "Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa."

Hapa unahitaji tu kufanya maombi ili damu ya YESU KRISTO ifanye kazi k**a ulivyoomba katika maombi yako.

6. Damu ya YESU KRISTO hututakasa na kutufanya tuwe huru.

Waebrania 13:12 "Kwa ajili hii YESU naye, ili awatakase watu kwa DAMU yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango."

Damu ya YESU KRISTO hutakasa.

Kutakasa ni nini?
Kutakasa ni kuondoa uchafu na kufanya kitu au mtu au eneo kuwa safi kiroho.
Damu ya YESU KRISTO kwa maombi yako inaweza kutakasa eneo la mwili wako unalotaka litakaswe, afya, ndoa, nyumba, ardhi n.k

7. Damu ya YESU KRISTO hutufanya tukae ndani ya YESU KRISTO.

Yohana 6:54-56 " Aulaye mwili wangu na KUINYWA DAMU YANGU anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake."

Kuinywa Damu ya YESU KRISTO ni kutafakari uwezo ulioko ndani ya Damu YESU KRISTO na kuutumia huo uwezo ulio ndani ya damu katika damu ya YESU KRISTO.
Pia ni muhimu kujua kwamba Mtu ambaye ameula mwili wa KRISTO na kuinywa damu yake ile iliyomwagika msalabani, ni yule ambaye anakaa ndani ya YESU KRISTO, na YESU KRISTO anakaa ndani yake.

8. Damu ya YESU KRISTO imetununua tuliokoka ili tuwe wa MUNGU kwa ajili ya uzima wa milele.

Matendo 20:28 "Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo ROHO MtakaTtifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, alilolinunua kwa DAMU YAKE mwenyewe."

Biblia inasema MUNGU ametununua sisi Kanisa kwa damu yake, hiyo ni kupitia YESU KRISTO Mwokozi wetu.

9. Damu ya YESU KRISTO hutufanya tuhesabiwe haki mbele za MUNGU.

Warumi 5:9 "Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika DAMU yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye."

10. Damu ya YESU KRISTO huleta ukombozi kwetu tuliompokea YESU KRISTO k**a Mwokozi wetu.

Waefeso 1:7 "Katika yeye huyo, kwa DAMU yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake."

Yako maeneo yako mengi yanahitaji ukombozi wa damu ya YESU KRISTO, kazi yako ni kufanya maombi ya ukombozi na damu ya YESU KRISTO itakukomboa.
Damu ya YESU KRISTO huleta ukombozi.

1 Petro 1:18-19 " Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa DAMU YA THAMANI, k**a ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya KRISTO."

11. Damu ya YESU KRISTO hutufanya tuwe karibu na YESU KRISTO.

Waefeso 2:13 "Lakini sasa, katika KRISTO YESU, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa DAMU yake KRISTO."

12. Damu ya YESU KRISTO hunena mema.

Waebrania 12:24 "na YESU mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili."

Ni jukumu lako tu kuishi maisha matakatifu ya Wokovu na kuomba katika jina la YESU KRISTO ukiomba damu ya YESU KRISTO inene mema na itanena.
Inawezekana unasemwa vibaya sana na Watu, Omba damu ya YESU KRISTO inene mema kwako.
Inawezekana unataka damu ya YESU inene mema kwenye ndoa yako, biashara yako, afya yako, kibali chako, kazi yako, mwili wako, Familia yako, Ardhi yako n.k
Ndugu Omba na damu ya YESU KRISTO itanena mema.

Ndugu, husika na YESU KRISTO na damu yake kwenye maisha yako.
Warumi 6:22 "Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa MUNGU, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.'
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.

Asante k**a umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU K**a Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.

Ubarikiwe.

Address

Muhuta

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Neema ya Kristo ya tosha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Neema ya Kristo ya tosha:

Share